TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Mimi NIMELIPIA umeme tarehe 16/9/2020
Lakini Hadi leo hii Ni tarehe 22/12/2020 umeme SIJAUNGANISHIWA kila nikiwapigia simu WANANIPA kiswahil TU
NIMELIPIA 320,000.wanasema INAHITAJIKA nguzo moja tapping pole.
Wenzangu mtaan wanasema walilipia baada ya mwez mmoja umeme uliwaka.
TANESCO KISARAWE mmezid aiseee
Je umelipa kwa jina gani na namba yako ya simu tafadhali
 
Je umelipa kwa jina gani na namba yako ya simu tafadhali
EDWIN ILOMO
0765929586
KAKA INBOX TUMECHAT NA WEWEKARIBIA MWEZ HADI LEO KIMYA.KILA SIKU MNAFAUATILIA MNAFAUATILIA...

Sms ya malipo HIYO hapo
REF:FH621651600265579 EDWIN R. ILOMO. umefanikiwa kulipia Bill Number 607 BILL:991032056804 TZS320960 RECEIPT:920260009135546 be 2020-09-16 17:13:00
 
Tanesco mkoa wa tabora kuna shida gani.Maanake umeme mkikatani masaa 10 yanapita mkierudisha ni saa 1 moja mnakata tena kuna tatizo gani?! Tumejaribu kuulizia majibu tunayopewa ni zaidi yanyodo...
Hapa DSM ndio michezo yao kila siku
 
Tanesco mkoa wa tabora kuna shida gani.Maanake umeme mkikatani masaa 10 yanapita mkierudisha ni saa 1 moja mnakata tena kuna tatizo gani?! Tumejaribu kuulizia majibu tunayopewa ni zaidi yanyodo....
Nileteeni mwanachato mwenzangu Kalemani. Au nasema uongo ndugu zangu?
 
NYINYI TANESCO KIUKWELI HAMNA HATA CHEMBE YA UBUNIFU KATIKA UTENDAJI WA KAZI ZENU, HIVI MNAONA NI SAHIHI KUKATA MITI MJI MZIMA NA KUHARIBU MAZINGIRA KISA NYAYA ZA UMEME!? HIVI MMESHINDWA KUBUNI NJIA NYINGINE ILI KUOKOA UKATAJI HOVYO WA MITI MKIELEWA KUWA DUNIA IKO KWENYE JANGA KUBWA LA MABADILIKO YA TABIA NCHI AMBAYO WATU KAMA NINYI NDIO MLIOTUFIKISHA HUKO, NASHANGAA ETI KUNA WIZARA YA MAZINGIRA NAYO HAIONI UKICHAA HUU! Hii nchi imefikia pabaya.
 
NYINYI TANESCO KIUKWELI HAMNA HATA CHEMBE YA UBUNIFU KATIKA UTENDAJI WA KAZI ZENU, HIVI MNAONA NI SAHIHI KUKATA MITI MJI MZIMA NA KUHARIBU MAZINGIRA KISA NYAYA ZA UMEME!? HIVI MMESHINDWA KUBUNI NJIA NYINGINE ILI KUOKOA UKATAJI HOVYO WA MITI MKIELEWA KUWA DUNIA IKO KWENYE JANGA KUBWA LA MABADILIKO YA TABIA NCHI AMBAYO WATU KAMA NINYI NDIO MLIOTUFIKISHA HUKO, NASHANGAA ETI KUNA WIZARA YA MAZINGIRA NAYO HAIONI UKICHAA HUU! Hii nchi imefikia pabaya
Upo umbali kitaalamu unapaswa kuachwa kutoka kwenye miundombinu ya umeme
 
Na nyinyi nyumba zenu zingekuwa hazijafikiwa na miundo mbinu nadhani namba tungekuwa tunaisoma wote lkn kwa sasa mnaona ni vizuri tu kuwaambia wenzenu wakae kusubiri miundo mbinu iwafikie
 
Je kuna mpango gan kuboresha huduma ya umeme Wilaya ya Ukerewe ambayo inapokea umeme kutoka bunda kupitia ziwa Victoria (Kisorya-Ngoma) ambapo kumekua na shida kwenye marine CABLE kila wakt hali inayopelekea wakazi wa ukerewe kukaa hta wiki nzima bila umeme
 
Huduma yenu ya kuunganisha umeme majumbani na viwandani ni miongoni mwa huduma zenye gharama kubwa huenda kuliko huduma nyingine yoyote, hakuna aliye aliyewalazimisha kutoa huduma hiyo bali ninyi wenyewe mlijiona mnafiti kuwa kwenye nafasi hiyo sasa inapofikia mahali inaonekana kana kwamba mnatoa sadaka tambueni mnawakosea wateja wenu.

Furaha yenu ni ipi wakati mkatapo umeme si chini ya mara 4/5 kwa siku wakati kwa wiki ni siku 2/3 zenye umeme peke yake tena si wa uhakika.

Jambo hili limekuwa sugu hasa Shinyanga vijijini ambapo kutokana na shughuli za kilimo hasa mpunga kuna mashine nyingi za kukoboa mpunga na kupaki mchele ambao unasafirishwa nje ya nchi na kwa matumizi ya ndani.

Ni vema wasimamizi wa vituo wachunguzwe huenda wakawa wanafanya haya kwa ajili ya interest zao!
 
Nipo kijiji cha ngombezi,wilaya ya korogwe,mkoa wa Tanga,kuna waya una hatari sana umepita juu ya nyumba yetu,tumeenda tanesco wilaya hapa korogwe wamesema tuandike barua tumeandika lakini mwezi wa pili sasa kila tukifuatilia wanasumbua tu,waya ule unatoa cheche kila mara,vipi mpaka yatokee madhara ndio mtastuka?
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

DESEMBA 17, 2020

TAARIFA YA MATENGENEZO KATIKA VITUO VYA KUZALISHA UMEME VYA KIDATU, KINYEREZI II NA SONGAS.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kuna matengenezo katika Kituo cha Kufua Umeme kwa maji cha Kidatu na Vituo vya Kufua Umeme kwa Gesi Asilia vya Kinyerezi II na Songas.

Kutokana na matengenezo hayo, baadhi ya maeneo nchini yataathirika kwa kukosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti.

Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi kuhakikisha mashine zinatengemaa haraka.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au kudondoka chini.

Toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu nawe, au wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: - Kitengo cha Miito ya Simu 0222194400 na 0768 985100

Mitandao ya Kijamii :
Website:

www.tanesco.co.tz

Instagram: tanescoyetu

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz,

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook: Tanesco Yetu

Imetolewa na;
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.

Hamna lolote, nilichouliza sicho ulichojibu, acha kujibu maswali ya msingi kwa mazoea, jibu swali Langu, Kuna uhusiano gani Kukatika kwa Umeme na Wakati mvua ikinyesha ?
 
Nipo kijiji cha ngombezi,wilaya ya korogwe,mkoa wa Tanga,kuna waya una hatari sana umepita juu ya nyumba yetu,tumeenda tanesco wilaya hapa korogwe wamesema tuandike barua tumeandika lakini mwezi wa pili sasa kila tukifuatilia wanasumbua tu,waya ule unatoa cheche kila mara,vipi mpaka yatokee madhara ndio mtastuka?
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi

Tutumie taarifa hizo inbox
 
Huduma yenu ya kuunganisha umeme majumbani na viwandani ni miongoni mwa huduma zenye gharama kubwa huenda kuliko huduma nyingine yoyote, hakuna aliye aliyewalazimisha kutoa huduma hiyo bali ninyi wenyewe mlijiona mnafiti kuwa kwenye nafasi hiyo sasa inapofikia mahali inaonekana kana kwamba mnatoa sadaka tambueni mnawakosea wateja wenu.

Furaha yenu ni ipi wakati mkatapo umeme si chini ya mara 4/5 kwa siku wakati kwa wiki ni siku 2/3 zenye umeme peke yake tena si wa uhakika.

Jambo hili limekuwa sugu hasa Shinyanga vijijini ambapo kutokana na shughuli za kilimo hasa mpunga kuna mashine nyingi za kukoboa mpunga na kupaki mchele ambao unasafirishwa nje ya nchi na kwa matumizi ya ndani.

Ni vema wasimamizi wa vituo wachunguzwe huenda wakawa wanafanya haya kwa ajili ya interest zao!
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi
 
USHAURI
Anzisheni mfumo ambao mtu akinunua vocher/umeme unaingia moja kwa moja kwenye mita yake
Sioni hiyo technologia ikiwa ngumu/ghali; hata ma IT wa hapa ndani wanaweza kutengeneza na kama mnaona hawana viwango; nunueni hiyo program mbona ni ya kawaida sana hata mitandao ya simu inawapita;
1. Fikiria unawawekea umeme wazee kijijini na macho hayaoni vizuri etu wakaweke tarakimu 20 kutoka simu ya tochi?
2. Au pengine umeacha watoto nyumbani umeme unakatika; ni hadi wawe na simu na wajue kutumia nk
3. Umeme umekatika (usiku) sijui ndio ukatafute battery au uende kwa jirani kuomba ndio uweke; ukweli ni mambo ya mwaka 47- tumepitwa na wakati
Naomba mboreshe ili muondolee adha wateja

Point sana, binafsi mimi nakimashine chao cha kuingizia lkn batani zake sinasumbua kuingiza hizo token namba, yaani mpaka uje kumaliza kuweka ushalowana jasho, so wakifanyia kazi huu yshauri itasaidia sana.
 
EDWIN ILOMO
0765929586
KAKA INBOX TUMECHAT NA WEWEKARIBIA MWEZ HADI LEO KIMYA.KILA SIKU MNAFAUATILIA MNAFAUATILIA...

Sms ya malipo HIYO hapo
REF:FH621651600265579 EDWIN R. ILOMO. umefanikiwa kulipia Bill Number 607 BILL:991032056804 TZS320960 RECEIPT:920260009135546 be 2020-09-16 17:13:00
HATIMAYE JANA NDO WAMENIUNGANISHIA UMEME HAWA TANESCO....
 
TANESCO kuna shida gani Pugu? Hii ni wiki ya pili sasa kila siku umeme unakatika bila kutupa taarifa ya kina. Mpaka leo sikukuu muhimu sana Kitaifa na kimataifa mmekata umeme. Mnataka tunywe vinywaji vya moto? Huku joto ndani kukiwa hakukaliki. Kama kuna mgao semeni tujue ili tujioange kwa hili. Psychologically this is a big torture
 
Back
Top Bottom