TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Hii sekta imekuja kuwa ya kiree sana asee, ndo kusema kwamba hamjui umuhimu wa nishati ya umeme wa wananchi au? Sikuhizi mkijiskia kukata mnakata tu iwe usiku wa manane iwe Mchana iwe ahsubuhi, Sawa kutwa nzima tunaweza kusema mnafanya ukarabati haya na usiku huu saa 5 mnakata umeme kwanini?

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
 
Sasa hivi hapa kinondoni naona umeme hauna nguvu za kiume unawaka kwa kubring bring kama indicator ya ndege. Inawezekana mmeajiri mtu anafanya mazoezi ya kuwasha na kukata kwa dharura.
 
Huku majohe viwege vipi jamanii .. umeme tangu jana saa tano usiku umekatika mpaka leo haujarudi.. shida ni nini?
 
Tanesco bajeti ya hii miradi yenu kisarawe II kigamboni bado tu? Hizi nguzo mmeweka bila waya inakuaje sasa
 
Bora magufuli afufuke afute hiyo tanesco yenu, yaan saiz umeme kukatika imekuwa kawaida na usipo katika tunashangaa... yaan Hah! Hv leo hawajakata umeme...

Na mpaka saiz naandika hapa umeme umekatika ... Nyaaambaf kazi kulipana mishahara mikubwa tu na wakat umuhim wenu hatuuoni.
 
Mm naomba kuuliza nimesikia Tanesco mnauza meter ambazo mtu anaweza kuifunga chumbn kwake kwa 340000 naomben ufafanuzi
 
Mm naomba kuuliza nimesikia Tanesco mnauza meter ambazo mtu anaweza kuifunga chumbn kwake kwa 340000 naomben ufafanuzi
Hapana TANESCO haina huduma ya kuuza mita wala kifaa chochote cha umeme bali inahusika na kuunganishia wateja umeme wale waliomba, kupimiwa na kulipia
 
Hapana TANESCO haina huduma ya kuuza mita wala kifaa chochote cha umeme bali inahusika na kuunganishia wateja umeme wale waliomba, kupimiwa na kulipia
Asante sana!! Kuna hii changamoto ya umeme ktk nyumba za kupanga, unakuta wapangaji mnategeana kununua umeme mwisho wa siku mnalala giza au mmoja ndio anaumia Zaidi kwa kununua umeme kila mara unaoousha, je Kuna njia mbadala Kupunguza makali ya Hilo tatizo ?
 
Hapana TANESCO haina huduma ya kuuza mita wala kifaa chochote cha umeme bali inahusika na kuunganishia wateja umeme wale waliomba, kupimiwa na kulipia
Sema ndg zangu Tanesco kuna jambo nashindwa kuwaelewa mlikuja kubadilisha mita ya zamani mtaa Lindi/congo nyumba namba 69"kariakoo.

Ile mita ya zamani ilikuwa na unit 41 hamkuzirudisha/kuhamishia kwenye mita yenu mpya mliyoweka.

Lakini cha kishanganza mita mliyoikuta ni ya makazi ila nashangaa feni fridge na taa kwa siku natumia unit 6.1 je hii ni haki.

Au tuna kiwanda bubu chumbani?
Naomba majibu tafadhali
 
Sema ndg zangu Tanesco kuna jambo nashindwa kuwaelewa mlikuja kubadilisha mita ya zamani mtaa Lindi/congo nyumba namba 69"kariakoo.
Ile mita ya zamani ilikuwa na unit 41 hamkuzirudisha/kuhamishia kwenye mita yenu mpya mliyoweka
Lakini cha kishanganza mita mliyoikuta ni ya makazi ila nashangaa feni fridge na taa kwa siku natumia unit 6.1 je hii ni haki
Au tuna kiwanda bubu chumbani?
Naomba majibu tafadhali
Tafadhali onesha

Wilaya

Namba ya simu

Namba ya mita

Imebadilishwa lini

Kwa hatua zaidi
 
Back
Top Bottom