TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Ndugu mteja,
Gharama ni shilingi 27,000 hivyo tunakushauri ufike ofisi ya TANESCO iliopo karibu na wewe na utapewa maelekezo zaidi
Mimi nataka mnipunguzie gharama ya umeme maana nikinunua umeme wa 10,000 napata unit 28 wakati sina matumizi makubwa ni matumizi ya kawaida, hebu nipe mwongozo kwanza
 
Mimi kwangu surveyor alikuja toka 28/04/2021 nipo ndani ya mita 45 panahitaji nguzo moja ila mpaka leo TANESCO hawataki kunipa control number, sasa sijui hizo siku 60 zinaanza kuhesabiwa kuanzia kwa surveyor au kuanzia siku uliyopewa control number. TANESCO naombeni majibu
Ndugu mteja,
Tusaidie taarifa zako sahihi ulizotumia kuomba umene kwa ajili ya ufuatiliaji. Pia tutashukuru kupata mawasiliano yako.
Asante
 
Ndugu mteja,
Tusaidie taarifa zako sahihi ulizotumia kuomba umene kwa ajili ya ufuatiliaji. Pia tutashukuru kupata mawasiliano yako.
Asante
Jina: Lwitiko Mwambene
Eneo: Chipaka
Wilaya: Momba
Mkoa: Songwe
0753154053
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

Septemba 28, 2021

TAARIFA YA MABORESHO KITUO CHA KUPOKEA NA KUPOZA UMEME CHA SINGIDA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake kuwa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Singida 220/33kV kitazimwa, ili kumruhusu Mkandarasi anayejenga njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 400 kufanya kazi katika kituo hicho na kuwezesha kuwasha vituo vya Singida na Dodoma katika msongo wa kilovolti 400 kama ifuatavyo:-

Jumamosi Oktoba 02, 2021 kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi 11:00 jioni.

Maeneo yatakayoathirika:

Mkoa wa Manyara na baadhi ya maeneo katika mikoa ya Singida, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Jumapili Oktoba 03, 2021 kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni.

Maeneo yatakayoathirika:
Mikoa ya Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Mara, Geita, Simiyu, Manyara na baadhi ya maeneo katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliyokatika, toa taarifa Ofisi ya TANESCO iliyokaribu au Kituo cha Miito ya Simu Makao Makuu: +255 222 194 400 na +255 768 985 100.

Mitandao ya Kijamii:

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook Kirjaudu sisään Facebookiin

Imetolewa na;
Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO MAKAO MAKUU.
IMG_20210928_204903.jpg
 
Wadau inasikitisha sana kwa TANESCO KIGAMBONI wapo KIMYA Umeme Umekatika toka Jana Saa 2 Usiku Mpaka Sasa Haujarudi na Hakuna TAARIFA yoyote iliyotolewa na UONGOZI WA TANESCO KIGAMBONI
Ni Vema kama kuna TATIZO wateja wakajulishwa Kukaa KIMYA kwa UONGOZI ni DHARAU kwa WATEJA WENU.
 
Umeme UMEKATIKA Kisiwani Kigamboni toka Jana saa 2 Usiku mpaka Muda huu HAUJARUDI hata Taarifa ya Uongozi hakuna
 
Wadau inasikitisha sana kwa TANESCO KIGAMBONI wapo KIMYA Umeme Umekatika toka Jana Saa 2 Usiku Mpaka Sasa Haujarudi na Hakuna TAARIFA yoyote iliyotolewa na UONGOZI WA TANESCO KIGAMBONI
Ni Vema kama kuna TATIZO wateja wakajulishwa Kukaa KIMYA kwa UONGOZI ni DHARAU kwa WATEJA WENU.
Rais wa Kenya kaagiza umeme ushushwe bei kwa 33% sie tuna lalama umeme umekatika. Halafu uko juu mara mbili ya Kenya. Nchi ya laana.. Tunachojua ni kuteka watu na kesi za kubumba tuu.
 
Tunaenda kuharibu mitambo Mtera very soon. Umeme utarejea ktk hali yake ya kawaida pale tu zile tenda zetu za kuagiza mafuta mazito ya kuzalishia umeme kwa mitambo ya Aggreco itakapofufuliwa.

Vinginevyo endeleeni kulalama. Tuko serious tunataka kula
 
Wadau inasikitisha sana kwa TANESCO KIGAMBONI wapo KIMYA Umeme Umekatika toka Jana Saa 2 Usiku Mpaka Sasa Haujarudi na Hakuna TAARIFA yoyote iliyotolewa na UONGOZI WA TANESCO KIGAMBONI
Ni Vema kama kuna TATIZO wateja wakajulishwa Kukaa KIMYA kwa UONGOZI ni DHARAU kwa WATEJA WENU.
Wiki nzima hii Kigamboni umeme ni kama discolight ...haya ni maandalizi ya justification ya kubinafsisha shirika
 
Naomba namba yenu nipige niwape maelezo hiyo sehemu
Mafundi wetu wa idara ya matengenezo wapo eneo hilo wanaendelea na jitihada za utatuzi ili kurejesha huduma ya umeme.Tunawaomba uvumilivu wenu
 
Kisiwan ipi hiyo?Umetazama luku yako?
Mi nipo hapa Asimwe nakula umeme upo kisiwan yote
 
Msaada, surveyor alipokuja mara ya kwanza jirani yangu aligoma umeme usipite kwake hivyo ikanilazimu kuzunguka pakahitajika nguzo mbili.
Jana nimeongea nae kakubali nipitishe kwake hivyo nitahitaji nguzo moja tu.

Je siku watakayokuja kuniwekea si tunaweza fanya hayo mabadiliko au watafuata alichoandika surveyor watumie nguzo mbili wakati sehemu ya kutumia nguzo moja ipo ili hiyo moja wakampe mteja mwingine
 
Tanesco wilaya muleba mkoa kagera Kuna tatizo gani mbona umeme tangu Jana asubuhi mmekata na taarifa hakuna mnatukwamisha wengine kula kwetu mpaka umeme uwepo bila hvyo ni njaa tu tusaidieni tafadhali
 
mkuu naomba kujua kama umeshajaza fomu ya maombi ya kuunganishiwa umeme inachukua mda gani surveyor kufika site?

Nimejaza fomu ya kuunganishiwa umeme toka mwezi wa 6 mpaka mwezi huu sijatembelewa na surveyor kila nikienda Tanesco naambiwa surveyor atakuja.
 
Back
Top Bottom