TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
3997d64ef2aec626aa376ee92cea3759.jpg


Katika maonyesho ya Wahandisi Wanawake TANESCO tumekuwa namba moja


Asanteni

TANESCO
MAKAO MAKUU
HUDUMA KWA WATEJA
Kituo cha miito:0768985100 AU 022 2194400
Barua pepe:customer.service@tanesco.co.tz
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.twiter.com/tanescoyetu
www.facebook.com/tanescoyetu
 
Habari za mihangaiko wakuu.

Tanesco kuna tatizo gani?? Huku Goba mpakani umeme umekatika muda mrefu toka mchana hadi sasa hivi bado tuko kwenye giza.

Fanyeni haraka tuweze kuwa katika mwanga, hili giza ni hatari sana aisee, yaani hadi kakimeo changu kana charge 4% tu kakizima ndio basi tena.

Please Tanesco, rejesheni umeme bana au mnasubiri kutajwa kwenye ripoti ya Makinikia na Almasi??
Tanesco kuna matatizo mengi to, kikubwa ni kuwaombea watekeleze majukumu yao vyema.
 
Ahsante mkuu,
Washaurejesha aisee, kimeo changu kiliisha charge tangu saa moja nikalala moja kwa moja kwa hasira, sasa ndio nimeshtuka nikakuta usharejeshwa
safii

Sent from my iDevice using Tapatalk
 
Tanesco kwa nini mbagala siku za jumamosi umeme huwa lazima asubuhi ukatike mnarudisha jioni. Kwa nini jumamosi mnatuhudhi sana. Sir wengine weekend ndo siku za kutulia nyumbani na familia zetu. Mnatuboa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco kwa nini mbagala siku za jumamosi umeme huwa lazima asubuhi ukatike mnarudisha jioni. Kwa nini jumamosi mnatuhudhi sana. Sir wengine weekend ndo siku za kutulia nyumbani na familia zetu. Mnatuboa.

Sent using Jamii Forums mobile app
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA UMEMEMKOA WA TEMEKE

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Temeke kuwa kutakuwa na kazi ya matengenezo ya njia ya ya msongo mkubwa wa 132kv, kubadilisha nguzo zilizooza na kufanya maboresho kwenye transforma, iliyolenga kuimarisha ubora na upatikanaji wa umeme, Siku ya Jumamosi, tarehe 09 sept, 2017 kuanzia saa 02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 jioni

Kutokana na matengenezo hayo baadhi ya maeneo yatakosa umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Eneo lote la mkuranga, Yombo maguruwe, Tandika nyamwera, Dovya, Njia panda ya mwinyi, Kilakala, Mabomba nane, Mwisho wa rami, yombo Chalinze, yombo Malawi, Tandika maguruwe, Kisiwani sandali, Buza, Yombo vituka, Mashine, Mbagala kichemchem, Kibondemaji, Zakhem, Kizuiani, Rangi tatu, Mbande, hospitali ya Rangi tatu, mbagala mission, kibangulile, Mgeni nani, Kipati, Makuka, njia ya jeshini, Mbagala sabasaba, Toangoma, Kongowe, ukumbi wa Darlive, Am steel, East afrc polybagy, Maweni industry, Colourful ltd,

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:

Dawati la dharura Mkoa wa Temeke 0714485488, 0783360411, 0765654767 au
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400/0768 985 100.

Tovuti:www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Barua pepe:
customer.service@tanesco.co.tz

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
08/09/2017

TANESCO Makao Makuu

Huduma kwa Wateja

Simu: 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz

Tovuti:www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook.com/tanescoyetu

www.twitter.com/tanescoyetu

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO
 
Tulinunua umeme kwa mpesa, tukapata token bila shida ilikua ni tarehe 19/08/2017

22124324272
Rcpt MAXCO33EMDB68126462
Units 22.5KWH

Token 7311 6177 2500 8893 4095

Cost TZS 6557.38
Serv Charge TZS 0.00
Tax TZS 1442.62
Total TZS 8000
eSign

Ila uligoma kuingia meta ikisema TOKEN USED.

TUkapiga mpesa wakatuelekeza tuwapigiwe. Basi tukawapigia nikaambiwa niende mbezi kibanda cha mkaa pale kwenye ofisi zenu.

Nilipokelewa vizur kontena la kwanza getini emergency mpaka nikajiona mfalme. (Hongera kwa wale madada)

Ila nikelekezwa kontena jingine pale nikakutana na muhudumu kizaazaa... (Ni mpuuzi)


Ila tatizo ni kwamba mpaka leo hii hatujabadilishiwa token mpaka imekua shida.





Sent from my Nokia ya Tochi using JamiiForums Mobile app
 
Tulinunua umeme kwa mpesa, tukapata token bila shida ilikua ni tarehe 19/08/2017

22124324272
Rcpt MAXCO33EMDB68126462
Units 22.5KWH

Token 7311 6177 2500 8893 4095

Cost TZS 6557.38
Serv Charge TZS 0.00
Tax TZS 1442.62
Total TZS 8000
eSign

Ila uligoma kuingia meta ikisema TOKEN USED.

TUkapiga mpesa wakatuelekeza tuwapigiwe. Basi tukawapigia nikaambiwa niende mbezi kibanda cha mkaa pale kwenye ofisi zenu.

Nilipokelewa vizur kontena la kwanza getini emergency mpaka nikajiona mfalme. (Hongera kwa wale madada)

Ila nikelekezwa kontena jingine pale nikakutana na muhudumu kizaazaa... (Ni mpuuzi)


Ila tatizo ni kwamba mpaka leo hii hatujabadilishiwa token mpaka imekua shida.





Sent from my Nokia ya Tochi using JamiiForums Mobile app
Tunaomba namba yako ya simu mpendwa mteja

TANESCO Makao Makuu

Huduma kwa Wateja

Simu: 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz

Tovuti:www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook.com/tanescoyetu

www.twitter.com/tanescoyetu

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO
 
Mmekata umeme huku kwa bi mkubwa wangu KIGAMBONI tangu asubuhi naambiwa kila ikifika J
MOSI lazima mkate mnarudisha usiku.
si mseme kama mmezidiwa m'bebwe[emoji196] [emoji84]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani kwa mara nyingne tena narudi kulalamikia mradi wa umeme uliofanywa na Tanesco mwaka 2014 katika kijiji cha kwekitui kata ya mamba tarafa ya Soni wilayami Lushoto mkoaniTanga.

Inasikitisha kuona mpk leo mradio huo amabo ulianza toka mwaka 2009 haujakamilika umetengenezwa nusu nusu.

Nasema nusu nusu kwa kuwa bado kuna nguzo zimesimama tu bila waya na kwa idadi ni nguzo nane hazina waya zimesimama takriban mwaka wa ili unaisha. tunaomba kujua tatizo ni nini?

Kama ni uzembe wa mtu mmoja kwa nini asiwajibike
Kama mkishindwa mseme ili tuende ngazi za Juu zaidi mpk tujue mwisho wake.

Naomba msaada wenu.

Simu 0 6 5 5 0 4 8 3 0 2.
 
Back
Top Bottom