TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tunatambua changamoto za eneo husika tunachukua hatua stahiki
Tunaomba sana mtusaidie huduma ya umeme iwe stable. Umeme ni uti wa mgongo wa uchumi wa watu wengi huku mijini.Tusaidieni Kimara na maeneo mengine yote ya Dar tuwe na huduma ya umeme ya uhakika. Tunatumia sana umeme. TANESCO ,
Nashauri muuchukulie mkoa wa Dar kama eneo maalum lenye kipaumbele maalum.
 
Jana nimetoa Malalamiko yangu kwenye special thread ya TANESCO lakini sijajibiwa, na leo jamaa wameanza kukata tena umeme bila taarifa. Hii ni kero kubwa sana.Lkn tarehe 28,najua cha kufanya,maana bila kushituliwa hata kidogo hamuwezi kushituka.
 
Tanesco leo mafinga kuna nini mbona mnakata sana umeme mkinichomea vyombo nawashtaki
 
Jana nimetoa Malalamiko yangu kwenye special thread ya TANESCO lakini sijajibiwa, na leo jamaa wameanza kukata tena umeme bila taarifa. Hii ni kero kubwa sana.Lkn tarehe 28,najua cha kufanya,maana bila kushituliwa hata kidogo hamuwezi kushituka.
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka saa ngapi

Kwa hatua zaidi
 
Hivi hizi namba zenu za emergency 0715768589/0684001068 zina watu maalum ambao mnawapokelea au huduma inawaelemia maana hata ukipiga una serious problem haipokelewi...
Sasa Kama mna upungufu wa watumishi toaeni ajira hapo emergency maana ufanisi wa kazi unapungua
 
Umelipa lini kwa jina gani namba ya simu tafadhali
Ndugu, naona suala langu imekuwa gumu kufanyiwa kazi, badala yake 'napigwa viswahili' tu.

Naomba unisaidie tu namba za headquarters nifuatilie huko, maana hawa watu wenu hapo Mlandizi ni kama wanachukulia poa!
 
Back
Top Bottom