Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,042
- 17,320
Bunge DHAIFU la CCM limepitisha azimio la kubinafsisha bandari ya DSM kwa kampuni ya DP World ya Dubai kwa miaka 100 hadi 2123.
#MyTake:
1. Maamuzi haya yamelenga kunufaisha watu wachache na kufuta urithi kwa vizazi vijavyo. Mwaka 2123 hakuna yeyote kati yetu atakayekua hai. Maana yake tumeamua kuwaachia msalaba wajukuu zetu ambao hata hawajazaliwa.
Unadhani Nyerere alishindwa kubinafsisha madini, bandari, mbuga za wanyama? Angeweza but alifikiria vizazi vya baadae. Ila sisi tumeamua kuuza urithi wa vizazi vyetu kwa tamaa ya muda mfupi. Tukikubali huu ujinga wajukuu zetu watapiga viboko makaburi yetu.
2. Kagame aliwahi kutukejeli tumpe bandari ya DSM atupe nusu ya bajeti ya nchi kila mwaka. Tukaona ametudharau. Lakini leo tunajiuza "cheap" kwa waarabu. Hakuna cha nusu wala robo ya bajeti. Kama tumeshindwa kuendesha bandari si bora tungempa Kagame, maana heri mwendawazimu uliyemzoea kuliko kichaa mpya.
3. Kampuni ya DPWorld inatuhumiwa "kupora" bandari nchi mbalimbali kwa kigezo cha uwekezaji. Bandari ya Sarubaya (Indonesia), Batangas (Ufilipino), Palao (Peru), Dakar (Senegal), bandari ya Djibout etc. Huko kote vimebaki vilio. Badala ya kujifunza, tumejipeleka kichwakichwa tukale za uso.
4. Katika kuonesha jinsi bunge lilivyo DHAIFU, limetoa siku 1 tu wananchi kutoa maoni yao. Yani jambo litakaloathiri maisha yetu na vizazi vyetu kwa miaka 100 ijayo litolewe maoni siku 1? Hawa watu wana kichaa? Halafu maoni yatolewe ukumbi wa Msekwa, uliopo bungeni. Ebo.!
Bandari inagusa maisha ya kila mtu, kuanzia mkulima wa Runzewe hadi Mwalimu wa Ludewa. Magari, mafuta, vyakula, nguo, pembejeo vinapita bandarini. Kugusa bandari ni kugusa maisha ya kila mtu. Ingeundwa kamati kukusanya maoni nchi nzima, sio kusema watu wakatoe maoni ukumbi wa Msekwa. Mwananchi wa Namtumbo anafikaje Msekwa?
5. Wananchi kataeni upuuzi huu. Mkinyamaza kwa kuona ni jambo la kisiasa msije kulia baadae. Maana mna "kaupuuzi" ka kunyamaza mkidhani waathirika ni wanasiasa tu. Utadhani bei ya petrol inapanda(ga) kwa wanasiasa tu. Siku yakiwachachia ndo mnaomba kupaziwa sauti. Ukikaa kimya usiombe kupaziwa sauti.