Tanga jiji la kishamba sana, nashindwa kuelewa kwanini mkoa huu ulipewa heshima ya kuitwa Jiji

Tanga jiji la kishamba sana, nashindwa kuelewa kwanini mkoa huu ulipewa heshima ya kuitwa Jiji

Povu la nini kaka? Kwa kifupi mji wa Tanga umejaa umasikini wa kutisha
.
Screenshot_20181007-120621.jpeg
 
Tanga hamna kitu...ilikuwa inategemea bandar...baada ya bandar ya dsm kuchukua nafas...mji ukafa na hautainuka tena (ukweli Mchungu) why? Kwanza hakuna rasilimali yenyr nguvu ya kuvuta mkusanyiko wa watu Pili Mzunguko mbovu wa biashara kutokana na kuwa kat ya two giant cities Dsm and Arusha...Tatu wakaz wenye kipato hawana asili ya tz na kamwe hawawekez nchin wanachopata wanapeleka kwao...Nne Wakazi wa Tanga hawathamini Elimu
.
Screenshot_20181007-120621.jpeg
 
Nimekuwa jijini Tanga kwa siku mbili tatu hivi. Siyo mara yangu ya kwanza kufika, ila kila nikifika huku huwa nashangaa kwa nini huu mkoa unaitwa jiji.

Mji wenyewe mdogo halafu halafu watu wamezubaa sana.

Utashangaa ukipanda boda boda ikifika kwenye mataa hata kama yuko peke yake anasubiri taa ya kijani. Yaani hawajali muda.

Nyumba za udongo mpaka kati kati ya mji, vighorofa vya kuhesabu.

Ila nasikia huu ni kati ya miji iliyokuwa maarufu hapo zamani.
6a50c16763ce2d5a7a929366cf1443e1.jpg
Miji mingi bado sana japo imepewa heshima hiyo
 
Mleta mada unalijua jiji la Frankfurt? Kama hulijui rudi tena Tanga utaona image ya Jiji Hilo la Ujerumani. Wajerumani hawakurupuki mzee baba...ramani ya Mji wa Tanga ni copy ya Frankfurt. Ovaaaa!!
 
Unasema hivyo kwakua umetoka Dar,
Ila ukiishi nje ta Tz hasa EUROPE au America ukija Dar nako utasema hivihivi
 
Kwa maoni yangu Tanga ndio mji uliopangwa vizuri zaidi Tanzania. Yaani pale hata magari yawe mengi vipi hapawezi kuwa na foleni, LAKINI SASA mji umepooza, mtaani kumepooza, nyumba za makuti hadi mjini kabisa, mitaani vitu vingi hakuna.
Kwa wali wa nazi na vyakula vitamu, it's next to none!
 
Back
Top Bottom