TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

Siyo Moshi tu, Morogoro pia umeme full kukatwa. Yani ni balaaa.
 
Soma namba mliipenda wenyewe
 

Wakuu palikuwa na uzi hapa:


Hii mambo ni nchi nzima. Yaweza kuwa ndiyo maana tumeingia mitini.

Beberu kaamua kutupiga kipapai kidogo.

Tuna kamdomo sana!

Hiiiiii bagosha!
 
Kila siku mnakata umeme. Sasa karibu saa tatu usiku tangu asubuhi hatuna umeme. Hamjali, mnatukejeli tukiwapigia simu, hampokei. Kalemani tusaidie
 
Hata hajafukiwa wanataka kuturudisha kwenye mgao
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni....kweli JPM aliwanyoosha. Mimi sijawahi kuwa mshabiki wa JPM.. na tangu aingie madarakani sijawahi kukaa gizani kiasi hiki.....huku mitaa ya Dodoma sehemu kubwa hakuna umeme na sasa yameshapita masaa matatu....eti kisingizio mvua iinyesha kidogo mara ukakatika....haijawahi kutokea for 5 years naapa. sasa wameanza kabla hata hajazikwa .... naona wanaturudisha zama za wataalam wa kutapisha maji mtera
 
Hehehehe
 
Kila zama na kitabu chake, wakati mikoa kama Dar, Morogoro, Tanga, kukatika umeme bila taarifa kwa masaa kadhaa karibia kila siku ni kawaida, Tanzania ni yetu sote wacha na nyie Dodoma, mjifunze maisha ya Tanzania wengine.

Mhm Rais Samiah Suluhu kaza mama kuna watu wanataka kuku sabotage ili miradi ya mwendazake uikomalie na wewe.

Maendeleo hayana chama!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…