Tanga: Mjamzito afariki dunia kituo cha afya kwa kukosa Tsh. 150,000

Tanga: Mjamzito afariki dunia kituo cha afya kwa kukosa Tsh. 150,000

Kesi za watu wa afya kama hukuwepo eneo la tukio usiwe mwepesi sana wa kuhukumu.

Serikali inanadi huduma bure kwa mama na mtoto, sasa wewe zidisha msamaha kituoni kwako ndio utajua hujui.

Yote kwa yote, kabla ya kuwa mjamzito au ukiwa mjamzito jiandae vyema vinginevyo hutafurahia kabisa ukienda hospitali na utalaumu wasiostahili.

Kwetu huduma ni bure, kujifungua kawaida au kwa upasuaji na vifo vya uzazi ni nadra sana kutokea lakini bure hii ni mzigo kwa kituo, kuna haja sasa serikali ibadilishe hii sera kwani haiendani na uhalisia.

Pole sana kwa wafiwa, Mungu awafariji.. pia haki itendeke kwa watoa huduma.

Watu wa afya tujifunze, tumeshakuwa sikio la kufa na sisi ndio mbuzi wa kafara.
 
Mkuu acha kulinganisha maisha Yako na wengine mkuu ,familia zingine kupata hata Hiyo laki Hadi ukoo mzima ukae vikao zaidi ya vitatu .
Hawa vijana hawajui maisha huko maporini, mtu anakosa hata hela ya kibaba cha mafuta, yaani hela ni mpaka tena msimu wa mazao. We Angalia hata vibanda wanavyoishi.
 
Watoa huduma ya afya wapo sahihi.

Hivi kuna sehemu unaweza kwenda ukahudumiwa bure? .

Wahudumu wa afya ili wapate pesa ni lazima wewe uumwe utoe pesa utibiwe ndipo nao wapate pesa.

Heshimuni kazi za watu acheni kuwakandamiza.
Kumdai hio pesa baada ya kujifungua kulikuwa na tatizo gani?
 
Kwanini wasimfanyie operation then wamdai !? Yaani utaacha mtu afe kisa laki na nusu!??
Washenzi hao, mimi nina ndugu yangu alikufa akiwa mdogo sana on his teens alikuwa na pumu ya kubana mapafu ile unapiga sindano yanaachia.

Kwa kukosa buku 5 ya sindano mtabibu aligoma kumchoma akabanwa pumu hadi kupoteza maisha. Laiti hilo lingetokea nikiwa na utu uzima wangu huu ilikuwa ni kummaliza huyo muhusika yani ni aidha kisu cha shingo afilie mbali na yeye. Wala nisingewaza kwenda jela.
 
Watoa huduma ya afya wapo sahihi.

Hivi kuna sehemu unaweza kwenda ukahudumiwa bure? .

Wahudumu wa afya ili wapate pesa ni lazima wewe uumwe utoe pesa utibiwe ndipo nao wapate pesa.

Heshimuni kazi za watu acheni kuwakandamiza.
Mkuu kuwa na hekima sasa, hapo kuna msiba na wameachwa watoto bila mama, mbona Emotional quotent EQ yako ni ndogo hivyo. Unaleta ligi utafikiri ni mabishano ya simba na Yanga, yaani haufeel chochote kwa binadamu kupoteza maisha kwa 150K, hata kama uko sawa hiyo si jadi yetu
 
Pesa yote hiyo mbona sijawahi ona ikitozwa popote?

Serikali mtendeeeni Haki huyu mtu Kwa kuwawajibisha waliosababisha haya mauaji japo maisha yake hayatarudi tena.

R.I.P
uko sawa,tatizo ni pale kama huna pesa mda huo,wauguzi nao wanafuata taratibu za malipo zilivo maana sie tunaoenda kupata huduma Huwa tunagoma kulipa bills,all in all serikali iweke utaratibu special Kwa wajawazito wanateseka sana.
 
Mkuu kuwa na hekima sasa, hapo kuna msiba na wameachwa watoto bila mama, mbona Emotional quotent EQ yako ni ndogo hivyo. Unaleta ligi utafikiri ni mabishano ya simba na Yanga, yaani haufeel chochote kwa binadamu kupoteza maisha kwa 150K, hata kama uko sawa hiyo si jadi yetu
Ndo nilikua nawaza nimepoteza fahamu hanijui sipati matibabu nikizinduka wanipe bili
 
Madaktar wawe na utu kazi kuokoa maisha
Hawapaswi kuwa na utu, wanapaswa kufuata standard operating procedure ya hospitali, ambayo imepitishwa na government regulator, in this case Wizara ya Afya.

TUJENGE NCHI inayoendeshwa kitaasisi, sio huruma za mtu. Dunia haiendeshwi hivyo.
 
Inasikitisha sana, ubinaadamu unatupungua. Hasa mwanamke mwenye mimba ni mtu wa kujaliwa na kuhudumiwa ipasavyo.
 
Back
Top Bottom