Tanga ilitakiwa uwe mkoa wa pili kwa uchumi baada ya Dar Es Salaam

Labda tusaidie tafsiri sahihi ya umaskini. Huenda tuna tafsiri tofauti
 
Mpumbavu unajua hali yangu mimi naweza kukulisha na ukoo wako wote mwaka mzima, wacha dharau za kisenge hizo
kwa bahati mbaya uwezo huo huna na hata elimu hauna kwa sababu ungekuwa nayo ingekuwa imekukomboa, na pesa hauna, na hata matusi usingetukana ungetoa hoja. matusi hayo yanakuja kwa frustration zako za kimaisha na ninakusamehe bure.
 
Tena unaivunja heshima hiyo ID kwa kuleta maneno ya shombo, matajiri wala hawapigi kelele wewe ni kapuku tu unayenyanua mabega .
 
Tena unaivunja heshima hiyo ID kwa kuleta maneno ya shombo, matajiri wala hawapigi kelele wewe ni kapuku tu unayenyanua mabega .
sioni kama nimeandika chochote kibaya hapa tupo kujadili kwa hoja ila wewe ndiye unayetukana. au nakosea?
 
kwa bahati mbaya uwezo huo huna na hata elimu hauna kwa sababu ungekuwa nayo ingekuwa imekukomboa, na pesa hauna, na hata matusi usingetukana ungetoa hoja. matusi hayo yanakuja kwa frustration zako za kimaisha na ninakusamehe bure.
Wewe ungekuwa na elimu usingeleta hoja za kipumbavu kutoa sweeping statement kuwadharau watu wa Tanga tunakuona wewe fala tu na majivuno ya kishamba. Wenye fedha na elimu kubwa wala hawajitangazi bali matendo na kazi zao ndiyo zinawatambulisha hivyo wewe bwege tu.
 
sioni kama nimeandika chochote kibaya hapa tupo kujadili kwa hoja ila wewe ndiye unayetukana. au nakosea?
Rudia tena kusoma sentensi ya kwanza ya post yako # 70 uone kama inatoka kwa mtu anayejiheshimu. Ulileta maneno ya kipumbavu lazima ujibiwe kipumbavu
 
Mkoa umebarikiwa kila kitu
Sijui wagosi wanafeli wapi
Kabla na baada kidogo ya Uhuru, Mkoa wa Tanga ulikua ni Mkoa wa pili wenye uchumi mkubwa baada ya dar es Salaam.


Tanga iliporomoka baada ya zao la mkonge kumkosa soko duniani kitu ambacho kilipelekea Bandari kufa na hatimae viwanda vingi kama sio vyote kufa.

Kwa sasa zao la mkonge limefufuka baada ya ulimwengu kurudia matumizi ya mkonge dhidi ya plastic na Bandar unafanya kazi now japo sio kwa kiwango chake, ila Tanga itafufuka.

Kuhusu uvivu wa watu wa Tanga Sina cha kusema Zaid ya kuangalia utamaduni wa watu wa pwani wengi ni wavuvi na wa minazi ambayo haikuitaji kila siku kukuja mgongo na wavuvi wengi wanavua usiku
 
yeah a
yeah anajenga pale barabara ya 8 almost limefikia asilimia 95%
 
Umedadavua vema mkuu shukrani
 
Umeongea point,wabongo usipolima wanakuita we mvivu
 
hayo mandeleo yanatoka wapi wakati vijana kwa wazee wanashinda kwenye vijiwe vya story na bao
Mbona hata Arusha,Dar, Dodoma zinaendelea lakini wenyeji siyo walioleta mapinduzi makubwa ya maendeleo ?
Issue hapa ni serikali wameshindwa kupeleka maendeleo ya kweli, mashamba ya mkonge yamekufa, viwanda mbalimbali vimekufa/vimeuliwa, reli haipo tena, uwekezaji hakuna tena, bandari hakuna cha maana angalau miaka kidogo wamefanya maboresho.

Kwa hii nchi yetu, serikali ndio mdau mkubwa wa maendeleo, bila wao hakuna kitakachoendelea, case study Dodoma,Arusha na Dar.
 
Mkuu umetema madini adimu sana. Hapa watabisha watumwa wa mzungu tu maana wako radhi wauze bia feki ili waonekane nao ni watu kwa mawazo yao
Kama wewe ushajiwekea level na standard za juu za mafanikio kama biashara kubwa,magari na uwe na miradi mbalimbali ili ujiskie umefanikiwa ukimuona mwenzako ameridhika na baiskeli yake na kunywa kahawa unamuona kama loser na mvivu. Unatakiwa uishi ukijua kua kuna philosophy mbalimbali za maisha na kila philosophy ipo sahihi kwa jamii fulani.

Kuna kijiji cha kimasai walikataa umeme na maji sababu wanaamini mkileta umeme na maji waswahili(mmasai kila mtu mwingine anamuona mswahili) watakuja na kuharibu mfumo wao wa maisha na kupafanya eneo hilo sio la kimasai tena na kua la kibepari,Masai yupo Radhi abebe madumu na punda kufata maji ya kununua mbali tena ananunua kwa waswahili awape mifugo yake kuliko umletee maendelo hayo kwenye boma lake,hayo unayoona wewe maendeleo kwao sio maendeleo bali ni uharibifu wa mfumo wao wanouamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…