TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Mbona huku kwetu hawajaludisha.
Subiri, “wataludisha” next November!

Ama kweli ccm wana dhambi. Sasa wewe hata unavyoandika, haionyeshi kama ni mtu anayeweza kuifahamu haki yake, let it alone kuidai.
 
Inasikitisha na kuustaajabisha kuhusu mgao waumeme. Tangu asubuhi hakuna umeme ili hali viwanda vyetu vidogo vidogo vinahitaji umeme kwa jili ya maisha yetu ya kila siku.

Mtu ana kiwanda cha mbao na asubuhi anawaaga familia kuwa ifikapo jioni atawaletea matumizi ya siku kinyume chake anafika kazini na kukuta umeme hakuna mwisho wa siku anaitesa familia kwa kutowaletea matumizi ya kila siku.

TUMECHOKA TUMECHOKA. tuelezwe sababu ni nini?. Tunamkumbukka sana Prof, Muhongo. Wakati wake hapakuwapo na matatizo kama haya.
 
Mkuu jamaa hawajali mambo ya umeme ili mradi ccm inakubalika. Si umeona wanechukua kata ngapi?
Suala la wananchi kuipensa ccm ni la kisanyansi ,si lazima mpige kura dola itatumika
 
yaani hapa nacomment nikiwa gizani..
wameunyakua vup !
nasubiri kesho niufanyie timing ili ukirudi tu nichaji kiwanda changu cha TECNO..
 
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*

*TAARIFA YA KUANZA KUREJEA KWA UMEME *

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa umeme umerejea katika Mikoa yote Saa 07:11 Mchana isipokuwa Mkoa wa Mbeya kutokana na hitilafu iliyopo katika njia ya Mufindi.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Kwa mawasiliano zaidi

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd
twitter.com/

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

01/12/2017
Matapeli tu nyie
 
Mkuu pole umeandika kwa hisia sana. Vumilia hakuna namna. Wanasema serikali sikivu imekusikia.
 
Hivi kumbe mambo ya mgao bado yapo, sisi wa solarpower tunavuna tuu miale ya jua, nshasahau hata luku inanunuliwaje
 
Mmechoka mgao wa umeme Ila bado mnaipenda CCM hakika hatutoboi
 
Umeme umekatika tena kudadeki mzigo kwenye friji ukiharibika naenda kuchoma moto ofisi za ccm
 
Uchwara yuko busy kuinyoosha nchi. TUTANYOOKA TU! Na hili joto la December kama hali itaendelea kuwa hivi ya umeme wa kusua sua kazi ipo.

dah tabu tupu usiku hakulaliki na joto la dar sasaivi balaa umeme unakatwa ovyo ovyo tulitegemea maisha bora ila day to day afadhali ya juzi
 
Kumbe we ndo msemaji wa TANESCO! Pongezi zako mkuu
Mkuu siyo lazima niwe msemaji wa TANESCO
ni sawa na mawakili wanavyozijua sheria
lakini hawaingii bungeni kutunga sheria.
pia usisahau hili jamvi linaunganisha watu
wa kada zote.Week end njema.
 
Eti matamko ndo yatamaliza matatizo tuliyonayo ikiwemo hili la Umeme? Unaota wewe. Mmebaki kuangalia kila kitu kwa jicho la ushabiki. Na bado, for you deserve all the shit.

Watu wengine sijui mnatumia nini kufikiri? Wewe endelea kukumbatia ccm, halafu ukisubiri chadema watoe matamko ili ccm irekebishe swala la umeme. There you go! Way to think! Mtanyoroshwa tu hadi mpate akili
Hahahah
Braza acha hasira, nimeongea kawaida lkn umetumia nguvu sana
 
MAHANJU
Unapoandika jitahidi kufanya uchambuzi wa mambo unayoandika. Kuhusu suala la umeme, huoni jitihada zinazofanywa. Ule mradi wa stiglers george unazani utaingiza megawati ngapi katika gridi ya taifa? Tatizo vijana wa chadema kutamani jambo fulani litokee kama ndoto bila kuwekeza jitihada kufikia hiyo ndoto.
Watu wanataka umeme uwake sasa hiyo "hapa kazi tu" ni ya kuzuia mikutano ya CDM . Masaa 12 umeme hamna then unataka mtu asome hizo megawatt za kwenye makaratasi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Aco kila siku
Wakuu huu mgao wa umeme wa siri siri japo unaonekana kwa macho.. Nasema wa siri kwasababu huana maelezo ili watu tujipange kwa kununua ma generator.. Kwa mfano huku mbeya umeme ni kawaida kukatika sa mbili hasubuhi na kurudi sa tano usiku.. Ikumbukwe umeme kwa hii miaka ni muhimu sana kwa shughuli za viwanda vyetu vidogo vidogo kama saloon, welding n.k

Swali nnalo jiuliza ni nani wa kutumbuliwa kwa huu uzembe wa mgao wa umeme usio na kifani? Maana kama kutumbua kwenye sector ya umeme tumetumbua sanaaa hivi sahivi ni zamu ya nani!?

Na anayejua sababu ya i kukatika na huu mgao wa kutisha ni ipi?

nchi ya viwonder
Acheni uchochezi. Hakuna mgao wowote. Mbona umeme uko kila siku?.
 
Mwendokasi project imeishia njiani nw inatoa huduma mbaya wakati miundombinu yake aikuisha
 
Aco kila siku

Acheni uchochezi. Hakuna mgao wowote. Mbona umeme uko kila siku?.
Unaelelewa nini ukiambiwa mgao wa umeme ama unafikiri unagawiwa kama kwenye matenga ya nyanya.... Unabishiwa hodi mlangoni kwako... Jiongeze mkuu..
 
Back
Top Bottom