Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

HUa sielewi watu wanaolazimisha mtu utoke nyumbani kila asubuhi na urudi usiku sababu tu huna kazi, yaani kwa mfano unatoka unaenda wapi sasa wakati kazi zote skilled zinaombwa kwa utaratibu wa barua ama barua pepe ama simu.
Watu wanamaanisha abadilishe kijiwe tu. Kipindi flani nilipitiaga hio hali mwenzangu akawa anasisitiza nitoke tu. Kwa kuwa nilikuwa sina pa kwenda nilichokuwa nafanya nachill zangu mpaka muda wa saa 10 kisha nasepa naenda kijiwe kwa wana.

Ubaya wake ni kuwa kama huingizi hata 100 ila alimradi nimetoka tu.
 
Mkuu toka hapo. Tafuta mishe nje ya Mkoa ulipo kimya kimya. Ukibadili mazingira na unakoenda komaa mbaya.

Jitahidi huko ukiwa, fungua account za malengo za watoto weka pesa za kutosha kwa ajili ya watoto ili wasiteleleke kielimu.

Nia yako ikiwa ya dhati Muumba hatokuacha, matendo yako yaongee zaidi kuliko maneno.

Tafuta hela kama kichaaa, weka akiba zako za kueleweka na ikiwezekana anzisha makazi yako kwa ajili ya Watoto.

Be a Man of Steel.
 
HUa sielewi watu wanaolazimisha mtu utoke nyumbani kila asubuhi na urudi usiku sababu tu huna kazi, yaani kwa mfano unatoka unaenda wapi sasa wakati kazi zote skilled zinaombwa kwa utaratibu wa barua ama barua pepe ama simu.

Mwanaume unatakiwa uwe na plan b.. yaani ukisimamishea kazi ndio unashinda ndani kutwa nzima unalala na kuamka kutazama tv?

Kuwa na vijiwe vya kupigia deiwaka hata wekend.. siku ukiachishwa kazi yako unaenda kushinda plan b yako
 
Pole aiseh!
Huyo mwanamke hana mapenzi tena na wewe maana ameshakuona ni mzigo. Jiandae na ratiba za kuchelewa kurudi na kuto kurudi nyumbani kabisa.
 
Exactly mkuu, umenipa neno sahihi "kubadilisha kijiwe"
 
Kati ya vitu ambavyo naogopa kwenye maisha yangu ni kuoa wanawake wa namna hiyo….Daah! ndo maana kwenye ndoa wanaume tunakufa mapema, maana maswaibu ni mengi.

Mkuu ukifanya masihara utapata ugonjwa wa moyo au magonjwa ya B.P kwa kuwaza sana.

Tusikimbilie kuoa kwa uzuri alionao mwanamke au kwa kipato cha mwanamke, bali tabia na hurka. Pole sana mkuu
 
Mwanaume unaweza kuishi na mkeo akiwa hana mishe. Ila mwanamke kuishi na mwanaume hana mchongo ni ngumu. Sema ile kikawaida mwanaume ni nguzo ya familia.

Hata kama unabet lakini kuna mambo lazima uyafanye kama baba hapo nyumbani. Cha msingi ni kupambana hata hiko kidogo unachopata kifike nyumbani. Usawa huu wanaume wengi tu hawana michongo na wake zao ndio wanasimamia shoo.

Ila nasisi wanaume licha ya hizi changamoto tusikae tu, make sure unafanya jambo ili mradi uhudumie familia.
 
Yani mawazo lazima cha msingi ni kukaza tu, mishe mishe zipo mjini. Ila vitimbi vyake visije mfanya akaleta zile za kuuana, hapa itakua sio poa kabisa. Mwishowe atajutia akiwa nyuma ya nondo na mke ndo hivo wana wanakula tu kirahisi.

Jitahidi kutumia huu mwanya kama changamoto ya kukujenga. Pia ningemshauri mdau asali sana na mungu atamsaidia
 
Mwanaume unatakiwa uwe na plan b.. yaani ukisimamishea kazi ndio unashinda ndani kutwa nzima unalala na kuamka kutazama tv?

Kuwa na vijiwe vya kupigia deiwaka hata wekend.. siku ukiachishwa kazi yako unaenda kushinda plan b yako
Hii ni kwa kila fani? Ama inachagua fani?
 

Watu kama hao ishi nao kwaakili.
Kuwa mvumilivu, jifanye hamnazo, kisha muongezee mtoto mwingine,
Mengine siwezi yasema hadharani
 
Hpn nibora asitombwe Bora hzo zarau kuliko kugegedewa huku unajuwa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…