TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Temeke Emergency
Mobile 022 213 8352
Home 0758 880 155

Tafadhalo onyesha namba yako ya simu na tatizo kwa hatua zaidi
Je kuna utaratibu gani kwa nyumba ya wapangaji,mpangaji ukitaka kuweka mita yako?
 
Je kuna utaratibu gani kwa nyumba ya wapangaji,mpangaji ukitaka kuweka mita yako?
Unapaswa kupata ridhaa ya mwenye nyumba na unatambue kuwa ukihama utaiacha hapo hapo kwa kuwa utakuwa haujalipia gharama ya mita bali umelipia gharama ya kufungiwa umeme.Aidha lazima tukague na kujiridhisha kuwa upo uhitaji wa kufanya hivyo.Tunakushauri ufike ofisi za eneo lako kwa hatua zaidi
 
Na gharama ni kiasi gani? Au ndio hiyo ya kawaida? 27,000/
 
Tanesco ofisi ya Rafia sijui ilokuwa ofisi ya tank bovu ikahamia Rafia mnachokitafuta mtakipata muda si mrefu.

Inaonekana ni masugu au siyo?!

Kwanini mnawakatia wananchi umeme kila siku ?

Kwani mna matatizo gani? [emoji2369][emoji2369]
 
Rais amesema muondoe kero za wananchi kabla wananchi hawajafikisha kero zao kwa viongozi wa juu.

Mmemsikia leo?

Sasa nyie endeleeni kufanya myafanyayo mtavuna myapandayo!

[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Isyesye mbeya tangu jana hakuna umeme mpaka Leo usiku umeme haujaridi ni kwanini?
 
TANESCO Kimara mwisho maeneo ya dawasco,matangini,TRA,Mavurunza ...hatuna umeme asubuhi hii na ni kawaida kukiwa hata na vinyunyu tu umeme unakatwa.
Ni tatizo sugu kwa line hii yaani mvua zikianza umeme unakatwa.
Hebu tanesco chungulia hapo nje uone hivyo vinyunyu lakini huku umeme ushakatika.
Line nyingine umeme hausumbui hata kuwe na mvua lakini yetu hii ni miaka mingi sana mvua zikianza tu mateso.Inaonekana mna mtambo wenu mbovu line hii kama sio transformer basi ni mtambo wa huko Ubungo unaolisha maeneo haya unasumbua hamtaki kusema ukweli maana umeme unakatwa huko huko Ubungo line yote.
Hebu tutendeeni haki wananchi wa maeneo haya tumeshalalamika vya kutosha.
Tufungieni mtambo mpya au tuhamisheni line zenye uhakika.
Mmetusumbua sana kwa muda mrefu.
 
Niwapongeze TANESCO kwa kazi nzuri mnazozifanya. Tunaziona juhudi zenu za kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma hii

Pamoja na hayo, naomba mnifahamishe vizuri juu ya kinachohitajika zaidi pale mteja anapoomba kubadilishiwa kiwango cha matumizi ya umeme, yaani kutoka matumizi makubwa kwenda matumizi madogo. Niliomba huduma hii, nikajaza fomu. Nimekaa muda mrefu, nikakuta hakuna mabadiliko. Nilipowauliza TANESCO kulikoni, wakasema hawana gari la kutembelea kufika nyumbani ili kujiridhisha kwanza. Nilipowauliza ni lini wanatarajia kupata gari, wakasema hata wao hawajui ni lini. Nilipoomba niwatafutie usafiri wangu mimi mwenyewe, walikataa. Mpaka sasa sijui ni lini watashughulikia suala hili. Naomba tusaidiane.
Eneo ni TANESCO -Makambako.
 
Yaani kwa namna TANESCO mlivyo wasumbufu na majibu ya hovyo hovyo nawaandalia bango moja murua kabisa, ambalo mama akiliona tu anakula kichwa kuanzia waziri na vifutu wote wa hii Halmashauri na mkoa.

Nawasalimu Tanesco kwa Jina la JMT.

Kazi Iendelee
 
TANESCO KIGAMBONI..Tafadhalini sana tafuteni ofisi nyingine..ile iliyopo ni ndogo sana..unafika asubuhi unakaa foleni saa zima unasubiri kwenda kuomba fomu ya kuunganishiwa umeme..jitahidini ...naomba unisaidie majibu ya maswali yangu..
1: mkiwa mnakwenda kumuwekea mteja umeme, huwa mnaangalia na ramani ya eneo husika au mnapachika tu nguzo na kuvuta waya zenu? Kuna kiwanja changu mmepitisha umeme katikati ya kiwanja changu nimewaambia mje mtoe sioni mnawajibika, mnataka nitoe rushwa?
2: Nguzo za umeme mnauza bei gani? Zile za magogo na zile za zege bei ikoje?..kuna site yangu inahitaji nguzo tano..'according to surveyor'...aliekuja kufanya survey na nikiweka inakuwa mali ya umma..hii imekaaje?
 
Umeme wilaya ya Mpwapwa unakatika kila baada ya masaa machache. Kwa zaidi ya miaka miwili umeme haujawahi kufikisha saa 24 mfululizo. Tatizo ni nini?
 
Umeme wilaya ya Mpwapwa unakatika kila baada ya masaa machache. Kwa zaidi ya miaka miwili umeme haujawahi kufikisha saa 24 mfululizo. Tatizo ni nini?
Ndio maana hakuna watu wa kuja kuwekeza wala maendeleo 0 hapo Mpwapwa kwa sababu ya vitu vya kijinga kama hivi
 
Umeme wilaya ya Mpwapwa unakatika kila baada ya masaa machache. Kwa zaidi ya miaka miwili umeme haujawahi kufikisha saa 24 mfululizo. Tatizo ni nini?
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

Jina: MKAZI WA WILAYA YA MPWAPWA.

Eneo: WILAYA YOTE YA MPWAPWA.

Wilaya: MPWAPWA.

Namba ya simu: Ya DC au?

Tatizo: KUKATIKA KWA UMEME MARA KWA MARA. UMEME HAUJAWAHI KUKAA SAA 24 MFULULIZO.

Toka lini: 2019 hadi sasa.

Tafadhali tambua kuwa Wilaya ya Mpwapwa umeme haukatika Wilaya nzima kama unavyodai, Tutumie taarifa kamili tufatilie swala lako kikamilifu.Tuma hata inbox lengo letu ni kukuhudima maana tunaamini nia yako ya kutoa lalamikowetu ni sisi kulifanyia kazi na wewe kupata mrejesho pamoja na kuona mabadiliko

Huduma Kwa Wateja

TANESCO Makao Makuu
 
Jina: MKAZI WA WILAYA YA MPWAPWA.

Eneo: WILAYA YOTE YA MPWAPWA.

Wilaya: MPWAPWA.

Namba ya simu: Ya DC au?

Tatizo: KUKATIKA KWA UMEME MARA KWA MARA. UMEME HAUJAWAHI KUKAA SAA 24 MFULULIZO.

Toka lini: 2019 hadi sasa.

Ahsante sana

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
View attachment 498143

Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.

Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;

1. ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2. NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3. KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4. JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5. MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6. KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7. KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;
 
Shida:Mtaa hauna nguzo wa umeme na umezungukwa na umeme
Eneo:Iseni Bondeni B kisesa
Mtaa:Iseni bondeni B Kisesa
Wilaya:Magu
Mkoa: Mwanza
Ili ufike: kutoka stand kisesa unaenda na barabara ya moja kwa moja mkono wa kabla hujafika stand ya iseni ,ukivuka kidogo stand ya bodaboda wanapopaki mtaa wote hauna nguzo
 
Naomba kufahamu, je rimoti ya kuwekea luku inapochakaa au kuharibika, mteja anatakiwa kununua mpya?
Screenshot_20210411-172656.jpg
 
View attachment 498143

Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.

Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;

1. ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2. NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3. KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4. JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5. MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6. KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7. KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;
Jamani tunaomba huku bonde la Rukwa/bondeni Sumbawanga kuna katizo la umeme wa REA ambalo nahisi halijawa hitokea katika inchi hii,mpaka inakera yaani.

Tukiuliza tunaambiwa matatizo ya kiufundi sasa matatizo gani hayaishi jamani.

LAELA ambao ndo makao yetu makuu wapo kimya tu .
 
Back
Top Bottom