TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Maeneo ya Mbezi Beach Jogoo na Africana Umeme hakuna huduma ya Umeme tokea saa saa mbili asbh Hadi usiku huu.
Sisi wa kupata riziki kwa saloon na kuchomea tutaponea wapi
 
Donge tanga umeme umekata saa 5 mchana mpaka muda huu kiza, hili shirika limechoka! Inatakiwa waturudishie meter za zamani ambazo unalipia ulichotumia sio hizi luku ambazo unanunua ambacho hujatumia
 
TANESCO mlidai mnafanya marekebisho na kuongeza umeme kwenye grid hata hivyo tangu Hilo lifanyike mmekuwa mkikata umeme kwa muda mwingi zaidi... Arusha njiro umeme unaonekana kama ni upendeleo Fulani hivi... Jirani anaweza kuwa na umeme nyumba nyingine Giza...Hebu muwe wazi ... Shida ni Nini? Mnalazimisha watu kununua hayo majenereta au ??
 
TANESCO mlidai mnafanya marekebisho na kuongeza umeme kwenye grid hata hivyo tangu Hilo lifanyike mmekuwa mkikata umeme kwa muda mwingi zaidi... Arusha njiro umeme unaonekana kama ni upendeleo Fulani hivi... Jirani anaweza kuwa na umeme nyumba nyingine Giza...Hebu muwe wazi ... Shida ni Nini? Mnalazimisha watu kununua hayo majenereta au ??
Tumekusikia mkuu, tutalifanyia kazi. Ni baadhi ya wakurugenzi wetu wakijaribu kuwathibitishia wake zao kuwa wako kazini kwa kukata kata umeme
 
TANESCO SHENZI KABISA ....
SHIRIKA LIMEWASHINDA ...SHIRIKA LINA WASOMI HILI KWELI [emoji22]??
 
Hivi kwani hatuwezi kupata umeme sehemu nyingine zaidi ya Tanesco?
Mimi mwenyewe nlishawahi kuwaza hivyo ...Kwamba kuwe hata na Kampuny Shindani ya Umeme sio TANESCO peke yao ...kwasababu hawana sifa ya kukidhi mahitaji ya kitaifa.

Serikali itoe Fursa kwa Kampuni hata kama ni Binafsi !

Kunatakiwa kuwe na Ushindani wa kihuduma kwenye hii Secta .

La sivyo Hawa TANESCO watatuchelewesha kimaendeleo kama Taifa ....Umeme ni Nyenzo nyeti sana kiuchumi , kiulinzi na Usalama wa Nchi.
 
TANESCO miezi 6 mliyopewa na yule mama inakaribia kuisha badala tuanze kuona unafuu naona umeme ndo unazidi kukatika bila mpangilio...
 
Habari ya Leo jamani huu mgao wa umeme kahama unatisha hasa sir tuliepo Kanda y BULUNGWA hatujapata umeme wa uhakika kwa zaidi ya siku 5 masaa yanakwenda na umeme hakuna sijui tatizo ni nini na kahama hawatoi taarifa ya Nini chanzo tunataabika sana mpaka basi
 
Tarehe 19 January imefuka Kuna umeme mpya umeingia katika gridi ila mgao kahama hakuna nafuu tuombe mfunge substation ya umeme maana kwa Hali ilivyo ni mtihani
 
Tanesco inakuwaje katika Wilaya umeme uko makao makuu tu ukitoka nje ya mji hata km 3 haziishi hakuna huduma ya umeme. Hii ni aibu ya Shirika? Taifa? Au jamii husika?
 
Back
Top Bottom