Tanga: Milioni 21 waliyoiomba Wazee kwa ajili ya Tambiko yakwamisha Ujenzi wa Barabara

Nyuma ya Wazee kuna 'Wazee' na ndio wenye kutaka kula hizo tozo
 
Barabara ya kupita wenyewe wanataka wahongwe kuondoa madudu yao
 
Unaweza ukastaajabu, lakini ndio ukweli. Barabara ni kwa ajili ya wananchi wenyewe, lakini wananchi wenyewe ndio wanahitaji walipwe pesa ya kufanya tambiko ili barabara ipite.

Je, ni lazima barabara ifanyiwe tambiko? Isipofanyiwa haipitiki?
Your browser is not able to display this video.


Note: Ukisikiliza hii video vyema ni kama kuna harufu ya upigaji. DC ana figure ya 21 M, ila mzee anasema kwenye vikao walikubaliana 15M.
 
Wapeni wazee wa kwa Msisi, mbona wamepunguza kutoka mil. 21 hadi 15? Wapeni fidia ya maeneo yao sio lazima mkute majengo, hayo mnaona miti na mapori ni makazi yao ya mizimu.

Sent from my G3121 using JamiiForums mobile app
 
Angalia matambiko yalivyo na nguvu! Uliletewa utamaduni wa kizungu kwamba Mungu kagawanyika katika nafsi tatu ukaitikia "ndio mzee" ni uuuuungwana?
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Ushenzi wa namna hii ndio ulikuwa unamfanya waziri wa barabara wa miaka hiyo (JPM) kuhamisha kabisa njia
 
Wapeni hao wazee wapunguze njaa.mbona za kununua ndege na wapinzani zipo
 
Kwa nini uite mapepo mkuu?
Hiyo ni elimu pana sana kwenye maandiko matakatifu. Kwa kifupi, ni Malaika waliohasi na wako busy kututoa kwenye mstari wa kumuelekea Mungu wetu.
Na labda tunaweza tusiwe na uelewa wa kutosha kuhusu viumbe hivyo na tulivyonanyo kwenye maisha yetu ya kila siku lakini vipo. Na sio kwa Waafrika tu bali Duniani kote. Na kweli vina uwezo na hao Mababu wa Matambiko wanalijua hilo vizuri.
Hatahivyo suala la kuwafuata ama kuwategemea ni uamuzi wa binadamu.
Na ndio kurahisisha mambo Amri ya kwanza Mungu inatuambia tusiabudu “miungu” wengine.
 
wasipewe hata mia, wasilete mambo ya ovyo ovyo. Pesa ya kuitia mizimu yako unataka ulipwe na serikali
 
Nimeisikiliza ile clip, nimegundua wazee wako sawa asee

21m ni kiasi kidogo sana kwa kitakachoenda kufanyika hapo

na kama serikali ikidharau, hata kama barabara itafanikiwa...

Tutashuhudia ajali za ajabu ajabu sana maeneo hayo

Nashauri serikali wawe wapole tu, hiyo pesa ni ndogo sana mbele ya mizimu ya mababu zetu.
 
Halafu mimi nimeshangaa hawa wazigua wenzangu wameanza kuijua hela kuanzia lini?

Maana hata ukienda kuoa kule mahali huwa ni sawa na bure!

Ukienda kuaguliwa bei sawa na bure!

Sasa hilo dau la ma milioni chungu nzima hayo tangu lini?!

Lini wameanza kuijua hela hawa wagosingwa?
 
Wazee wamechoma kuachwa nyuma kwenye 10%wameona wajiongeze waiombe kwa njia mbadala big up wazee
 
Ukishangaa ya musa.... hawa wazee ni wazee wahuni tu hapo ndipo namkumbuka mwendazake, angekuwepo wala wasingeleta ujuha huu. Hawa hawataki maendeleo hakuna haja ya kuwabembeleza pitisha barabara kwingine halfu waone wajukuu wao wakijifungulia maporini kwa kukosa usafiri, ukikosa barabara maana yake utakosa soko la mazao yako,hata umeme wataukosa sababu hizo nguzo zitasafirishwa na nini, watu wa Tanga wamejawa na imani za kishirikina sana.
 
Hii nchi tunaelekea pabaya sana aisee.

Tunafikia hatua ya kuamini mambo ya kishirikina hadi kutumia mamilioni ya wananchi kuyapeleka milima korelo?
We huna heshima kwa Chifu Hangaya eenh??kuna kitu natafuta.HESHIMU MACHIFU!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…