Tanga: Milioni 21 waliyoiomba Wazee kwa ajili ya Tambiko yakwamisha Ujenzi wa Barabara

Hii nchi tunaelekea pabaya sana aisee.

Tunafikia hatua ya kuamini mambo ya kishirikina hadi kutumia mamilioni ya wananchi kuyapeleka milima korelo?

WITCHCRAFT AND THE GOVERNMENT IS NEGOTIATING?! ASTONISHING.
 
Hio ni dili.... Lazima kuna watu nyuma ya hao wazee...

Kwani lazima barabara ipite hapo si wahamishe uelekeo tu...
 
Wewe acha kujipendekeza sio Mzigua,Wazigua tunaijua pesa kabla wewe huna dalili ya kuja Duniani
 
Hao wanaotaka mamilioni kwa ajili ya tambiko ni wahuni na wahujumu uchumi.
Walete break down ya hayo mamilioni tuone
Isije kuwa kuna asilimia kadhaa za viongozi wa serikali waliopanga huo mchongo wa kudai mamilioni ya tambiko.
Waambieni hao wazee barabara inajengwa kwa faida yao na watoto wao waache ungese.
 
Ndo umeamishwa hivyo na umekubali kuamini mkuu, siwezi kukubadili imani yako.

Ila kwangu mimi matambiko si mapepo yalikuwepo toka enzi na enzi. Huyo mkuu wa wilaya si mjinga kunegotiate na hao wazee, lazima watakuwa wamejaribu wameshindwa.

Nimeshuhudia visa kadhaa kwenye ujenzi kugoma maeneo ya matambiko.
 
Uwe na siku njema.
 
Huu ujinga na upumbavu ndo unasababisha nchi hii isiendelee!

How comes Mkuu wa Wilaya anazungumzia watu kulipwa hela za serikali ili wafanye tambiko???

Kama hawataki barabara kwa nini mnawapelekea? Waacheni na uchawi wao waendelee kuwa masikini na izo fedha za barabara pelekeni sehemu wanapojua maana ya maendeleo!


 
Tunaanza kuweka mambo ambayo baadae yanaweza kuleta matatizo katika kutoa maamuzi. Ukishakubali hayo matambiko yafanyike huko, huoni sasa matambiko mengi tu yatatokea sehemu nyingine za nchi? Je, katika Sheria ya Manunuzi tambiko linakadiriwaje? Hivi CAG atahakiki vipi gharama za hii kitu na kutoa thamani ya fedha kwa kazi ya tambiko lililofanyika?
 
Hivyi Mbunge na mawaziri kutoka Tanga wameshindwa kuwaelimisha Hawa wachawi? Au na wao wanajipatia chochote Kama ulivyosema.
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…