TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Habari za muda huu wana Jamii,

Kuna baadhi ya vitu sivielewi kuhusu hawa TANESCO

1) Mtu unapohitaji huduma ya umeme unatakiwa kununua nguzo?

kwa sababu nikiangalia katika kijiji changu cha NAIBILI (Kilimanjaro wilaya ya Siha) mwananchi anatozwa shilingi 200000(laki mbili ) kununua nguzo , nje ya hapo kuna gharama nyinginezo kama 27000 kwa ajili ya mita bado kuna 30000 kwa ajili ya mkaguzi anayekuja kukagua nyumba yako kama inafaa kuvutiwa umeme.
kwa mantiki hiyo mwananchi anatakiwa alipie zaidi ya Tshs 250000.

Naomba mnieleweshe kama ni halali kwa mwananchi kununua nguzo ili nisije nikajichanganya.

Asanteni.

Naomba kuwasilisha.
Bas huko siha mnapgwa haswaa nnachojua ukilipia nguzo umelipa kila kitu mpaka mpaka ufungaji ila kwenye ukaguz kawaida hua wanataka li 10
 
Bas huko siha mnapgwa haswaa nnachojua ukilipia nguzo umelipa kila kitu mpaka mpaka ufungaji ila kwenye ukaguz kawaida hua wanataka li 10
mmmh yaani huku unalipia kila kitu yaani ishakuwa kero rushwa ipo nje nje utadhani TAKUKURU hawapo
 
Habari za muda huu wana Jamii,

Kuna baadhi ya vitu sivielewi kuhusu hawa TANESCO

1) Mtu unapohitaji huduma ya umeme unatakiwa kununua nguzo?

kwa sababu nikiangalia katika kijiji changu cha NAIBILI (Kilimanjaro wilaya ya Siha) mwananchi anatozwa shilingi 200000(laki mbili ) kununua nguzo , nje ya hapo kuna gharama nyinginezo kama 27000 kwa ajili ya mita bado kuna 30000 kwa ajili ya mkaguzi anayekuja kukagua nyumba yako kama inafaa kuvutiwa umeme.
kwa mantiki hiyo mwananchi anatakiwa alipie zaidi ya Tshs 250000.

Naomba mnieleweshe kama ni halali kwa mwananchi kununua nguzo ili nisije nikajichanganya.

Asanteni.

Naomba kuwasilisha.
Kulipa elfu 30 ni halali, kulipa elfu 27 na laki 2 nguzo iyo wanajua Tanesco mana ndo wanao toa gharama
 
Kulipa elfu 30 ni halali, kulipa elfu 27 na laki 2 nguzo iyo wanajua Tanesco mana ndo wanao toa gharama
Elfu 30 ya mkaguzi ni utapeli surveyor ni muajiriwa wa shirika anatakiwa asipewe chochote anatumia Gari la serikali ila Kuna malipo ya mchoro na contractor ambayo ni nje ya gharama za tanesco ndo mteja anatakiwa kulipa
 
Nimesoma malalamiko mbalimbali ya wateja wa UMEME! mm pia nikapata mstuko na kujaribu kufuatilia! Lkn pia nikasikia majibu yenu juu ya KILICHOITWA - unit za umeme kuisha kwa HARAKA -

Hii hali imetokea hivi karibuni, majibu yenu yalikuwa " hali hiyo inatokea kipindi hiki kwa kuwa wananchi wengi msimu huu wapo MAJUMBANI.

NILINUNUA umeme tarehe 19/12/2023 kwa tsh 20,000/= nikapata unit 51.9 KWH .matumizi ya hapa nyumbani ni
1 - rice cooker
2- pasi ( mara mojamoja jumapili)
3- feni vyumba 2 usiku kucha na mchana .
4- fridge
5- taa za kwenye ukuta ( fensi)
6- Tv
Umeme huu ulidumu siku 8.

Tarehe 27/12/2023 saa 20:32nilinunua tena umeme kwa tsh 20,000/= nikapata unit 42.1KWH

Matumizi yangu yamezidi kidogo kwani nimeongeza FENI jingine hivyo feni ziko 3 zinazokesha.

Fridge nilikuwa nalizima wakati wa mchana sababu ya joto kali lkn hivi sasa linafanya kazi muda WOTE.

Matumizi mengine yamebaki kama kawaida. Leo ni siku ya 10 umeme bado upo.

Tarehe hiyo hiyo 27/12/2023 saa 19:58 nilinunua umeme kwa tsh 20,000/= nikapata unit 56.1 KWH ( huu niliponunua sikuuona nilidhani umeshindikana nimeuona leo kwenye simu)

Kwanini 20 , 000/= unit 51.9 KWH
Kwanini 20 ,000/= unit 56.1 KWH

Iweje 51.9 unit Zitumike siku 8
Halafu 42.1 unit zitumike zaidi ya siku 10

NAWASILISHA
Ongeza earthlod kwenye nyumba yako usiweke moja kama mafundi wa zamani mwambie fundi wako akuwekee tatu na zikae kwa mfumo wa triangle umeme kupotea utapungua na utakaa na kuhusu umeme kutofautiana kwa same amount hua Kuna kua kukatwa Kodi ya pango kama umeanza kukatwa unit zinatofautiana ukienda kituo kikubwa utapewa risiti ukiisoma unaelewa ila kwenye simu ngumu kuelewa
 
Kama Kuna mtu ana changamoto ya umeme alete hapa ntajaribu kutoa maelezo kwa kile ninachokijua
 
TANESCO, Maji ya Chai, USA River, Arumeru, Arusha :
Siku ya jana mmekata umeme asubuhi na kurudisha majira ya saa 5 usiku. Leo pia mmekata pia asubuhi hii hatujui mtarudisha muda. Huu mbona ni mgao mkali sana? Tafadhali tunahitaji umeme ili shughuli zetu za uchumi zisiathirike!
 
Wafanyakazi wenu wanapokuja kutuunganishia umeme hasa unapopewa mita mpya wanadai malipo tena kwa nguvu!! Ndiyo utaratibu wenu ?! Mita si tumelipa kwa control number ?! Hizi wanazodai zinaenda wapi ?! Tena wanadai mpaka 50,000/= !! Tuwekeni wazi hapa.
 
Mkoa Tanga, Wilaya Tanga, kata mabawa B, mtaa Mikanjuni B, eneo maarufu makuburini mwisho, Jana nimeripoti Tatizo kuwa nyumbani kwangu umeme haupo( haufiki kwenye Mita) kutokana na loose connection kwenye nguzo ya Tanesco. Aidha, nimepewa reference number 5217413, hata hivyo mpaka sasa sijapigiwa Simu kuja kutatua tatizo. Namba yangu ya simu 0713673276. I look forward for positive feedback. Shukrani.
 
Tanesco hamuwezi kazi,leo taifa stars inacheza watu ilibidi wakae nyumbani na familia zao waangalie mpira,nyie mnakata umeme,kunduchi hakuna umemd,limekuwa kama shirika la mtu flani na anaamua anavyotaka kuhusu umeme,mnafaidika na nini umeme ukikatika? Kuna watu nahisi wanafaidika na kukatika huku labda
 
Mimi nina wasiwasi hawa wanafaidika na kukatika huku kwa umeme,mbona kipindi cha magu aliwabana na hii hali ikaondoka,tulikaa miaka 3 hakuna hili tatizo,na wakati alipoingia alilikuta akalikomesha,alivyoondoka limeanza tena[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787],hakuna mgao hawa ni janja janja tu na hajapatikana mdadisi wa kuwakamata tena janja janja yao
 
Back
Top Bottom