TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kwa hiyo ina maana ni nchi nzima umeme haununuliki waziri mwenye dhamana na shirika amelala usingizi mpaka rais tumekwisha.
nashangaa tanesco wameshindwa kuwa na backup jamani kwamba system hii ikifeli tunawasha hii yani tuko kwenye ujima kama miaka ya 1960s huko
 
Nyie Tanesco ni wapuuzi sana sijawahi kuona shirika ambalo baada ya kujiendeleza ndio tunarudi nyuma. Siku ya tatu karibu nchi nzima inalia juu ya kukosekana kwa umeme kupitia njia ya mitandao.
na mapesa yote wanashindwa kuwa na backup na watu wa usalama wanaacha tu nchi inahujumiwa tanesco hawaangalii wamepoteza billions ngapi kwa siku tatu hizi
 
Hatari na inasikitisha sana sidhani kama ingekuwa kampuni ya mtu binafsi asingekubali kupoteza pesa kwa siku hizi zote.
Ni nchi nzima mkuu, kama una akiba ya unit kwenye meter yako jitahidi uzime vifaa na taa za ziada maana hakuna anayejua hili tatizo litatatuliwa lini, labda wadukuzi waliodukua bomba la mafuta la huko USA wameelekeza mashambulizi yao Tanzania!
 
Wenye kelele za sukuma gang mara wajane mko wapi msaidie tanesco kurudisha Luku ama kweli mwamba kaondoka na mambo yake mazuri. TUTAMKUMBUKA

Poleni mliopata hasara kwa ukosefu wa Luku
 
Mifumo,mifumo,
Kama uhai wa binadamu,
Kuna wakati ina changamoto....
Juzi USA wamepigwa kwenye mabomba ya mafuta na wakasumbuka balaaa,
Na wao ndio Wana kila kitu, Sembuse sisi wa dunia ya tatu?

Sent from my V2027 using JamiiForums mobile app
kwanini kusiwe na backup kuwa mfumo huu ukijamba tunawasha huu hii kitu ni uzembe wa hovyo kabisa
 
kwanini kusiwe na backup kuwa mfumo huu ukijamba tunawasha huu hii kitu ni uzembe wa hovyo kabisa
imagine kaka shirika linahudumia watanzania millioni 60 linatengemea mfumo mmoj tu alaf sawa mnao mmoja jiandaen na changamot bas pia hamn mpak waziri aseme fanyeni hivi...dah...
 
Tuwape muda Tanesco....

Sent from my V2027 using JamiiForums mobile app

Hii hali ndo inatugawa sana.
Wengi wanalia wachache wenye nacho wanafurahia.

Unawapaje muda Tanesco kwenye suala kama hili. Kama ni kudukuliwa kwanini wasiseme mapema.

Acheni usenge wazee watu tunategemea hii nishati kujiingizia kipato kumamake.

TANESCO acheni usenge kumamake😈😈😈😈😈😈😈
 
Haileti mantiki Tanesco hawana backup server system. Ikitokea ofisi ya server imeungua au mafuriko.

Tuna tatizo la mfumo wa elimu hapa naona kwa wahusika hao IT manager and Priciple IT systems officers. Waziri anafika anawauliza mbele ya kamera hamna backup system. Waende wakajifunze System management kutoka Vodacom. Na Tanesco hawajawahi kutangaza hizi nafasi njee wanagroom vijana wao wa ndani humohumo hii pia ni shida sana.

Bord inabidi ijiuzulu kwa hili maana ni zaidi ya dhahama. Bodi inatakiwa iwe.mbele zaidi kuhusu system recovery plan.
 
Mfumo mfumo mfumo......


Namba ya Muamala: 08745298 TSH 500 haukufanikiwa kutumwa kwenda kwa LUKU. Sababu System could not process transfer. Salio lako Jipya ni TSH 23,889. Asante!
 
Mpango wa kuuza magenerator naona unafanikiwa kwa kasi
Hizi mambo tulikuwa tunasahau asee, but zinaanza kuibuka upya tena kwa ustadi wa kipekee, na unaona bimkubwa ametulia au hajui kinachoendelea..!.

But angekuwepo jamaa now tungesikia mengine 😬!, Afrika pasipo kushurutishwa tena kwa mijeledi mambo hayaendi.
 
Namba ya Muamala: 648171097. Umenunua LUKU Tsh 6,500 Kwenye Namba ya Mita: 43002261956 wakati 2021/03/21 21:52:50, Gharama TSH 100: TOKENI:50377900650532133840. Salio lako jipya ni TSH 44,739.

Asante!....naombeni Tanesco muweze kunirudisha hela yangu kwenye account yangu ya halopesa maana hio meter imebadilishwa wameweka mpya.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Namba ya Muamala: 648171097. Umenunua LUKU Tsh 6,500 Kwenye Namba ya Mita: 43002261956 wakati 2021/03/21 21:52:50, Gharama TSH 100: TOKENI:50377900650532133840. Salio lako jipya ni TSH 44,739. Asante!....naombeni Tanesco muweze kunirudisha
hela yangu kwenye account yangu ya halopesa maana hio meter imebadilishwa wameweka mpya.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Nimestuka sana
 
Back
Top Bottom