TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kwa heshima na taadhima namuomba waziri mwenye dhamana ya nishati atutangazie mgao wa umeme na atupe ratiba ya mgao huo ili tuweze kujipanga kwa kujua tunahifadhi vipi vyakula vyetu na pia tuweze kuwapa appointments za uhakika wateja wetu wanaosubiri huduma zinazotegemea umeme. Muda huu umekatika huku kwetu na kwa sababu hakuna ratiba sijui utarudi saa ngapi na hata wateja wangu siwezi kuwapa appointments za uhakika.

Hakutakuwa na tatizo tukitangaziwa mgao wala sioni kama watanzania tunajali sana kutokuwa na umeme kwani tumeshazoea. Hofu yangu tu ni sera yetu ya viwanda ita-suffer sana.

Nategemea muheshimiwa waziri umenipata.
 
Huku Oyster Bay tayari wamekata. Tutatumia generator ila mawazo yangu yapo kwa watanzania wenzangu wa kipato cha chini pembezoni mwa jiji.
 
Huku dar toka tanesco walipoamriwa kulivunja jengo lao la ubungo basi imekuwa kama kisasi kila siku wanakata umeme, nadhani wanalipiza kisasi kwa mh. Raisi, kwa hiyo wakutumbuliwa hapa sijui awe nani

Jamaa wameamua kumjibu!!! Unaboa ofisi wanayopatia Ridhiki !!!! Hawawezi kukuacha hivihivi!!!! Ila tunaoumia ni sisi wananchi!!! Magu hawezi kuwaomba msamaha Kwa kubomoa ofisi yao.
Wito: Magu waombe msamahama tanesco ili wapunguze makali ya mgao!!! [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wamekata tena umeme aisee.toka juzi wanakata afu waziri alijigamba umeme kukatika itakua historia na ukikatika anajiuzulu naomba ujiuzulu leo ni siku ya tatu umeme unakatika na hamna maelezo ya kutosheleza.mm navyoona huu ni mgao tu.

Tanzania ya viwanda gani na umeme huu wa shida?hiyo hela ya kubomolea jengo la Tanesco si mngeimarisha huduma ya umeme?
 
Mitambo yetu inamifumo ya kujilinda yenyewe mara hitilafu itokeavyo.

Kuanzia leo tareh 1 tunaongeza 30mw kny grid kuu kisha January tunaongeza 30mw.....hivyo kama kwenu hakuna umeme kaangalieni cutout zenu.
 
Dar tayayari washakata Na kurudi hapo mpaka sa 12 jioni Na ukirudi watakata tene ....hapo sasa ndo utana Umeme wa makengeza ...mtaa ule umewaka mtaa huu umezima yaani shida tupu
 
anayetakiwa kutumbuliwa ni medard kalemani,jamaa alimtoa kwenye madini akamuundia wizara yake kumuepusha na balaa kwa kuwa aliwahi kuwa mwanaasheria wa nishati na madini,na anahusika kwa namna moja au nyingine kwenye mikataba,alikompeleka ndio balaa sasa

pia tanesco hujiendesha kwa ruzuku,maapato ya serikali yameshuka,haiwezi kuiwezesha tanesco,

pia ni mwana mpendwa mbunge wa chato,atamtumbuaje?sana sana watawavamia wakuu wa tanesco na kuwadhalilisha kwa kuwatumbua

wao wamelenga kupiga dili stiglers,wanasahau kwamba nishati ni suala tata
wamwombe radhi "Confehesemi mramba"
 
Mitambo yetu inamifumo ya kujilinda yenyewe mara hitilafu itokeavyo..
Kuanzia leo tareh 1 tunaongeza 30mw kny grid kuu kisha January tunaongeza 30mw.....hivyo kama kwenu hakuna umeme kaangalieni cutout zenu.
We kama ni kishoka bila shaka picha yako imebandikwa tanesco
 
Keki zilikuwa kwenye oven ndo hasara tayari hiyo.sasa najiuliza ni Tanzania gani ya viwanda tunayo ihubiri?toka juzi wanakata umeme tena masaa mengi....mhhh mm naona kama mambo sio mazuri huko.na hatujasikia taarifa yoyote toka Tanesco.yaan ndo tumejiajiri kwa hivi vitu vidogo vidogo but umeme sasa imekua issue
 
Back
Top Bottom