Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Je umeme umefika kwenye makazi yakoNaomba kuuliza mm nimeomba umeme sasahivi ni mwaka unaisha kila nikienda naambiwa nguzo hamna zikija ntapigiwa simu nikalipie ndo nije kufungiwa . je hii ni sawa?? Mm sehem yangu ni nguzo moja na ni kijijini umeme ntakaofungiwa ni wa rea. Nashindwa kuelewa kwann nisubirishwe mda mrefu hivi??
Alipofika alikuambiaje? Jina lako namba ya simu na wilaya gani tafadhaliUmeme kwenye makazi yaliyonizunguka upo ni hatua 60 kutoka kwangu ndo umeme ulipo na savea kashafika kwangu mara 2 ila sijapata umeme. Naomba msaada tafadhali.
Nguzo haziuzwi tafadhali kamilisha wiring kisha njoo chukua fomu tupime na kukupatia gharama halisi
Ahsante kwa taarifaTANESCO MASASI NI TATIZO KUBWA NA WALA SIWEZI KUMSHAWISHI MTU KUFANYA SHUGHULI YOYOTE YA UZALISHAJI INAYOTEGEMEA NISHATI YA UMEME.
Siyo kwamba Masasi ni eneo baya kuishi ama kufanya uwekezaji, la hasha, ni pazuri na panavutia mno kama mtu una nia ya kujiongezea kipato chako na hata cha taifa kwa ujumla. Ila kwa muda mdogo niliokaa eneo hilo nimegundua kuwa bado kuna tatizo la ugavi wa nishati ya uhakika ya umeme.
Mazingira ya wilaya hii pia yanathibitisha kuwa hapo awali kulikuwa na shida kubwa ya maji maana asilimia ya nyumba nyingi za bati zina vikinga mvua ili pindi mvua ikinyesha basi watu wapate maji ya mvua m, lakini si haba sasahivi jitahada ya mamlaka ya maji katika eneo hilo inaonekana. Huduma ya maji inazidi kuimarika siku hadi siku.
Matatizo huanza pale umeme wa Tanesco unapokatwa na mitambo ya mamlaka ya maji (MANAWASA) pia hulazimika kuzimwa ndipo hapo wananchi pia hukosa maji. Umeme wa Masasi ni zima waka zima waka na muda mwingi huwa ni low voltage kwahiyo iwapo una mtambo unaoendeshwa kwa nishati ya umeme basi kwa eneo hili la Masasi hesabu kama imekula kwako.
Sijui wawakilishi wa wananchi katika bunge la jamhuri ya muungano wanalichukuliaje suala hili, au waandishi wa habari wanafanya nini ili ujumbe umfikie raia namba moja pale ikulu Dodoma, je wataalam wa Tanesco wanawasaidiaje watu wa Masasi?
Masasi kuna shida ya umeme ndugu zangu Watanzania tunaomba serikali iliangalie eneo hilo, litengewe fungu la pesa na tatizo la umeme libaki historia ili watu wa eneo hilo pia wayafurahie matunda ya neema ya nchi yao.
Ni eneo gani? Wilaha gani namba ya simu tafadhaliKama mnasema nguzo haziuzwi mm ktk eneo langu umeme nauona karibu sana na savea walishafika wakatathimini nakuona zinahitajika nguzo mbili kutoka na kuwa nipo pembeni kdg ya barabara zilimopita nguzo lakini toka mwezi wa nane hakuna kilichofanyika kwann mtu msimweleze tu ukweli akatafuta namna ya kupata umeme mbadala maana ktk nyumba umeme ni wa muhimu sana ktk ulinzi wa nyumba nakosa ni wapi nikalalamike nikija humu mnaniambia niweke namba na mahali nilipo lkn kushughulikia ni hakuna ,, tanesco mnakwama wapi mbona mnatoa huduma kwa upendeleo?
Tunashukuru kwa taarifa maeneo mengieo yalikumbwa na changamoto ya mvua kubwa iliyolega adhari kwenye miundombinu ya umeme.Tafadhali onyesha eneo simu na tatizo kwa hatua zaidiTanesco Kinondoni Mnazingua sana aisee, Leo tangu asubuhi eneo la Tandale chama kumetokea shoti ya umeme kuna maeneo mengine hayana umeme
Tunapiga simu tangu asubuhi ipo bize na inapopokelewa hamsemi chochote
Kutiana hasara tu mnaboa sana
Nipo halmashauri ya buchosa mkoa wa mwanza na mawasiliano yangu ni 0768145634Ni eneo gani? Wilaha gani namba ya simu tafadhali
TANESCO sijui umefikia wapi na kuifanyia kazi suala la Umeme Kimara mwisho? Leo jtano ndio mmetia fora aisee umeme unakaa saa moja halafu unakatwa tena saa nzima. Hii sijui ni mara ya ngapi unakatika.. Countless time. Hebu niambie Kimara mwisho kuna nini? Kwanini historia ya huduma ya umeme kimara sio nzuri kabisa? Na umeme unakatwa huko huko Ubungo. Last time nimepiga simu naambiwa kuna shida control room. Kwanini msiondoe hiyo mitambo mibovu mkatufungia mitambo yenye uwezo wa kubeba load ya sasa hivi wilaya hii ya kibamba? Mji huu unakua inabidi na nyinyi muongeze uwezo kuendana na ongezeko la matumizi ya umeme. napita hapa udart kote hakuna umeme, hivi mnajisikiaje TANESCO?Tunashukuru kwa taarifa tunaifanyia kazi tafadhali
Tunatambua changamoto za eneo husika tunachukua hatua stahikiTANESCO sijui umefikia wapi na kuifanyia kazi suala la Umeme Kimara mwisho? Leo jtano ndio mmetia fora aisee umeme unakaa saa moja halafu unakatwa tena saa nzima. Hii sijui ni mara ya ngapi unakatika.. Countless time. Hebu niambie Kimara mwisho kuna nini? Kwanini historia ya huduma ya umeme kimara sio nzuri kabisa? Na umeme unakatwa huko huko Ubungo. Last time nimepiga simu naambiwa kuna shida control room. Kwanini msiondoe hiyo mitambo mibovu mkatufungia mitambo yenye uwezo wa kubeba load ya sasa hivi wilaya hii ya kibamba? Mji huu unakua inabidi na nyinyi muongeze uwezo kuendana na ongezeko la matumizi ya umeme. napita hapa udart kote hakuna umeme, hivi mnajisikiaje TANESCO?