TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tanesco mfanye kazi kwa kuzingatia miiko ya kazi zenu.Sio kwa hizi zima washa,zima washa Kama Kuna mtoto mdogo anachezea. Kabla atujaanza kuwachoma kwa wenye mamlaka. Mnatukera sana, hata taarifa hamtoi Kama hamjui kazi yenu, au mnataka serikali iwasaidie.Hakuna haja ya kuuliza ni wapi,kwa mkipita na hicho Kigali chenu cha emergence service hamuoni giza au Kama ni mchana hamuoni ukimwa, mpaka mpigiwe simu japo mnapita pale pale. Nendeni na wakati.
 
Kwa kweli mnakera jamani huku Kigamboni ndo kabisa haipiti siku hamjakata na taarifa hamtoi...
Na kila saa kukata hadi mnatuunguzia vitu
 
Asante, ulianzishwa uzi kwa ajili hiyomkuu upo hapaJF
Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO
Kwakweli Zamani Tanesco na mashirika mangine ya serekali huduma zilikua mbovu Sana, mteja ukifika kusikilizwa ni shida, Kila mtu yupo busy na Mambo yake, ila kwa Sasa kweli Mambo yamebadilika. Hasa nitoe pongezi kubwa kwa Tanesco, juzi need likua na shida nikalazimika kufika Tanesco Handeni, Yani kuanzia getini unapata good welcome, ndani Kila mtumishi anakusikiliza kwa wakati , mnyonge mnyongeni lakini hakiyake mpeni. Tanesco sasahivi wako vizuri Sana, na hasa Handeni ni powa Sana, congole kwenu kwakweli.
 
mimi nilitoa lalamiko langu lenye kumbu kumbu TB_3609 ya tarehe 25/01/2025....kwenye tawi la Tanesco Tabata....tatizo lilikuwa mita kuwa chakavu vibonyezeo vimeharibika vinafanya kazi kwa shida sana....umeme ukiisha inakuwa ngumu kuingiza umeme...tatizo hilo nililiripoti tokea tarehe 25/1/2021 yani hadi leo hakuna fundi alie kuja kuangalia tatizo...hapa najipaga kulipeleka tatizo langu kwa katibu mkuu ambae i rafiki yangu mkubwa...nita hakikisha nawafundisha adabu kuanzia kitengo cha huduma kwa wateja hadi maofisa wengineo...aiwezekani tulipie huduma harafu watumishi mshindwe kuja kutupa huduma stahiki kwa muda stahiki....
 
Tumepokea taarifa kwa ufatiliaji na hatua zaidi tafadhali
 
Tanesco, naomba niwafikishie malalamiko kuhusu mkuu wa kitengo cha manunuzi kanda ya MAGHARIBI (WEST ZONE).

Huyu jamaa anaitwa KABENDELA na ofisi yake ipo TABORA akisimamia manunuzi mikoa ya KIGOMA,TABORA,KATAVI na SHINYANGA.

Huyu jamaa ni mtu anayerudisha nyuma shirika la umeme Tanesco katika eneo hili kupitia idara ya MANUNUZI.

Huyu mzee Kabendela ni mla Rushwa. Kiufupi hafuati taratibu za manunuzi wala taratibu zilizowekwa na mifumo ya MANUNUZI kwa maana ya TANEPs.

Kwa mfano anaweza kutoa letter of intention to award kwa mzabuni X alafu baada ya siku chache akatoa barua nyingine kwa mzabuni P baada ya kuhaidiana 10%.

Taarifa za malalamiko zimeshamfikia Meneja wa Kanda, na baadhi ya vyombo husika.

Hakuna mfanyakazi hata mmoja wa Tanesco ndani ya Kanda asiyejua tabia mbaya na ulafi wa mzee Kabendela.

Hivyo basi kwa kuwapa taarifa hizi naomba mfuatilie malalamiko haya na mfanye uchunguzi wa suala hili ili mchukue hatua mnazoona zitafaa kisafisha shirika lenu la TANESCO hasa idara ya Manunuzi kanda ya Magharibi.
 
Tanesco, Eneo la Isyesye baadhi ya maeneo na Sae karibia na Mitambo yenu Kuna Changamoto na Umeme kila kwa Siku Unazima Zaidi ya Saa 12 na Kibaya Zaidi hatuna Taarifa yeyote.
Mbaya Zaidi tatizo ni la Muda mrefu lipo Constant haiwezi pita siku Mbili bila tatizo hili.
Tunaomba Mlitatue.
 
Sasahivi Tanesco wanajitahidi , wanafanya kazi na kero wanazifanyia kazi kwa haraka, mengine ni changamoto za kiutendaji tu, tuwaahukuru kwa kazi nzuri kwa sasa.
 
Habari TANESCO
Hii post nimeirudia kwa msititizo kwani niilipost tena nafikiri mwaka jana
Niliwashauri mnunue technologia ya kuwezesha mteja akinunua token iende moja kwa moja kwenye mita yake...Naamini hii ni technologia niya kawaida ambayo hata hapa nyumbani ( TZ) wanaweza kutengeneza;
1. Imagine umeacha watoto nyumbani umeme uishe
2. Imagine umeme umeisha usiku wa manane na mita ipo nje
3. Imagine umeme umesha usiku wa manane na huna battery za kuweka kwenye kile kimita cha vocher
4. Imagine unataka kukwawekea wazee umeme kijijini ( wazee wa miaka 70+ wataweza kuona tarakimu 20 kwa simu ya tochi?

Mambo ni mengi sana yaani ukifikiria vizuri utaona kuna kitu hakipo sawa kwenye technologia
Nafikiri lengo lisiwe kufikia watu wengi pekee...liwe ni pamoja na maboresh ya huduma
 
Tumepokea ushauri wako tafadhali
 
Tumepokea taarifa kwa ufatiliaji na hatua zaidi tafadhali
1617455386275.png

asante kwa msaada kesi yangu ya tarehe 25/january/2021 umenisaidia leo mafundi wameenda...ubarikiwe sana japo bado nina hasira nao ila nitawafanyia uchunguzi mwingine ambao utashusha ama kuongeza hasira yangu...ila kwa kesi namba TB_3609 umewasaidia...hukumu nimelegeza...

wajichunguze wenyewe na wabadilike....kuna watanzania mamilioni awana kazi...hivyo kuwaondoa hao wachache hakupunguzi kitu.....

be blessed...
 
View attachment 1742224

Tunashukuru sana kwa taarifa mpendwa mteja wetu
 
Kiukweli ili mji ukue kwa haraka lazima huduma za kijamii ziwe zinapatikana kwa ukaribu.hili la tanesco kusambaza nguzo viwanja vyote vilivyopimwa hata kama hakuna nyumba ni la kupongezwa
 
Kuunganishiwa umeme baada ya kulipia inachukua muda gani? TANESCO
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Hivi naomba kujua TANESCO umeme wa rea nguzo moja mnauzaje maana mamaangu kaambiwa nguzo moja laki nne kuvuta hadi nyumbn kwake, ni huku huku buhigwe.
 
Hivi naomba kujua @TANESCOumeme wa rea nguzo moja mnauzaje maana mamaangu kaambiwa nguzo moja laki nne kuvuta hadi nyumbn kwake, ni huku huku buhigwe.
Mteja halipii nguzo bali alipia gharama halisi ya kuunganishiwa umeme na kama eneo lako linahitahi nguzo unapaswa kusubiri miundombinu ikufikie
 
Back
Top Bottom