TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.

Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;
Ni lazima baada ya kulipia umeme kwa mteje asiyehitaji nguzo akae siku 30?
 
Utaratibu ni waliotangulia kulipia wanafungiwa umeme kwanza ndio anayefuata afungiwe inategemea sana na maeneo na wingi wa wateja
Ni lazima baada ya kulipia umeme kwa mteje asiyehitaji nguzo akae siku 30?
 
Kibugumo Kigamboni umeme umekatika, nimetoa tu taarifa. Na kila umeme ukikatika nitakujulisha, ili uone kama hiyo ni hali ya kawaida umeme kukatika so frequently and hapharzadly
Leo kulikuwa na hitilafu kidogo tunaifanyia kazi
 
Haijafutwa popote pale bali wateja wanawekwa makundi yanayoendana na matimizi yao
TANESCO mbona mnanipuuza??? Naomba mnibadilishe tariff nina matumizi madogo.. Msinipuuze na mimi ni mteja wenu.. Namba ya mita 54182960069
 
TANESCO mbona mnanipuuza??? Naomba mnibadilishe tariff nina matumizi madogo.. Msinipuuze na mimi ni mteja wenu.. Namba ya mita 54182960069
Upo kundi sahihi la matumizi ya nyumbani mpendwa mteja endelea kufurahia huduma
 
Mkuu, narudia mara ya tatu kuuliza. Mimi ni mkazi wa Kivule, nimelipia huduma ya kuwekewa umeme tangu mwezi August 18 mpaka sasa hatuna kitu. Pia nimeambiwa nisifike ofisi za tanesco UKONGA ila nitapigiwa simu, kwamba foleni ni kubwa. Hii ni sawa?
Upo kundi sahihi la matumizi ya nyumbani mpendwa mteja endelea kufurahia huduma
 
Nona huwa hamuoni/ huzioni sms za pm. Hii ni mara ya pili hakuna majibu
Wanachagua wa kuwajibu mkuu, nimepost zaidi ya mara nne. Jana nimevizia wakiwa hewani, lakini hawanijibu. Ukitaka ujibiwe haraka weka post zinazilosrma, "Nanjilinji mtaleta lini umeme." Yaani maswali ya ujumla tu, sio matatizo yanayolenga ofisi.
 
Nauliza . Hivi usiponunua umeme unaweza kubadilishiwa tarrif ?
Kama ni Ndiyo kwa nini?
 
Niliulizwa juu ya mkoa wa kilimanjaro kwanini mnawabadilisha wateja tariff 4 na kuwarudisha kwenye tarif 1 naomba ufafanuzu
 
Wanachagua wa kuwajibu mkuu, nimepost zaidi ya mara nne. Jana nimevizia wakiwa hewani, lakini hawanijibu. Ukitaka ujibiwe haraka weka post zinazilosrma, "Nanjilinji mtaleta lini umeme." Yaani maswali ya ujumla tu, sio matatizo yanayolenga ofisi.
[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] powa kiongozi
 
Mpendwa mteja tulikujibu swali hili kuwa kina uhakiki wa makundi ya watumiaji wateja nchi nzima hivyo kila mtena anakaa kundi linaloendana na matumizi yake
Niliulizwa juu ya mkoa wa kilimanjaro kwanini mnawabadilisha wateja tariff 4 na kuwarudisha kwenye tarif 1 naomba ufafanuzu
 
Back
Top Bottom