SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
Septemba 28, 2021
TAARIFA YA MABORESHO KITUO CHA KUPOKEA NA KUPOZA UMEME CHA SINGIDA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake kuwa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Singida 220/33kV kitazimwa, ili kumruhusu Mkandarasi anayejenga njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 400 kufanya kazi katika kituo hicho na kuwezesha kuwasha vituo vya Singida na Dodoma katika msongo wa kilovolti 400 kama ifuatavyo:-
Jumamosi Oktoba 02, 2021 kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi 11:00 jioni.
Maeneo yatakayoathirika:
Mkoa wa Manyara na baadhi ya maeneo katika mikoa ya Singida, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.
Jumapili Oktoba 03, 2021 kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni.
Maeneo yatakayoathirika:
Mikoa ya Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Mara, Geita, Simiyu, Manyara na baadhi ya maeneo katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga.
TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliyokatika, toa taarifa Ofisi ya TANESCO iliyokaribu au Kituo cha Miito ya Simu Makao Makuu: +255 222 194 400 na +255 768 985 100.
Mitandao ya Kijamii:
Twitter,
www.twitter.com/tanescoyetu
Facebook
Kirjaudu sisään Facebookiin
Imetolewa na;
Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO MAKAO MAKUU.