Tanga ilitakiwa uwe mkoa wa pili kwa uchumi baada ya Dar Es Salaam

Tanga ilitakiwa uwe mkoa wa pili kwa uchumi baada ya Dar Es Salaam

Mkoa umebarikiwa kila kitu
Sijui wagosi wanafeli wapi
Akuna Nchi au Mkoa unaoamini sana ushirikina ukawa na mafanikio, Tanga uchawi unauzwa hadi gulioni,Sasa hapo unategemea nini,Sehemu kama hizo labda haende mgeni ndio anaweza fanikiwa,lakini napo usijichanganye na wenyeji. No
 
Ukisiliza ile nyimbo ya wagosi wa kaya unaweza kudhani ni utani kumbe ndio ukweli
Tanga ya miaka hiyo ambapo hao jamaa waliimba wimbo huo na Tanga ya sasa ni kama mbingu ardhi!
Wimbo huo umetoka mwanzoni mwa miaka ya 2000 nadhani . Wakati huo Tanga ilikuwa haina usafiri wa daladala!.
Mimi nimeingia Tanga mwaka December 2004 na daladala nimezikuta na kwa sasa zimeongezeka.
 
Akuna Nchi au Mkoa unaoamini sana ushirikina ukawa na mafanikio, Tanga uchawi unauzwa hadi gulioni,Sasa hapo unategemea nini,Sehemu kama hizo labda haende mgeni ndio anaweza fanikiwa,lakini napo usijichanganye na wenyeji. No
Tanga jiji hakuna uchawi!
Mimi nimeoa jijini Tanga na watoto sasa ni wakubwa muda si mrefu nitapata wajukuu!
Mimi siamini habari za mahirizi kwahiyo watoto wangu tangu wanazaliwa hadi wanakuwa wakubwa hawajawahi vaa hirizi hata mara moja.
Sema maeneo ya Handeni kwa wazigua ndio kuna hizo tuhuma za kurogana lakini Tanga mjini hakuna habari za uchawi.
 
Tanga Haina chochote Cha kufanya iwe namba 2 Kwa Tanzania.

Sio rahisi kupita Mwanza au Mbeya ila hao kina Arusha na Moro watapitwa mwaka huu huu.

Uwepo wa Bandari na boda sio juhudi za watu wa Tanga Hadi useme inachangia sana kitaifa.
Kwenye hizo data ulizoweka Tanga ni ya 4 kwa kulipa kodi, hulipi kodi sana kwa kuwa na boda boda na tunajua Bandari si mapato ya Tanga yanahesabiwa juu kwa juu, hio kodi inalipwa vipi?

Jibu rahisi ni kwamba Tanga ina Viwanda na Biashara kubwa ambazo zipo systematically.

Na mifumo ikiwa rafiki Ni suala la muda mfupi mno Tanga kupita hio mikoa,

Nakupa mifano ya kampuni kubwa za watu wa Tanga ambao wameamua kuwekeza Nje sababu Tanga/Tanzania haieleweki
1. Pembe, wana kiwanda Tanga ila huwezi fananisha investment zao Kenya, Jamaa ni level za kina Manji na Gsm, Kenya ni maarufu sana na Wameteka soko la Hilo Nchi.

2. Tahmeed, tunayajua Mabasi yake na investments zake, moja ya kampuni kubwa zaidi Kenya

3. Tawakal jamaa wengine wa Tanga wenye investments kubwa Kenya

4. wapo wale matajiri wa Taqwa nao aka classic nao wamehamia KEnya.

hao wa 4 niliotaja net worth si chini ya nusu Trilioni,

wekezeni Tanga ipeni haki yake ya kimsingi soon utaona inawapita wengi tu.
 
Sawa ila mapato yanatoka zaidi mpakan na bandarini ambapo shughuli za wananchi ni chache.
unahisi hela za Bandari zinapitia Halmashauri ya Tanga? hazipitii, huyo ChoiceVariable anafahamu hilo ila anazingua tu, tushali discuss hilo humu.

soma hapo

tunakusanya kodi bilioni 300 bajeti ya jiji bilioni 25, nyengine zinaenda kujenga kwengine, hela inayokusanywa Tanga ingebaki kujenga mkoa tungekua mbali mno.
 
Hoja yako haina mashiko, Tanga ina bandari, pia Tanga ya siku nyingi huwezi linganisha na miji tajwa hapo juu.
wewe ndio hujui sifa za jiji, soma wikipedia, hii definition murua ya jiji

A city is a human settlement of a substantial size. The term "city" has different meanings around the world and in some places the settlement can be very small. Even where the term is limited to larger settlements, there is no universally agreed definition of the lower boundary for their size.[1][2] In a narrower sense, a city can be defined as a permanent and densely populated place with administratively defined boundaries whose members work primarily on non-agricultural tasks.[3] Cities generally have extensive systems for housing, transportation, sanitation, utilities, land use, production of goods, and communication.[4][5] Their density facilitates interaction between people, government organizations, and businesses, sometimes benefiting different parties in the process, such as improving the efficiency of goods and service distribution.

ukitoa dar hakuna jiji nchii hii inayolitendea haki neno jiji kushinda Tanga, tuichambue definition kwa vitendo.

1. extensive system ya housing
tanga imepangika, kuna taa za barabarani, nyumba zimepangiliwa, mitaa inaonekana, sehemu za kuishi zimetengwa, mitaa ya night club, mitaa ya family enterteinment etc hakuna shaghalabaghala, hakuna jiji nchi hii limepangika kama Tanga
481343406_942325031390881_3415335917463089788_n.jpg


2. Transportation
tanga kuna usafiri wote unaotumika nchi hii kuanzia treni, usafiri wa ndege, usafiri wa maji boat na meli za Bakhresa, usafiri wa Ardhini etc, kila sehemu ya jiji inafikika.

3. sanitation
tanga pengine ndio jiji pekee ambalo lina mifereji ya maji machafu level za Ulaya, mifereji size ya binadamu ambayo inakusanya uchafu wa jiji zima na kumwaga baharini, ukijenga nyumba huchimbi choo unalipia tu kwa mwezi majitaka unaunganisha system ya nyumba na system ya maji taka.

4. utilities
idara ya maji Tanga maji ni masafi, unakunywa kabisa, mara chache sana ndio unakuta maji yamechafuka, internet kila mahala, TTCL imecover jiji zima, wifi za kutosha, 5g, umeme wa uhakika, zimamoto etc tanga kuna hadi public garden, beaches na open space nyengine ambazo watu waliostaarabika wana chill.

5. production of goods and services
unafahamu viwanda vya Tanga nchi nzima kuna bidhaa kibao wanategemea Tanga ndio itengeneze.

so niambie wewe kwanini Tanga isiwe jiji na kwa kutumia vigezo gani vya jiji.
 
Ila Tanga inazidiwa na Morogoro na Kahama Kwa idadi ya watu Kwa matokeo ya sensa ya 2022 Hii hapa ndio Miji 25 yenye watu wengi Tanzania
sifa ya jiji ni kuwa na non-agriculture economy, watu wavutiwe na uchumi ambao sio wa kilimo, kuwe na huduma zote muhimu, watu wakiwa wengi for the sake ya kuwa na watu wengi ama uchumi tu kuwa mkubwa hakufanyi sehemu iwe jiji.

mfano mzuri ni moshi vijijini, kuna watu wengi balaa, mtu ana nyumba barazani analima migomba, uchumi upo vizuri, ila huwezi ita marangu ama Rombo jiji sababu pana dense population na uchumi mkubwa.
 
Back
Top Bottom