TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kuna tetesi kuwa kufuatia kuanza kuvunjwa kwa ofisi zenu.ubungo,kutakuwa na uhaba wa luku units. Nimejaribu leo kununua kwa mpesa naona kweli imegoma na hela imeeudi, je ni kweli?
 
Kuna tetesi kuwa kufuatia kuanza kuvunjwa kwa ofisi zenu.ubungo,kutakuwa na uhaba wa luku units. Nimejaribu leo kununua kwa mpesa naona kweli imegoma na hela imeeudi, je ni kweli?
Ndugu mpendwa mteja
Hakuna usahihu wowote wa tetesi zako tunakusii endelea kupokea taarifa rasmi kutoka vyanzo vyetu rasmi na sio kwa kila mtu
 
Ndugu mpendwa mteja
Hakuna usahihu wowote wa tetesi zako tunakusii endelea kupokea taarifa rasmi kutoka vyanzo vyetu rasmi na sio kwa kila mtu
Sawa,lakini mpaka muda huu nimeshindwa kununua umeme kwa mpesa na nilipo hakuna maxi malipo wala selcom. Kuna uhusiano na hizo tetesi?
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linakanusha Taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikiwataka Wateja kununua Umeme kwa wingi kutokana na zoezi linaloendelea la kubomoa Ofisi za Makao makuu ya TANESCO hivyo kupelekea kuathirika kwa mfumo wake wa LUKU.

Tunaomba Wateja wetu wapuuze taarifa hiyo, kwani TANESCO kama ilivyobainisha katika taarifa ya awali , huduma zote za umeme ikiwemo ya manunuzi ya LUKU zitaendelea kama kawaida .

Tutaendelea kutoa taarifa kila inapohitajika.

Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: -

Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd

twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
Novemba 27, 2017
 
Kwanini mmekata umeme tokea saa 4 asubuhi leo hadi sasa haujarudi? Ni Mbezi Beach. Jana mchana hivyo hivyo. Juzi pia. Kwanini inakuwa kila siku sasa umeme unakatika ghafla bila taarifa? Sababu ni nini?
 
Mimi nawashauri muanzishe mfumo wa kuwafungia umeme baada ya kulipa nusu ya gharama halafu nyingine mtu amalizie kwa muda wa miezi kadhaaa baada ya kufungiwa maana mtu hatakubali kukatiwa, na mtapata wateja wengi tu au mtu kama ana nia na anahitj umeme mfungieni alipe taratibu baada ya muda wa hata miezi mi3.

Fanyeni hii km kweli mnataka kukuza wigo wa mapato na huduma.Asante
 
Malalamiko yangu ni kwamba nimelipia umeme tarehe 8 Nov 17 lakini hadi leo sijawekewa umeme na waliolipia mbele yangu wanawekewa umeme na kila nikiwafuata wananiambia kesho tutakuja kwanini mnakua wasumbufu kwa wateja wenu tatizo lipo wapi??
 
Naomba kufahamishwa,taratibu za kuvuta umeme zikoje, nilipo zinatakiwa nguzo tatu, last week nilienda ofc za tanesco MKOA, nikauliza majibu yake mpaka Leo sielewii.

Wanadai, nguzo mi bure sema zimeisha, lakin naona majirani zangu, nguzo zinachimbiwa, tofauti yangu NA majirani zangu wao ni wanajeshi, mi mkulima WA kilimo cha kujikimu..
 
Naomba kufahamishwa,taratibu za kuvuta umeme zikoje,nilipo zinatakiwa nguzo tatu,last week nilienda ofc za tanesco MKOA,nikauliza majibu yake mpaka Leo sielewii..
Wanadai,nguzo mi bure sema zimeisha,lakin naona majirani zangu,nguzo zinachimbiwa,tofauti yangu NA majirani zangu wao ni wanajeshi,mi mkulima WA kilimo cha kujikimu..
3c6040cdc9411c2cc4437f7a4f073830.jpg
 
Kwanini mmekata umeme tokea saa 4 asubuhi leo hadi sasa haujarudi? Ni Mbezi Beach. Jana mchana hivyo hivyo. Juzi pia. Kwanini inakuwa kila siku sasa umeme unakatika ghafla bila taarifa? Sababu ni nini?
Umeme umerejea kama kwako badomtunaomba namba yakomya simu
 
Mimi nawashauri muanzishe mfumo wa kuwafungia umeme baada ya kulipa nusu ya gharama halafu nyingine mtu amalizie kwa muda wa miezi kadhaaa baada ya kufungiwa maana mtu hatakubali kukatiwa,na mtapata wateja wengi tu au mtu kama ana nia na anahitj umeme mfungieni alipe taratibu baada ya muda wa hata miezi mi3.Fanyeni hii km kweli mnataka kukuza wigo wa mapato na huduma.Asante
Mteja anaruhusiwa kulipa kwa awamu tatu lakini atafungiwa mara baada ya kumaliza malipo yote
 
Umeme umerejea kama kwako badomtunaomba namba yakomya simu
Bado haujarudi. Sielewi kwanini mnakata kila siku. Leo ndiyo umekatika muda mrefu kuliko siku nyingine. Kama mgao umeanza kwanini msitutaarifu ili tujipange? Kwa kweli imekuwa kero kubwa sana umeme kukatika ghafla tu bila taarifa siku mfululizo.
 
Tanesco bhanaa. Nimesikia Leo mnajinasibu kuwa mnatekeleza agizo la mh rais. Nikacheka Sana.

Nikajiuliza.
Mnatekeleza agizo la mh rais au mnatekeleza sheria ya nchi?
 
Tanesco bhanaa. Nimesikia Leo mnajinasibu kuwa mnatekeleza agizo la mh rais. Nikacheka Sana.
Nikajiuliza.
Mnatekeleza agizo la mh rais au mnatekeleza sheria ya nchi?
Kwa mujibu wa sheria ya aridhi ya mwaka 1999 kifungu cha 3 rais ndiye mwenye mamlaka dhidi ya aridhi kwa niaba ya Watanzania wote hivyo pamoja na kuwepo sheria yeye anaweza kuamua kubadili matumizi ya aridhi kutoka matumizi aina mojamkwenda nyingine
 
Hivi gharama ya nguzo ni sh ngapi na unatakiwa ku lipia cjui survey mfano longido arusha hatujui taratibu za tanesco
 
Kwa mujibu wa sheria ya aridhi ya mwaka 1999 kifungu cha 3 rais ndiye mwenye mamlaka dhidi ya aridhi kwa niaba ya Watanzania wote hivyo pamoja na kuwepo sheria yeye anaweza kuamua kubadili matumizi ya aridhi kutoka matumizi aina mojamkwenda nyingine
Na sheria ya kutokujenga ndani ya hifadhi ya barabara. HAINA NGUVU KWA RAIS.?
 
Kwa mujibu wa sheria ya aridhi ya mwaka 1999 kifungu cha 3 rais ndiye mwenye mamlaka dhidi ya aridhi kwa niaba ya Watanzania wote hivyo pamoja na kuwepo sheria yeye anaweza kuamua kubadili matumizi ya aridhi kutoka matumizi aina mojamkwenda nyingine
Hilo jengo la makao makuu ubungo ni la mtu binafsi au ni mali ya serikali?
Tuambieni ukweli tujue kama ni kodi zetu wananchi, maana ni haki yetu kujua...
 
Back
Top Bottom