TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Wakuu nahitaji kuweka umeme wa 3 phase kwenye jengo lakini mimi ni mpangaji, mnaweza kunipa muongozo nijaze vipi maombi kwenye app ya nikonekti?
 
Wakuu nahitaji kuweka umeme wa 3 phase kwenye jengo lakini mimi ni mpangaji, mnaweza kunipa muongozo nijaze vipi maombi kwenye app ya nikonekti?
Ndugu mteja kwenye app yetu ya nikonekt haina sehemu ya kuomba single au three phase, bali mteja wetu anaomba umeme kama kawaida. mteja atafungiwa single au three phase kutokana na mchoro wa mkandarasi wake na majibu baada ya vipimo vya survey. Hivyo kama unahitaji meter ya 3 phase na hapo ulipo panga kuna umeme tayari fika ofisi za tanesco na barua ya mwenye nyumba wako kukuruhusu mpangaji wake kuweka meter yako kwenye jengo lake kisha utajaza fomu maalamu (meter separation) kisha utafanyiwa vipimo na kulipia ^EB
 
Jana Usiku Majira ya saa 7 walikata na kurudisha asubuhi leo tarehe 24.01.2023. Na jioni hii wamekata tena. Tatizo ni nini. Eneo ni Toangoma - Kongowe DSM
 
Kumekuwepo na mazingira tosha kabisa ya RUSHWA kwa wafanyakazi wa TANESCO na MIRADI INAYOSHIRIKISHA shirika hii nayo mnataka tuwapeleke TAKUKURU ,?
 
Jana Usiku Majira ya saa 7 walikata na kurudisha asubuhi leo tarehe 24.01.2023. Na jioni hii wamekata tena. Tatizo ni nini. Eneo ni Toangoma - Kongowe DSM
Ndugu Mteja.
Tumepokea taarifa za changamoto ya umeme maeneo hayo iliosababishwa na kuanguka kwa baadhi ya nguzo, hivyo imelazimika kuzima line za umeme kwa ajili ya matengenezo. Tunawaomba radhi kwa adha yeyote mliyopitia wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kutatua tatizo
TANESCO Huduma kwa Wateja
0748550000 ^EB
 
Huu uzi ulitakiwa ufutwe kabisa maana hauna suluhu yoyote ya maana kwa mwananchi tangu umeanzishwa zaidi ya majibu ya kisiasa tu. Kila siku maswali tofauti kuhusu ukosefu wa umeme maeneo mbali mbali nchini,lakini jibu limekuwa halibadiliki. Kama mmeshindwa kuendesha shirika kwa ufanisi,kuweni wawazi ijulikane nani anawakwamisha ili lawama zielekezwe kwake.

Kilio cha umeme nchi hii ni kikubwa lakini miaka yote watendaji wake hamuwajibiki kwa namna yoyote. Mishahara mnajilipa mikubwa kwa kazi isiyoonekana.
 
Niliomba kuunganishiwa umeme via Nikonect app.
Contractor akajaza, surveyor akaja. System ikasema awaiting quotation and CN.
Jana nimeangalia status inasema: await re-surveyed. Leo inasema Surveyed. Control number haitoki, mwishowe nitatumia hii pesa.

Nipo Geita mjini.
Ndugu Mteja!

Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali tunaomba namba yako ya ombi la kuunganishiwa umeme ( Application number) kwa ufatiliaji na hatua zaidi.

TANESCO Huduma kwa Wateja

Simu 0748550000^EB
 
Kumekuwepo na mazingira tosha kabisa ya RUSHWA kwa wafanyakazi wa TANESCO na MIRADI INAYOSHIRIKISHA shirika hii nayo mnataka tuwapeleke TAKUKURU ,?
Takukuru hii hii au kuna ingine?😀😀😀😀
 
TANESCO MIMI NI.MKAZI WA KILOMBERO-SIKU ZA NYUMA TANESCO WALIPITISHA WAYA WA UMEME KATIKATI YA UWANJA WANGU LEO NIMEJENGA BOMA NIMEMALIZA NAWAAMBIA WAONDOE WAYA WA UMEME WA UPITISHE KWA PEMBENI ILI NIWEZE EZEEKA MWAKA WATATU SASA NAOMBA MNISIDIE HUKU TUNATESEKA SANAA.
 
Ndugu Mteja

Tafadhali onesha ni eneo gani? Wilaya na namba ya simu kwa hatua zaidi

TANESCO Huduma kwa Wateja

0748550000
Mwanza mjini Maeneo ya Pasiasi, Lumala, Msumbiji mpaka Kiseke kote umeme hakuna
 
Siku za mwanzo wa January Umeme ulikuwa stable kiasi Fulani. Time enjoy uninterrupted power supply. Sasa mmeanza taabu zenu. ON OFF, ON OFF, ON OFF. Offffffffffffffffffffffffffffff ndiyo kuanzia Jana imeshika Kasi.
Mpàka Sasa hakuna umeme toka saa 11:30 asubuhi.

KUNA NINI TANESCO MBONA MNAKERA?
 
Siyo huko tu Hata huku Mwanza kuna mgao toka Juzi mpaka leo hii, ratiba ni ile ile ya unakatwa asubui unarudi jioni, unakatwa jioni unarudi saa tano usiku
 
Duuu kumbe siyo Biharamulo tuu mpaka huko mmekalishwa kwenye kuti kavu
 
Hata huku[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Back
Top Bottom