Tangu Rais Dkt. Magufuli afariki, hakuna Habari za vifo vya Corona

Umefanya utafiti/uchunguzi na kuwa na data za kusibitisha hilo. Task Force/Kamati kuhusiana na Corona imeshaundwa kulingana na maeleze ya Rais tusubiri tuone.......
 
Mimi nina vyojua hizo waves zinakuwepo kutokana na matukio fulani fulani. Mfano mabadiliko ya hatua zilizochukuliwa za kupambana na covid kama lockdown. Unakuta serikali imepunguza masharti ya lockdown ndio inasababisha wave au wanafunzi kurudi mashuleni au festival kama xmas.
Sasa hapa kwetu hakuna hatua zozote zilichukuliwa ni nini kilisababisha hizo waves?
 
Acha Mihemko, ww hiyo shahada yako imekusaidia nn mpaka sasa
 
Toka Magufuli hatutoke ni muda sasa! Mjane mpaka sasa hivi anatibiwa bado unadai ni Covid aliyoambukizwa na Magufuli?
 
 

Attachments

  • VID-20210418-WA0055.mp4
    5.9 MB
Wewe mpaka sasa hivi pamoja na kuandikwa sana bado haujapa elimu ya kutosha ya magonjwa kama Covid. Haya magonjwa hakuna button ya “pause” ya kukusubiri!! Hili gonjwa wakati wa Magufuli lilitumiwa kisiasa labda ni kutokana na matamko yake kuhusu Covid. Mama amecheza nyimbo mnayotaka kuisikia lakini mpaka sasa hivi mambo ni yale yale!
 
Hapana. Waves zinatokea hata kama hatua hazijachukuliwa. Magojwa ya jamii hii hayajaanza kutokea sasa. Soma historia kuhusu magonjwa ya aina hii yaliyoua watu wengi miaka ya nyuma kama Spanish Flu kipindi hata hawajajua ni kwa nini watu wanakufa na hakuna hatua zozote zinachukuliwa uone hali ilivyokuwa. Kulikuwa na ''waves''.
 
Mkuu ni kitu gani kimesababisha kuwe na curves! Mafano Europe ni kutokana na hatua zilichukuliwa na serikali ndio imesabisha hizo curves! Hapa baada ya Magufuli kufa na gafla Corona nayo imeyoweka kwenye media!!
 
Acha Mihemko, ww hiyo shahada yako imekusaidia nn mpaka sasa
Shahada ya jiwe ilimsaidia nini ?

Kusema virusi vinatibiwa kwa kula malimao !??

Kukataa chanjo ya dhidi ya kirusi kwa madai ni agenda za mabeberu huku akipokea chanjo lukuki za watoto na ARV ! Huoni huo ni upofu wa fikra?
 
Je kwenye maombolezo walitembea na bakuli za kunawia?
 
Wapuuzi wachache ndio walikuwa wanaleta taharuki kuhusu Corona, JPM mzee wa misimamo aliwapotezea mazima.

Aliwapotezea mazima mpaka akajipotezea na yeye moja kwa moja.

Hiiiiii bagosha!
 
Kama ungeelewa hoja wala usingekurupuka kama unaoga nje!!

kuna hoja gani wakati walevi mmevamia uzi hapa!!!!

mleta mada anahoji,viko wapi vifo vya corona baada ya magufuli kututoka!!!mbona kama vile tatizo linaonekana haikuwa corona ila magufuli ndiye alikuwa tatizo???maana kelele zingeendelea.

nyumbu mnasema mama atachukua hatua si kama mwenda zake,kwamba corona inasubiri achukue hatua ndipo iamue inaendelea au maana yake nini!!!!
 
Mkuu kumbuka hizo waves za Spanish flu zilikuwepo 1918 -1920 kipindi cha kukaribia miaka mitatu. Hata Corona miaka hijayo inaweza kurudi tena na kuwa “wave”. Na wataalamu watatupa sababu za kuwa na wave nyingine. Mafano Spanish flu 2nd wave inasemekana ilitokana na movement za wanajeshi!

Covid imekuwa ni mwaka mmoja na ushee sasa. Hizi waves tunazozisoma uko Europe zimesababishwa na matukio fulani fulani hasa zimehusishwa na lockdowns.
Ninachopinga hapa ni Magufuli kafa gafla na Covid nayo imekuwa sio gumzo(kimya)! Mnasema ni waves!
 
Ule mwezi wa pili huenda ulimpa Magufuli stress sana maana alishuhudia watu wakikataa style yake ya uongozi wa nchi waziwazi. Wakatoliki walimgomea waziwazi, nahisi pale ndipo alipojua kuwa uraisi wake una mipaka
yaani hilo ndilo jibu
aliona kila dalili kuwa tamati imefikia, makusanyo yalishagota kabisa mpaka akaingia kodi za wenye kuwapangisha wapangaji mitaani nao walipe, miradi lukuki ikasimama km SGR, Nyerere Dam, Kigongo Busisi akajionelea ngoja akafungue Daraja la Kijazi na stand ya Magufuli, hapo hasira na matamshi vikaanza pishana ziara nzima ya DSM
 
Lilitumikaje? Mie wazazi wangu waliugua na waliponea ICU!! So tukubaliane corona ipo

Hoja hapa ni kwanini media haitangazi tena... Jibu ni kwamba walikuwa wanatangaza ili kumpa presha alichukulie hatua

Ila kuhusu corona kuwepo na kuua hilo halina ubishi unless ulikua hutembelei muhimbili February
 
Covid kwetu ni ugonjwa wa msimu (kwaimani yangu) so kuna wave ya wiki 2 hadi 3 kwa maambukizi ya mwezi 1 hadi mwezi 1½ ikipita hiyo basi hapo kuna kuwa na vifo vingi baada hapo pana poa na wataoondoka ni wenye udhaifu mkubwa kiafya.
Now the shift is below 40 yrs of age, be careful....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…