Tanga: Mjamzito afariki dunia kituo cha afya kwa kukosa Tsh. 150,000

Hiko kituo Cha Afya, kuanzia Mganga mfawidhi mpaka hao wapuuzi walompokea, Wasimamishwe kazi Mara Moja, na wafikishwe mahakaman.

Muongozo wa Serikali, huduma za Upasuaji Kwa Wamama Wajawazito ni BURE.
 
Kazi za utabibu zinahitaji watu wenye mioyo sana, sasa unakutana na lijitu limaskini lina madeni ya kausha damu, mwingine kazalishwa kaachwa yaani lazima roho iwe usugu wa kuzoea kuyaona maumivu ya wengine.
Uhudumu wa afya ni kazi kama kazi zingine watu wanafanya ili iwaingizie kipato ,msipende vya bure kwenye fani za watu.

Hao mpaka kufika hapo walipofika wametumia gharama kubwa sana pamoja na muda wao.
 
Serikali inabdi kurekebisha Sera zake sasa iki ziendane na Matakwa ya wananchi hapo kitambo kidogo Tanga kulkulwa na Bima ya Wajawazito wakaiondoa ingemsaidia sana..
 
Mungu amlaze pema uyu mama kichanga kwa kifo kichungu alichokipata kule Tanga
Nasikitishwa na serikali kutopata ufumbuzi endelevu wa majambo haya sugu.

Hatua ya kumuadhibu daktari aliyekuwa zamu, mtu wa usingizi na nesi wake sio suluhisho na kama kuna mwenye hoja naomba anijibu awa wa3 mnahisi ndio walioanzisha utaratibu wa wajawazito operesheni walipie 150k au ni wagonjwa wote hapo hospitalini.

Na lingine tatizo mnahisi ni kuacha kumuhudumia kisha alipie kifo kikamuwahi au malipo yoyote hakustahili kuyafanya kwakuwa serikali inatoa vifaa tiba na madawa kwenye madirisha ya madawa ya vituo vya afya vitolewe bure kisha viongozi wa hospitali wanaandaa utaratibu na risiti wateja wanapatiwa katika kuwachaji awa wagonjwa.(NARUDI)
 
Hiko kituo Cha Afya, kuanzia Mganga mfawidhi mpaka hao wapuuzi walompokea, Wasimamishwe kazi Mara Moja, na wafikishwe mahakaman.


Muongozo wa Serikali, huduma za Upasuaji Kwa Wamama Wajawazito ni BURE.
Mkuu una huo Muongozo unaosema huduma za upasuaji ni bure?
Wakati kwa Sasa Sio tu C/S mpaka kuzaa kawaida kwenye Hospitali kuanzia Ya wilaya kwa Sasa wanalipia?
Na sio aajawazito tu hata watoto pia Ile sera Ya under five imekuwa Sanamu kwa wananchi lakini kwa Serkali ni Kama imefutwa na ukikutwa umetibu mtoto hata Underfive mwenye miezi miwili au mmoja utadaiwa pesa na upewe kesi za kuhujumu uchumi...

Ni wakati sasa Wananchi sio kuilalamikia Hospitali bali wailalamikie Serikali kwa uundaji wa sera mbovu
 
Hamna kitu kama hiko, huduma za Upasuaji Kwa Wajawazito , Serikali inazilipia yenyewe.

Uchunguzi ufanyike
Duh huu upotoshaji huwa unanipa Hasira sana na ndo mara nyingi unasababisha majanga kwa watu kutokujiandaa mwisho wa siku akija akaambiwa unatakiwa kulipia Hana hata 100 kutokan na aliambiwa na fulani anateishi naye jirani kuwa ni bure...

Nafikiri unapaswa kupewa Elimu kuhusj maswala ya afya na sera zake kabla ya kucomments hivyi
 
Oyaaa , C-SECTION ni Bure .

Kwa uchache tu labda aambiwe kununua baadhi ya Dawa na vifaa tiba na ambayo haifiki hata Elfu Hamsini.

Tena , Ikiwa Mama Hana hata mia mfukon, ni lazima Apate huduma, ni LAZIMA, kwamba Kituo hiko Cha Afya kilikoswa Dawa na Vifaa tiba mpaka Marehem huyo aambiwe mpaka atoe Laki na hamsini??.


Uzembe ulofanywa na hao Wahuni wasojua wajibu wao ni lazima Tuupinge , MWANAMKE HATAKIWI KUFA KWA SABABU YA MIMBA AU COMPLICATIONS ZA MIMBA.
 
Nlipo nazifanya hizo , ni Bure hawalipii hata thumuni.
 
Oyaaa , C-SECTION ni Bure .

Kwa uchache tu labda aambiwe kununua baadhi ya Dawa na vifaa tiba na ambayo haifiki hata Elfu Hamsini...
Sawa Hebu nipe hiyo Sera inayosema hivyo Maana huku Katiak Hospitali tuna sera Tofauti ya Malipo kwa C/Section na kuna Muongozo mwingine wa malipo kwa Watoto uliotoka Since 2021 sasa ndo maana nataka kujua wewe huo muongozo Ni upi unautumia kusema C/Section ni bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…