Tanga: Mjamzito afariki dunia kituo cha afya kwa kukosa Tsh. 150,000

Tena hiyo ndogo...mi nilipigwa laki 2 na nusu tena serikali....wakataka nigomea bima nikasema nawashtaki...ndiyo kuogopa
Poleni mliopata operation pengine ni Kwa vile Mimi na ndugu zangu tuna bahati sijawahi kukutana na hiyo kadhia.
 
Kweli kabisa. Watu vijijini wamezoea kujifungia kawaida nauli tu ya kwenda hospital hamna ni anaenda Kwa miguuu jamaa anafanya masihara.
 
Kwa hiyo Dr. Walichokifanya hao wahudumu wako sawa au?
Ethically hawakuwa Sawa hata thumni ila systematically wako sawa ...

Kwanini kun vita kuu mbili kubwa hapo Ya kwanza ni ethics Hapo akipelekwa kwenye vikao vya Baraza la Taaluma kafanya Negligence iliosababisha kifo so yuko Hatiani..

Lakini lets Assume alimtibu mgonjwa na hakutoa hela hiyo ni vita nyingine ya Pili ni vita ya kimapato ambayo ndo hiyo vita ya system..
Haya matukio huwa ni magumu sana kuamua ikifika hapa..

Ndo maana kuna muda me nagombana na watu sana ni bora kutoa na kumuombea mgonjwa temporary Exemption hata kama itakucost Posho yako ila sio Kusababisha kifo
 
Naisikitikia nchi yangu , nahuzunika maana wabaya ni sisi , wazuri ni wao .

Siasa ni mbaya sana
 
Kwani utaratibu wa malipo ya matibabu si huwa inaandikwa bill halafu mgonjwa analipa baada ya matibabau?.

japo siyo lazima kama mgonjwa anao uwezo wa kulipia kila kitu baada tu ya kuandikiwa pesa anayotakiwa kulipa
 
Uzembe ulikuwepo upande wao ila Bado walihitaji kusaidika!
Sasa umeshasema msaada, msaada huwa ni hiyari sio lazima.

Na mara nyingi hizo case za C/S huwa ni elective kwa hiyo mtu anajua kabisa inabidi ajiandae , kwa kukosa yeye pesa asiwape watu lawama.
 
Hakika featuring hatari sana 🤣🤣🤣🤣🪑
 
Uhai kwanza na kuhakikisha mtoto na mama wako salama mengine baadae
Kifo kipo ila huyo wamemuua na kichanga chake
Waafrika makatili sana
Mama mtu anaona mwanae na kijukuu wanakufa huku wauguzi wanamtukana na kumuambia leta hela hii ni zaidi ya ushetani kwa kweli

Kama mpaka saa hii hawajawajibishwa basi wote ni wanyama tu
 
Maana wale watabibu wao wamefuata sheria.Ninashangaa kwa nini Waziri wa afya kawasimamisha.Sasa serikali si Iseme kuwa matibabu ni bure.Yaani hao watumishi wakishtaki wanashinda hii kesi.
Nchi inaendeshwa kisiasa sana.

Yani halafu sijui kwa nini watu wanashindwa kuelewa kwamba watoa huduma za afya ni waajiriwa kama waajiriwa wengine, yani linapokuja suala la mambo ya afya naona watoa huduma za afya wakikandamizwa sana wakati makosa yanaanzia huko juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…