Mim nilijua Muhongo baada ya kuondolewa kwa maslahi ya wachache,Nchi itaingia gizani na kwel Nchi ipo gizani,sisemi kwa sababu ya ushabiki bali kutokana na utendaji wake,kwa ambao wana kumbukumbu nzuri mgawo wa umeme ulitia fora miaka ile Ngeleja ni Waziri wa Nishati na madini,akaondolewa kwa kashfa,ila nakumbuka Ngeleja alituambia mgawo wa umeme hautaweza kuisha kwa miaka hii ya karibuni,lakin alivyoingia Mhongo tulisahau hiyo adhaa,na ni miongoni mwa Mawaziri waliokuwa wanaojua wajibu wao kiutendaji;na wenye macho waliona hilo;lakin sasa tumerudi kule kule kwa akina Ngeleja,Msabaha na Karamagi;hii Nchi ukiwa mchapakazi utafanyiwa figisu figisu mpaka utaondolewa,pamoja na mabaya yake kama Mwanadam lakini mazuri yake ni mengi zaidi na yenye faida.Wizara ya Nishati na Madini ni wizara ambayo ni pasua kichwa lakini siku zote lakini Muhongo hakika aliimudu,tusitegemee jipya kwa sasa wakuu.