The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
Unatengenezwa mbona enzi za ukoloni haukuwepo huo uvivu maana mji wa Tanga ulijengwa na mkoloniSababu gani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unatengenezwa mbona enzi za ukoloni haukuwepo huo uvivu maana mji wa Tanga ulijengwa na mkoloniSababu gani?
Tanga na Kahama wapi kunastahili kuwa Jiji?sifa ya jiji ni kuwa na non-agriculture economy, watu wavutiwe na uchumi ambao sio wa kilimo, kuwe na huduma zote muhimu, watu wakiwa wengi for the sake ya kuwa na watu wengi ama uchumi tu kuwa mkubwa hakufanyi sehemu iwe jiji.
mfano mzuri ni moshi vijijini, kuna watu wengi balaa, mtu ana nyumba barazani analima migomba, uchumi upo vizuri, ila huwezi ita marangu ama Rombo jiji sababu pana dense population na uchumi mkubwa.
Kumbe unatetea wakwe na siyo hoja, Tanga kuna bandari, misitu, matunda, mkonge n.k, pia tangu ukoloni Tanga ilikuwepo, nataka utaje wazawa matajiri wa Tanga tofauti na waarabu+ wahindiMusoma, Bukoba, Shinyanga, Tabora na Songea sio mikoa ya siku nyingi?!
Wewe nchi hii unaijua au ni mkimbizi umeigia TZ mwaka jana?!
Halafu hapo bandarini wafanya kazi ni maroboti , watu wa mikoani au kazi za bandarini zinafanywa na watu wa hapohapo Tanga?!
By the way Mimi ni mzinza kutoka Biharamulo mkoani Kagera ila nimeishi jijini Tanga miaka 9 (2005- 2014 ) na huwa natembelea Tanga kila baada ya muda fulani kwasababu hapo jijini Tanga niliacha watoto.
Sasa jiji la Tanga ninalijua vizuri na wakazi wa jiji hilo pia nawajua vizuri kwasababu ni wakwe na shemeji zangu.
Ndiyo umetengenezwa, watu wa Tanga wapo hata mikoa mingine, kazi kubwa kwao ni uzinzi na umbeaUnatengenezwa mbona enzi za ukoloni haukuwepo huo uvivu maana mji wa Tanga ulijengwa na mkoloni
Mkuu twende kwenye hali za wananchi acha na mbwembwe za kupanga miji, hata Karatu imepangiza vizuri sn, mji(makao makuu ya Mkoa) gani Tanzania maji ni ya shida? Moshi maji mpk vijijini n.k hali za kiuchumi za wananchi wa Tanga zikoje?wewe ndio hujui sifa za jiji, soma wikipedia, hii definition murua ya jiji
A city is a human settlement of a substantial size. The term "city" has different meanings around the world and in some places the settlement can be very small. Even where the term is limited to larger settlements, there is no universally agreed definition of the lower boundary for their size.[1][2] In a narrower sense, a city can be defined as a permanent and densely populated place with administratively defined boundaries whose members work primarily on non-agricultural tasks.[3] Cities generally have extensive systems for housing, transportation, sanitation, utilities, land use, production of goods, and communication.[4][5] Their density facilitates interaction between people, government organizations, and businesses, sometimes benefiting different parties in the process, such as improving the efficiency of goods and service distribution.
ukitoa dar hakuna jiji nchii hii inayolitendea haki neno jiji kushinda Tanga, tuichambue definition kwa vitendo.
1. extensive system ya housing
tanga imepangika, kuna taa za barabarani, nyumba zimepangiliwa, mitaa inaonekana, sehemu za kuishi zimetengwa, mitaa ya night club, mitaa ya family enterteinment etc hakuna shaghalabaghala, hakuna jiji nchi hii limepangika kama Tanga
View attachment 3250963
2. Transportation
tanga kuna usafiri wote unaotumika nchi hii kuanzia treni, usafiri wa ndege, usafiri wa maji boat na meli za Bakhresa, usafiri wa Ardhini etc, kila sehemu ya jiji inafikika.
3. sanitation
tanga pengine ndio jiji pekee ambalo lina mifereji ya maji machafu level za Ulaya, mifereji size ya binadamu ambayo inakusanya uchafu wa jiji zima na kumwaga baharini, ukijenga nyumba huchimbi choo unalipia tu kwa mwezi majitaka unaunganisha system ya nyumba na system ya maji taka.
4. utilities
idara ya maji Tanga maji ni masafi, unakunywa kabisa, mara chache sana ndio unakuta maji yamechafuka, internet kila mahala, TTCL imecover jiji zima, wifi za kutosha, 5g, umeme wa uhakika, zimamoto etc tanga kuna hadi public garden, beaches na open space nyengine ambazo watu waliostaarabika wana chill.
5. production of goods and services
unafahamu viwanda vya Tanga nchi nzima kuna bidhaa kibao wanategemea Tanga ndio itengeneze.
so niambie wewe kwanini Tanga isiwe jiji na kwa kutumia vigezo gani vya jiji.
Wewe ndiye umeelezea vizuri uhalisia kwani wengine hata historia hawajui na wanatoa comment za chuki tuSijui ndugu mwandishi unaongelea Tanga as mkoa au Tanga as mji, kwa Tanga as mji ni mji ulianza tangu mwaka 1890 wajerumani walipo ingia, Mji wa tanga ulipata hadhi ya kuwa manispaa tangu 1930, tokea hapo tanga ulikuwa mji kimbilio na namba moja kwa uchumi tanganyika mpka tunapata uhuru, mji wa tanga uliumbwa kwa mfumo wa capitalistic town, yaan walikuwepo watu na kampuni nyingi zenye nguvu ambazo ziliubeba uchumi, nani haikumbuki amboni na product zao kama ndoo za amboni na ndala za umoja? Uchumi wa kikapitalisti ulileta watu wengi tanga ili kufanya kazi, mji ulikuwa na mkoa ulikua miaka ya 70 mpka 80 sera za mwalimu nyerere ndio ziliua mji wa tanga na uchumi wake, azimio la arusha ndio lilimaliza kabisa uchumi wa pale, isingekuwa rahisi mji wenye uchumi wa mtu mmoja na makampuni ghafla ubadili upeo uwe mji wa kijamaa, walowezi wote waliikimbia tanga kwenda kenya, uingeleza na marekani, tanga kwa sasa uwekezaji una rudi taratibu, uchumi wa pale utakua, saivi wageni ni wengi, wenyeji siku zote huchelewa kujua kukimbizana na uchumi, ila soon uchumi wa kikapitalisti uta take over, sasa hivi wafanya biashara wenye asili ya ki asia wameanza jenga majengo marefu mjini, nina jamaa angu eng. Kwa mara ya kwanza ana tenda tanga ya kujenga jengo la orofa 10 pale mjini, jengo la wahindi, wale jamaa walinyang'anywa majengo yao yote mijini na sera ya kutaifisha, sekta ya ujenzi nayo huchangia uchumi
Tutake radhi mkuu kama umeona mmoja au wawili wako hivyo hizo ni tabia binafsi lakini siyo tabia za jumla za watu wa Tanga.Ndiyo umetengenezwa, watu wa Tanga wapo hata mikoa mingine, kazi kubwa kwao ni uzinzi na umbea
Mkuu kama wewe unatokea Tanga basi yaishe, nikimuona Makamba na Aweso napata wasiwasi na uwezo wenu watu wa Tanga. But wewe ni mchapaka kazi mkuuTutake radhi mkuu kama umeona mmoja au wawili wako hivyo hizo ni tabia binafsi lakini siyo tabia za jumla za watu wa Tanga.
Muulize akutajie vigezo vya kuwa jiji kama atarudi tena, watu wamejawa na chuki na kutoa kauli za jumla jumla bilakufanya tafitiMoshi inanyimwa hadhi ya jiji kwa sababu za kisiasa tufanye ni kweli!.
Je Musoma, Bukoba, Shinyanga, Kigoma, Songea , Tabora na Singida pia wamenyimwa hadhi ya jiji kwa sababu za kisiasa au hao nao ni wavivu kama watu watanga vile mnavyodai na wameshindwa kuwa machawa kama watu wa Tanga ili wapewe hadhi ya jiji?!
Waambie waambie hao wakujaWanakuja kula nyumbani kwenu?!
Nani anawanunulia chakula?!
Au ulishasikia serikali inapeleka Tanga chakula cha msaada?!
Na kama iko nyuma kiuchumi kwanini ikapewa hadhi ya jiji tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000?! Unajua kuwa Moshi wanaomba manispaa ipewe hadhi ya jiji na hadi Leo serikali inawazungusha kwakuwa vigezo haviridhishi?!
Wacha uongo soko gani umekuta wanauza uchawi?Akuna Nchi au Mkoa unaoamini sana ushirikina ukawa na mafanikio, Tanga uchawi unauzwa hadi gulioni,Sasa hapo unategemea nini,Sehemu kama hizo labda haende mgeni ndio anaweza fanikiwa,lakini napo usijichanganye na wenyeji. No
Halafu wakitoka vijiweni na kwenye bao wanakuja kula nyumbani kwako?!
Moja ya sifa ya watu wa Tanga ni utanashati wa kupenda kuvaa vizuri, je nguo wanazovaa wanatoa wapi wakati wanashinda kwenye bao na vijiweni?!
Je ulishafika Tanga ukakutana na mtu mwenye akili timamu yuko uchi?!
Nguo za kuvaa wanatoa wapi?!
Au ulishasikia serikali imepeleka Tanga chakula cha msaada na nguo za kuvaa kwa watu wa Tanga?!
Mkuu jamaa wanauchukulia poa mkoa wetu!Wanakula nyumbani kwako?! Nguo wanazovaa wanapewa na nani?
Ulishasikia serikali imewapelekea chakula na nguo za msaada?!
Mbona mbona manispaa yao imepewa hadhi ya jiji Tangu 2005 wakati Shinyanga,Bukoba,Musoma, Singida, Sumbawanga,Songea, na Kigoma Bado ni manispaa?!
Kwanini mji wa watu wavivu ipewe hadhi ya jiji sawa na Arusha, Mwanza, Mbeya na Dar?!
Tungekuwa na utawala wa majimbo Tanga ingekuwa mbali sana. Mwalimu Nyerere ndiye aliidogosha Tanga tena kwa makusudi kabisa .unahisi hela za Bandari zinapitia Halmashauri ya Tanga? hazipitii, huyo ChoiceVariable anafahamu hilo ila anazingua tu, tushali discuss hilo humu.
soma hapo
Pre GE2025 - Jiji la Tanga limepitisha rasimu ya bajeti ya Tsh. bilioni 25 kwa mwaka wa fedha 2025/2026
Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Jiji la Tanga limepitisha rasimu ya bajeti ya Tsh. bilioni 25 kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.491 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/2024, ambayo ilikadiriwa kukusanya Tsh. bilioni 21 kutoka mapato ya ndani. Akizungumza...www.jamiiforums.com
tunakusanya kodi bilioni 300 bajeti ya jiji bilioni 25, nyengine zinaenda kujenga kwengine, hela inayokusanywa Tanga ingebaki kujenga mkoa tungekua mbali mno.
Bila mapenzi wewe ungezaliwa? Wacheni chuki na sweeping statements za kuwadharau watu wa Tanga usikute nyie mumezaliwa kwenye nyumba za tembe lakini mnaitukana Tanga.Wanadeal na Mapenzi tuu
Kumekuchaaa!!Nyumba mganga, nyumba mchawi, nyumba shoga.
Kwa lugha fasaha ya Kitanga hao tunawaita wanyika (waporipori)Waambie waambie hao wakuja
Kiwanda cha soda cha Healtho ni one of the best product from Tanga. Toka enzi na enzi Tanga wana soda yao leo watu wanaidharau tangaBila mapenzi wewe ungezaliwa? Wacheni chuki na sweeping statements za kuwadharau watu wa Tanga usikute nyie mumezaliwa kwenye nyumba za tembe lakini mnaitukana Tanga.
Unajua kuna aina fulani ya ujinga ambao huwezi kuutibu hata kwa elimu, na wewe rafiki yangu unaonesha dalili zake zote. Unaposema eti “watu wa Pwani ni wavivu” unadhihirisha ujinga wa kihistoria ulioletwa na mkoloni na kupewa watu wa bara kama zawadi ya upumbavu wa kizazi. Umefundishwa kushabikia propaganda ya mkoloni bila hata kujua historia ya nchi yako.Mikoa ya kanda ya ziwa kama Kagera,Geita,Mwanza,Mara n.k ina kila kitu na pia watu wake Mwenyezi-Mungu alitubariki huwa tuna akili-kubwa.Hii mikoa ikiacha kuhujumiwa na serikali,itauzidi hata mkoa wa Dar es Salaam. Kitu pekee ambacho Dar es Salaam wanaizidi mikoa mingine ni bandari tu na ujinga ujinga mwingi wa watu wa pwani kama wazaramo.