TANESCO: Tuna upungufu, siyo mgao wa umeme. Wananchi endeleeni kuvumilia

Ushauri wa bure.
Maharage na MCHENGERWA wasiruhusiwe kuongea hadharani ili kulinda heshima zao.
 
Kitu anachofanya ndugu Maharage ni kumpaka punda rangi ili awe pundamilia
 


Upungu ndo uleta mgao, sasa anaongea nn
 
Kila kitu hii nchi ni kuvumiliaaa...!! Shwain kabisaaa mnakatwaaa...
 
Nchi hii tuna viongozi wa Ajabusana. Yaani Bwana Maharage Anaongea ujinga huu kwani wao kama Tanesko hawakuwaza miaka 10/20 nchi itakua na Ongezeko la Matumizi ya Umeme?

Yaani unakua na viongozi kama bwana Maharage Ambao hawana uwezo wa kuwaza miaka 50 mbele na kutafuta majawabu Badala Yake wanatafuta majawabu ndani ya tatizo hii nchi inafaa kuwekwa kwenye nchi bora yenye viongozi wasio fikiri na kutatua changamoto kabla hazijatokea.
 
Hakuna mgao
Ila Kuna upungufu kwa hivyo watu wanapata umeme kwa zamu.
Hivi tukipata umeme kwa zamu, si ndio mgao wenyewe hhuo?
Nhdugu maharage umekula maharage ya wapi?
[emoji1787][emoji1787]
 
Halafu kelele za kuuza nchi utazizuia wewe, serikali ikifanya hivyo watakuja akina mbowe waseme watanzania wenyewe tunaweza kujiendeshea mashirika yetu, then Tec nao wataandika waraka!!
Tatizo ni viongozi tuliowaweka madarakani, kwa kura zetu, kuteua washikaji kuendesha mashirika nyeti. Serikali ndio inapaswa kubinafsishwa iendeshwe na DP World ili waweze kusimamia uendeshwaji wa mashirika ya Umma: TRC, TANAPA, TPA, TIRDO, na baadhi ya Wizara km TAMISEMI
 
Inasikitisha sana hali ya umeme ilivyo, mjini ukipita kila mahali generator zimewashwa mnashindwa mchana kutwa na kelele za generator

Unarudi nyumbani jioni unakuta giza mtaa mzima, hapa napoandika ujumbe huu Niko gizani.

Hivi tunaelekea wapi?
 
Moja kwa moja..

Ndani ya wiki moja siku kama Nne pamoja na leo umeme umekatika kuanzia asubuhi unarudi saa 1 kasoro au mishale ya Saa 1 usiku.

Hali hii imepelekea shughuli nyingi kukwama, ukosefu wa maji, watu kulalamika nk nipo Dar lakini kama naishi kijijini Chimba unye.

Je, mtaaani kuna hali kama ya mtaa wangu au ipo mtaa wangu pekee ?

#UziTayari
 
Kwani we hukusikia ripoti ya uchunguzi iliyotolewa juzi?

TANESCO wamegundua maeneo ya buza buza kushuka chini huko hakunaga matumizi ya msingi ya umeme

Zaidi ya kuchajia simu afu zikijaa muanze kusumbua mitandaoni na habari za Yanga.
 
Kwani we hukusikia ripoti ya uchunguzi iliyotolewa juzi?

TANESCO wamegundua maeneo ya buza buza kushuka chini huko hakunaga matumizi ya msingi ya umeme

Zaidi ya kuchajia simu afu zikijaa muanze kusumbua mitandaoni na habari za Yanga.
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
 
Huo mtaa wako hauna jina?
 
Ndio utaratibu kipindi hiki cha jua kali...mgao
 
Ndio utaratibu kipindi hiki cha jua kali...mgao
Tanzania wananchi tunapata shida sana. Mchana inzi usiku mbu.
Sasa ukiangalia ishu ya umeme inaponyesha tu mvua tegemea umeme kukatika au kipindi kama hiki cha jua umeme unakatika pia.
 
Tanzania wananchi tunapata shida sana. Mchana inzi usiku mbu.
Sasa ukiangalia ishu ya umeme inaponyesha tu mvua tegemea umeme kukatika au kipindi kama hiki cha jua umeme unakatika pia.
Wananchi wa hali ya chini...makapuku...kajamba nani...walala hoi...wanyongwe...ndio tunapata shida
 
Mgawo wa umeme wa zamu hii ni mkali kuliko migao yote ambayo ilishawahi kutokea hapa nchini kwetu na duniani kote.

Mgawo huu ulianza kidogo kidogo mwezi Julai 2023 na kufikia mwezi August ukawa mkali ile mbaya hadi Mr January akaamua kuihama hiyo wizara.

Kinachosababisha huu mgawo TANESCO imekuwa haikisemi wazi. Inaogopa nini kukisema hata kama ni hujuma au ile software ya Mahindira iliyofungwa kwenye grid ya taifa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…