TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
[emoji41]
1695396512161.jpg
 
Ushauri wangu
Kipindi cha kiangazi kitumike kusafisha mabwawa kwani kwa sasa mengi yamejaa matope hata mvua ikinyesha uwezo wa kuweka maji pengine ni robo ya uwezo wake na ndio sababu kiangazi cha mwezi mmoja tu maji yanaisha na kuanza mgao
Mkiyasafisha watu watakosa umeme kipindi kimoja na pengine kuupata kwa miaka 10 bila usumbufu tofauti na sasa ambapo Mvua ikinyesha sijui ndio mnaona tatizo limeisha kumbe ni sawa na kufunika moto kwa majivu....
 
Kati ya mawaziri nishati na wakurungezi wa tanesco shindig hata wajiga wanajua ni Makamba na Maharage wake.Tena wafie mbali sio kwa mateso haya mliosababisha kwa watanzania.
Mlikuja na hoja wakati JPM kulikuwa hakuna serives kumbe saga tu nyambafuuuuu.Kaongeze bei huko TTCl simu sio lazima hasa kwa kutumia ttcl,
 
Tanesco,nimenunua umeme iupitia nmb hamjanipa tokeni,huku tano yangu mmekula umeme hamjanipa Kwa kifupi mmeniibia Mimi mteja wenu.
 
Unaweza kucheka na kushangaa lakini TANESCO wanaogopa mwenge balaa. Mwenge ukipita sehemu yenu jua mtapata neema ya umeme kwa siku chache. Sikujua mwenge una nguvu hivi!
 
Ah ah Singida toka jumamosi hadi leo tuna maji ya kutosha na umeme ambao Tunaweza kuuzia inchi jirani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwenge wenyewe ni mwanga tosha, umeme wa TANESCO uzimike hiyo si itakuwa balaa? Kazi ya mwenge inajulikana, mojawapo ni kumulika wazembe, sasa ni mzembe gani atakubali mgao utokee uliko mwenge? Majibu yake atayapata huyo bosi wa umeme wa eneo hilo
 
Kinyerez leo siku ya nne umeme haujakata,mgao umeisha nn ama ndo tanesco wanatunywesha maji then tuvute pumz muda wa mapumziko kabla ya kurudi uwanjan
 
Mmesema mpo ktk ukarabati si ndio.. busara ni kumtangazia mwananch wa eneo husika mnakata na kurudisha muda gani.

mlinikaririsha huku bujingwa ilemela mnakata 12 alfajir unarud moja jioni.

shida leo mmekata 11 jioni hadi sasa saa4 usiku giza..! Yaan utaratibu wenu umekaa hovyo kama mvurugiko wa breed
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto, tangazo hilo ni la kweli na kila Mkoa utafanya mabadiliko kwa utaratibu maalumu, hivyo kwenye Mkoa wako zoezi hili likifika utafahamishwa tafadhali.^OK
Naomba tuwasiliane dm
 
Back
Top Bottom