Tanesco kwa nini mbagala siku za jumamosi umeme huwa lazima asubuhi ukatike mnarudisha jioni. Kwa nini jumamosi mnatuhudhi sana. Sir wengine weekend ndo siku za kutulia nyumbani na familia zetu. Mnatuboa.
Sent using
Jamii Forums mobile app
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA UMEMEMKOA WA TEMEKE
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Temeke kuwa kutakuwa na kazi ya matengenezo ya njia ya ya msongo mkubwa wa 132kv, kubadilisha nguzo zilizooza na kufanya maboresho kwenye transforma, iliyolenga kuimarisha ubora na upatikanaji wa umeme, Siku ya Jumamosi, tarehe 09 sept, 2017 kuanzia saa 02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 jioni
Kutokana na matengenezo hayo baadhi ya maeneo yatakosa umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Eneo lote la mkuranga, Yombo maguruwe, Tandika nyamwera, Dovya, Njia panda ya mwinyi, Kilakala, Mabomba nane, Mwisho wa rami, yombo Chalinze, yombo Malawi, Tandika maguruwe, Kisiwani sandali, Buza, Yombo vituka, Mashine, Mbagala kichemchem, Kibondemaji, Zakhem, Kizuiani, Rangi tatu, Mbande, hospitali ya Rangi tatu, mbagala mission, kibangulile, Mgeni nani, Kipati, Makuka, njia ya jeshini, Mbagala sabasaba, Toangoma, Kongowe, ukumbi wa Darlive, Am steel, East afrc polybagy, Maweni industry, Colourful ltd,
Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:
Dawati la dharura Mkoa wa Temeke 0714485488, 0783360411, 0765654767 au
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400/0768 985 100.
Tovuti:
www.tanesco.co.tz
Mitandao ya kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu
Barua pepe:
customer.service@tanesco.co.tz
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
08/09/2017
TANESCO Makao Makuu
Huduma kwa Wateja
Simu: 0768985100/0222194400
Barua pepe:
customer.service@tanesco.co.tz
Tovuti:
www.tanesco.co.tz
Mitandao ya kijamii
www.facebook.com/tanescoyetu
www.twitter.com/tanescoyetu
TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO