TANESCO NA MIRADI YA REA.
Nimeshawahi lalamika hapa ni kwa jinsi gani namna nilivyocheleweshewa kuungwa huduma ya umeme hasa kwenye maeneo ya vijijini.
Nipo wilaya ya Mufindi kijiji Cha Mkalala, nahudumiwa na ofisi ya TANESCO Mafinga.
Katika kijiji chetu tulipata umeme wa REA 2019.
Mkandarasi anayefahamika kwa jina la Sengerema ndiye aliyepewa tender ya kusambaza umeme ndani ya kata yetu ya Mninga na kata kadhaa ndani ya mkoa wa Iringa.
Mkandarasi alifanikiwa kuwasha umeme mnamo mwezi wa September 2019.
Baada ya kuwasha nyumba kadhaa hakuwahi kurudi tena katika kijiji hicho kuunga umeme katika kijiji na kata yetu ila tu ukifanya juhudi binafsi mkandarasi anakuja kufunga Mita mara moja na kuondoka. Juhudi binafsi ni zipi? Yaani kwa sasa wako vijiji vingine ndani ya Iringa, so ukihitaji Mita inakulazimu umtafte mkandarasi na umlipe pesa binafsi kama nauli (hongo) ya kiasi Cha 100,000 ndipo Fundi anakuja kufunga mita y'ako tuu na kuondoka.
Hivi sasa kuna wateja wengi Sana ndani ya kata ya mninga yenye vijiji 5 (Ikwega, Mninga, Mkalala, Kihanga na Itulituli) ambao tulishalipia huduma ya kuungwa umeme toka 2019 lakini hatujapata huduma, tatizo letu tumemfikishia Meneja TANESCO wilaya lakini hakuna kilichofanyika zaidi ya kuambiwa mkandarasi ana upungufu wa vifaa yaani Mita lakini huyo huyo mkandarasi ukitoa pesa basi Mita unafungiwa mara moja.
Kucheleweahewa kufungiwa Mita zaidi ya mwaka mmoja na nusu hakujatukosesha huduma ya umeme tu, bali kumeikosesha serikali mapato ambayo yangetokana na ununuzi wa umeme.
Kafariki Magufuli hivi hili tutamlilia nani Ili umeme tuupaate bila ubabaishwaji?