TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Naomba kujua gharama na hatua za kufuata unapotaka kufungiwa mita yako binafsi katika nyumba,au frame mlizo panga.

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
ZIJUE TARATIBU ZA KUFATA ILI KUFUNGIWA UMEME NA TANESCO

HATUA YA KWANZA (MAOMBI YA MWANZO

[emoji843]Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika ndani ya kanda yake bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

[emoji843]Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

[emoji843]Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

[emoji843]Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa na umekamilika (orodha zao zipo TANESCO)

[emoji843]Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, Kitambulisho cha taifa nk (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

[emoji843]Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa maandishi wa ruhusa ya mwenyenyumba. mteja anashauriwa kuja na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni. (kama mita ya awali ina deni hatoruhusiwa kuomba mita ya pili)

[emoji843]Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya husika.

[emoji843]Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika au la taasisi husika

[emoji843]Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

[emoji843]Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo:-

[emoji843]Kuisoma fomu ( Mkataba wa kufungiwa umeme baina ya mteja na TANESCO) kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja hadi kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

[emoji843]Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za TANESCO. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

[emoji843]Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

[emoji843]Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

[emoji843]Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana hapo chini:

Muda wa kupimiwa ka kupewa makadirio

[emoji843]Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu) Ndani ya siku 7 za kazi

[emoji843]Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100) Ndani ya siku 10 za kazi

[emoji843]Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)
Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya TANESCOA ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (Control Number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms).wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena TANESCO bali TANESCO watakuwa na taarifa zake zote kupitia mifumo kuwasiliana na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

[emoji843]Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu) mteja atafungiwa umeme ndani ya siku 30 za kazi

[emoji843]Kama ujenzi wa njia ya nyongeza utahitajika (mita 30- 100) mteja atafungiwa umeme ndani ya siku 60 za kazi

[emoji843]Kama mfumo mpya wa usambazaji utahitajika kujengwa au mfumo wa umeme mkubwa utahitajika kujengwa ( kama hakuna mfumo eneo husika) yaani zaidi ya mita 100 kutoka kwenye nguzo ya TANESCO mteja atafungiwa umeme ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA HUDUMA KWA WATEJA

[emoji338]Kituo cha huduma kwa wateja Makao Makuu: - 0768985100/0222194400

[emoji843]Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

[emoji843]Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

[emoji843]Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

[emoji843]Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz
[emoji843]WhatsApp za huduma kwa wateja Nchi nzima

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA ZETU

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO
 
ZIJUE TARATIBU ZA KUFATA ILI KUFUNGIWA UMEME NA TANESCO

HATUA YA KWANZA
(MAOMBI YA MWANZO

Asante sana

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
Unapaswa kutoa taarifa ofisi za eneo lako

Uchunguzi utafanyika kugundua chanzo cha tatizo na kama umekiuka matakwa ya maombi uliombea kisha taarifa itaonyesha chanzo na kama unastahili fidia au laa
Sawa...
 
TANESCO naomba mje hapa kitongoji cha lyalamu,kijiji cha Ilunda,kata ya mtwango,mkoa wa Njombe kwenye transformer yenu ya REA inaharibika kila wiki toka nifike hapa umeme unawaka siku 2 unakata siku 5 nadhani machine yenu inatatizo LA kujizima ghafla mafundi wakija wanatengeneza lakini tatizo linajirudia,na mwezi uliopita waliwachangisha wakazi wa hapa Tsh 3000 kila mmoja wawalipe mafundi wenu lakini still umeme bado unazingua ,nadhani tumeelewana msaada unahitajika sababu ni kero sana!
 
Ahsante kwa taarifa tafadhali onyesha namba ya simu kwa hatua zaidi
 
Mtu akitaka kuunganisha kwenye nguzo uliyo nunua tanesco unafanyaje?
Mteja hanunua nguzo wala mita bali analipia gharama ya kuunganishiwa umeme ( service line connectiom fee) hivyo umiliki wa mteja unaanzia baada ya mita kwenda ndani kuanzia mita kwenda nje ni miindombinu ya TANESCO
 
Tanesco mbona mna kata kata Sana umeme huu mtaa wa Tabata Mangumi, Sanene, Barakuda mtaunguza vitu kila baada ya dakika chache mna kata na kuleta
 
Kuna hitilafu imetokea tunaifanyia kazi hudima itarejea mapema
 
Ahsante kwa taarifa tafadhali onyesha namba ya simu kwa hatua zaidi
Nimewatajia location wakuu,namba ya simu ya nini tena? Hebu muwasiliane na wakuu wa idara yenu hapa njombe wawatume mafundi waje warekebishe maana tupo Giza siku ya tatu hili eneo hapo nilipo watajia wakuu!
 
Unapotoa taarifa kwetu ni wajibu kutoa taarifa kamili hata inbox kwa huduma bora
 
Hivi TANESCO mkoa wa Songwe mnashida gani maana kila weekend lazima mkate umeme na mnajinasibu siku hizi hakuna mgao wa umeme,hivi ninavyoandika hakuna umeme na jana mmekata siku nzima.
 
Eneo gani haswa

Namba ya simu tafadhali
 
Mliniomba no za simu na mahala ninapo kaa pamoja na matatizo yangu lakini naona kimya hata kunijibu tu text zangu mmeshindwa ,au mnafurahiya ninayo teseka?ngoja nijipange nihamie kwenye umeme jua tu maana sio kwa kupoteza pesa hivi tena kwaajili ya mtendaji kazi wenu asiye mwaminifu.
 
Tafadhali tutumie tena

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Namba ya taarifa

Hata inbox
 
Back
Top Bottom