TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TAARIFA YA HITILAFU YA UMEME MKOA WA IRINGA

HABARI FEEDER YA KIHESA IMETOKA KWA EARTH FAULT NA OVER CURRENT MAENEO YALIYOATHIRIKA NI:- Majembe, Kihesa sokoni,Semtema, Mwachang'a, Mtwivila, Mkimbizi, T.T.C.L minarani, Changalawe, Nduli, Tumaini Chuoni.

Juhudi za kurudisha Umeme katika hali yake ya kawaida zinafanyika

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

TANESCO- Iringa
17/1/2018
 
je nafanyeje ikiwa natashuka kwenye T4 ikiwa matumizi yangu yatashuka chini ya unit 70 kwh
nafanya taratibu gani ili kushuka kwenda T4 ikiwa nitapunguza matumiz yangu yakiwa chin ya unit 70
 
Nyie Tanesco Manyoni mnakatakata mno Umeme, tatizo nn haswa? Kwa siku mnakata zaidi ya Mara tatu! Mtutangazie km kuna tatizo la Umeme bwana! Mtakuja kutuunguzia vitu vyetu
 
TANESCO/REA -Kisarawe...tunashkuru kutufikishia huduma ya umeme maeneo ya kati ya Mvuti na Chanika.

Naomba kujua lini mtatuwashia umeme...Kila kitu tayari hadi transformer ila hatujajua lini tutakwenda kulipia na kuwashiwa.
asant.
 
TANESCO naomba kujua inachukua siku ngapi kuunganishiwa umeme ukiwa umeshalipia (nguzo moja) maana nina mwezi lakini sioni kinachoendelea.. Niko mwanza nisaidieni
 
Tunakamilisha taratatibu za ndani kisha umeme utawaka
 
TANESCO naomba kujua inachukua siku ngapi kuunganishiwa umeme ukiwa umeshalipia (nguzo moja) maana nina mwezi lakini sioni kinachoendelea.. Niko mwanza nisaidieni
Siku 60 za kazi kama umezidi mita 30 mpaka 100
 
Samahani mimi nina mlalamiko ya miita mwaka watano huu nimeandika barua zaidi ya sita ilaaTatiazo langu halijawahii kushugulikiwa.

Tatizo nilifungiwa mita ya mashine ya zamani inaleta hesabu tofautti na uhalisia, nimbovu kwa ujumla. Ilifugwa kabla hata ya ujio wa luku. Mfumo wa luku ulipokuja wateja wote wa mita za zamani walibadilishiwa kasoro mimi. Nimeombahuduuma ya luku zaidi ya mara sita ila bila kufanikiwa.

Mimi ni Dennis Arthur wa mogitu pembeni ya shule ya msingi mogitu katesh hanang manyara tanzania.
Naomba msaada wenu wakuu.
0754627252
 
Napenda kufahamu kwamba kunatatizo gani la umeme kahama kwa siku mbili mfululizo umeme unakatwa asbh na kurudishwa jioni na inapendeza mkiwa mnatoa taarifi ili nasi wafanyabiashara tujipange kisaikolojia! Tatizo Nini na ili zoezi litafanyika kwa siku ngapi?
 
Tumepokea kwa ufatiliaji na hatua zaidi mkuu
 
Napenda kufahamu kwamba kunatatizo gani la umeme kahama kwa siku mbili mfululizo umeme unakatwa asbh na kurudishwa jioni na inapendeza mkiwa mnatoa taarifi ili nasi wafanyabiashara tujipange kisaikolojia! Tatizo Nini na ili zoezi litafanyika kwa siku ngapi?
MFUMO WA KUTUPATIA TAARIFA/LALAMIKO

1.JINA.....................................

2.SIMU....................................

3.MKOA...................................

4.WILAYA................................

5.MTAA/KIJIJI/KATA.........

6.JINSI YA KUFIKA................

7.KITU/ALAMA/MTU MAARUFU.............................

8.NAMBA YA MITA................

9.TATIZO LAKO/UNACHOHITAJI....................

10.NAMBA YA TAARIFA ULIYOPEWA.................

"TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO"
 
Dah umerudi. Asante tanesco
 
TANESCO boresheni huduma kwatunao nunua umeme kwenye simu

Mimi niko kanchi jirani nimependa sana mfumo wao wa kununua umeme kwa njia ya simu hivo ningependa hii huduma itumike hata kwetu iko hivi :-

Unapo fanya muamala kwa mara ya kwanza mtandao hukuhitaji kuweka namba mita ukisha kamilisha muamala wako namba inasajiriwa kwenye mufumo hivo kila ukitaka kununua umeme hautajitaji tena kuingiza namba ya mita utakuta jina lako unachagua unaendelea kufanya muama wako.

Mfano
758c5f1cac1c1068e11e9575c076fcb5.jpg

0ca4850c2988e9c64391b233bbbcd0d0.jpg

39d08e7fc5f6f96f600ffe2c26b11b16.jpg

3f6c48feb2de9dabea97e195732effe8.jpg

6248087427f765a8b1017199bd07a6eb.jpg

Nb. Hata ukitaka kuangalia umeme ulio nunua kwa mara ya mwisho unapata details zote kwa kupitia m pesa
 
Vp ule utaratibu uliokuwepo mwanzo wa kulipa deni kwa asilimia hamsini mara ununuapo umeme umesitishwa? Je ni utaratibu gani kwa sasa unatumika? Mimi naona utartibu ule wa mwanzo ndio uliokuwa unafaa kwani mteja analipa deni lake bila maumivu.
 
Back
Top Bottom