TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Maoni na ushauri shirika lingizwe ktk ushindani wa biashara kwa kuza umeme na kukusanya mapato yani kodi na private sector competition wakandalasi wasambaze umeme na matengenezo kunga wateja kwa Kasi zaidi na wafanyabishara wauze meter na kusajir kama line za sm kwa haraka Ili kuongeza ufanisi na tija zaidi kwa masilai ya taifa na watu wake. Ayo ndio maoni ya kizalendo kwa shirika la tanesco
 
Hawa tanesco hawajielewi, Iringa kila siku wanakata umeme saa 12 asubuh wanarudisha usiku, sijui usiku umeme utanisaidia nini kwenye biashara!
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto, tumepokea taarifa za hitilafu ya miundombinu maeneo hayo, tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, wataalamu wetu wanafanya jitihada katika zoezi hilo matengenezo yatakapokamilika huduma itarejea.^EB
TANESCO,

Je! Kuna kitu gani kinachoendelea kuhusu kukatika hovyo kwa umeme karibu kila kona hapa nchini?
Je! Ni mgao wa umeme umeanza rasmi ama kuna sababu nyingine zaidi ya hii?

Ni vyema muwe wawazi katika hili kuliko kutafuta sababu zisizojitosheleza. Malalamiko ni mengi mno, lakini sababu mnazo zitoa kwa. kusema kweli hazina mashiko kabisa.

Toeni ratiba kamili kila siku kuhusu mgao huu wa umeme ambao ni dhahiri kuwa upo, ili watu wajipange vyema kuendesha shughuli zao.
 
Hello TANESCO kuna tangazo nimeliona kwenye mitandao kwamba mita zinazoanzia namba 04, 05, 06, 07 na 013 zinatakiwa zibadilishwe kwani muda wa matumizi yake ni mwisho mwezi ujao......tangazo hili lina ukweli wowote?
 
TANESCO MKO WAPI KUNA LINKS ZA MATAPELI HUKU WHATSAPP (SPOOFING) . WAMETENGENEZA PAGE FAKE KAMA INAVYOONEKANA HAPO CHINI. WANAKUSANYA NAMBA ZA MITA ZA UMEME KUPITIA FAKE SITE. BILA SHAKA WANAWEZA KUWAFANYIA UTAPELI WATEJA WENU KWA KUTUMIA HIZO MITA NAMBA ZAO. TOENI TAHADHARI HARAKA ILI KUWANUSURU WAPENDA VYA BURE

1695282810526.png

matapeli Tanesco.JPG
 
Tanesco : Nitofautishieni kati ya:

1. Mgao.
2. Upungufu wa umeme.

Zingatieni: Sababu ya Mgao ni nini.

Asante sana

#tanzaniayenyenuru.
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto, tumepokea taarifa za hitilafu ya miundombinu maeneo hayo, tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, wataalamu wetu wanafanya jitihada katika zoezi hilo matengenezo yatakapokamilika huduma itarejea.^EB
Muogope Mungu,hitilafu kila siku ngaramtoni mnakata umeme
 
Zamani ipi???

Wenyewe wamekuja na mfumo mpya wa ndani ya siku 7 unaunganishiwa umeme. Sasa kwa wiki tatu ni halali watu kulalamika.
So they are better

Maana Wengine tulisubiri for six months

Siku hizi three weeks tunalia

Hongera Tanesco
 
Hello TANESCO kuna tangazo nimeliona kwenye mitandao kwamba mita zinazoanzia namba 04, 05, 06, 07 na 013 zinatakiwa zibadilishwe kwani muda wa matumizi yake ni mwisho mwezi ujao......tangazo hili lina ukweli wowote?
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto, tangazo hilo ni la kweli na kila Mkoa utafanya mabadiliko kwa utaratibu maalumu, hivyo kwenye Mkoa wako zoezi hili likifika utafahamishwa tafadhali.^OK
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom