Habari za Asubuhi.
Naanza kukosa imani na haya majibu yako unayotujibu humu ya kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
Hao wataalamu uliosema jana wapo Eneo la Tukio wamekuwa GHOST hawaonekani kwa macho au ama.
Yule mama nimeongea na Jana usiku anadai hakuna aliyempigia wala aliyefika pale, na alikaa barazani kwenye mkeka siku nzima akiwasubiria.
Mnamtesa mama wa watu buree.
Bora atoke akajitafutie Riziki zake za ukulima.
Sijaelewa uliposema ( WATAALAMU WAKO ENEO LA TUKIO SASA HIVI )
ni kwamba wewe umedanganywa na hao mafundi wa Bagamoyo au wewe umetudanganya sisi ? Wich is wich ?
Any way siku mkijisikia kuja mtakuja.
Mama wa watu simwambii tena akae akusubirieni , mtajijua wenyewe na kazi zenu mnafanyaje.
Mi nakaa kimya . Kazi njema nazodhani labda unazifanya hapo.