Ndugu Mteja
Tunashukuru kwa taarifa, Tumezipokea kwa ufatiliaji na hatua zaidi.
TANESCO Huduma kwa Wateja
Makao Makuu
0748550000
-Kwa niaba ya wakazi wa Mwanalugali (kiwanja cha hisia Kali), tunashukuru Menejiment ya TANESCO Makao Makuu na TANESCO Mkoa wa Pwani,hususani Meneja wa TANESCO Kibaha.
-Siku moja baada ya idara ya huduma kwa wateja Makao Makuu kupokea taarifa yetu na kuahidi kuifanyia kazi , utekelezaji wake tumeuona.
-Tunatoa shukrani kwa Management ya TANESCO Kibaha kwa kutuma mafundi kuja kutandaza nyaya kwenye nguzo tisa ambazo,zilisimikwa tarehe 13July2022.
-Wananchi wa Mwanalugali (kiwanja cha hisia Kali) tunashukuru kwa kusikia kilio chetu cha muda mrefu.
Lakini, Mradi wa Mwanalugali (kiwanja cha hisia Kali) ,ulikuwa unahitaji nguzo 15
- lakini kwa kuwa tarehe 30.06.2022 wakati wa kufunga mwaka Shirika lilikuwa na nguzo chache site, Mradi huu ulipatiwa nguzo 9 kwa kuanzia.
-Wakazi wa Mwanalugali (kiwanja cha hisia Kali) tunaomba Management ya TANESCO kumalizia nguzo 6 zilizosalia.
-Vifaa vingine vilibaki,labda kama vilihamishwa kupelekwa site nyingine.
-itapendeza kama nguzo zilizosalia zitaletwa na kujengwa,
- Mwezi September 2022 wakazi wa Mwanalugali tuje kulipia service line ya shs320,960.
-Kwa mara nyingine tena, wakazi wa Mwanalugali tunashukuru Management ya TANESCO kwa huduma nzuri. Mwenyezi Mungu awabariki.
Ombi
1). Tunaomba Manejiment ya TANESCO Makao Makuu, Mkoa wa Pwani na Kibaha kuleta nguzo zilizosalia tunaamini,hili lipo chini ya uwezo Regional Manager Kibaha
2). Menejiment ya TANESCO Kibaha,wapitie michoro ya mradi huu wa Mwanalugali (kiwanja cha hisia Kali).
3). Regional Manager Pwani, kama suala letu, lipo nje ya uwezo wako,tufikishie kwenye Mamlaka husika,
NB: Projects has always the time frame to finish.it is high time this project is brought to an end.