TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Jamani TANESCO kuna shida gani huku Chamaazi kwa mapunda kila siku for almost a month mnakata umeme mama 6 Mara usiku hatuna umeme na hata Sasa naandika hapa hatuna umeme na hamsemi shida ni nn ...no notes mnakata Mara ghafla unarudi tena ...semeni shida ni nn na kwann ni hapa tu kwa mapunda
 
Mambo ya kipumbavu sana haya asee, Kukatia watu umeme bila taarifa na mnajua ni kitu cha muhimu ni ishara ya madharau na kuonesha ni namna gani mnatumudu au?
 
Mambo ya kipumbavu sana haya asee, Kukatia watu umeme bila taarifa na mnajua ni kitu cha muhimu ni ishara ya madharau na kuonesha ni namna gani mnatumudu au?
Toka saa 5asubuhi mpaka sasa hivi saa 4.40 usiku hakuna umeme, jamani mnatukosea sana wananchi
 
Tanesco Kuna Shida gani mbona nimenunua umeme toka juzi naweka lakini unagoma unaandika error Shida inaweza kuwa nini.

Nikajua labda nilikosea number za mita lakini naona zipo sawa tu Shida ni nini?@TANESCO
 
Tanesco Usa River.maeneo ya maji ya chai,Imbaseny; mmekuwa mnakata umeme alfajiri na kurudisha usiku saa 2 kila siku.Tafadhali hili tatizo mshughulikie au kama kuna magao mtuambie ili tujipange.
 
Ni kweli CHANGAMOTO zipo lakini naona hii imezidi kwani, kiangazi tuliambiwa sababu ni kupungua kwa vina vya maji kutokana na ukame na uchepushaji wa mito.

Sasa matatizo ya kukatika kwa umeme ni kiufundi au hujuma? Kweli tutakuja kuendelea kweli? Na waheshimiwa mnaona au mnaishi dunia ipi?
 
Back
Top Bottom