SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
DESEMBA 17, 2020
TAARIFA YA MATENGENEZO KATIKA VITUO VYA KUZALISHA UMEME VYA KIDATU, KINYEREZI II NA SONGAS.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kuna matengenezo katika Kituo cha Kufua Umeme kwa maji cha Kidatu na Vituo vya Kufua Umeme kwa Gesi Asilia vya Kinyerezi II na Songas.
Kutokana na matengenezo hayo, baadhi ya maeneo nchini yataathirika kwa kukosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti.
Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi kuhakikisha mashine zinatengemaa haraka.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza
Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au kudondoka chini.
Toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu nawe, au wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: - Kitengo cha Miito ya Simu 0222194400 na 0768 985100
Mitandao ya Kijamii :
Website:
www.tanesco.co.tz
Instagram: tanescoyetu
Barua pepe:
customer.service@tanesco.co.tz,
Twitter:
www.twitter.com/tanescoyetu
Facebook:
Tanesco Yetu
Imetolewa na;
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.