Story za watu hapa jf na social media kulalamika umeme kukatikakatika ila kwa mwanza haikuwepo mpaka nikafikia hatua nikajua ni ya majizi,mapiga deal na yenye vyeti fake yanaongea uongo ili serikali hii inayojali wanyonge ionekane haifanyi kitu na kiuhakika niliungana na Rais wetu mpendwa,Musa wetu anayetupeleka Kanaani nchi ya ahadi katika ku ya enjoy hayo majizi yakilalamika
Sasa bwana,hii week iliyopita hadi leo ni timbwili katika jiji hili liliolompa DR JPM Urais,tunakatiwa umeme balaa,10 minutes ago wamekata,jana walikata asubuhi hadi jioni,siku tatu zilizopita mfululizo wanakata usiku kucha
TANESCO jamani,Hii ni Mwanza,hizo katakata zenu za umeme kafanyeni kimara na Moshi
Kuweni na human face pande hizi,eboooo.