Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na Kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza bandari ya Dar es Salaam
Yaani Dubai waje kuendeleza bandari Tanzania??

Huu ni ulemavu wa aina Gani lakini??

Hawa wasomi wanaomaliza vyuo kila siku wanafanya nini na elimu zao??

Mbona huko ulaya hawatuiti tukaendeleze za kwao??
Wakuite una nini cha kuwa wakati kujisimamia tu wenyewe hatuwezi mpka mgongo wao
 
HUU MKATABA UNAANZA LINI JAMAANIII!! KAMA NI 2024 YAANI +100YRS, JE WEWE NA MIMI NI KIZAZI CHA NGAPI TOKA KWAKO AU KWANGU KITAPOKEA KIJITI TOKA KWA HAWA MAJIZI!!!
Tuna tawaliwa na wasiyo watanzania

Nimawazo yangu tu👣👣
 
CHADEMA ACHENI UPOTOSHAJI, HUU NDIO UKWELI JUU YA MKATABA WA DP WORLD NA TANZANIA.

✅UFIPA kama kawaida yao, wazee wa kuongea urongo kwa maslahi yao ya kisiasa, kujaza watu hofu na taharuki pasi na msingi, tumewashawazoea na hakuna cha ajabu wanachoweza kufanya tena. Hii ni ishara tosha kwamba hawana hoja walichobakisha ni vioja tu, wapuuzwe.

✅Mkataba huu kati ya DP World na TPA kwa niaba ya Serikali ya JMT chini ya Rais Samia Suluhu una faida gani kwetu, kwanini mkataba huu ni muhimu sana wakati huu kuliko wakati wowote ule?

✅Kwanza, achana kabisa na propaganda za UFIPA juu ya kwamba tumetoa bandari yetu 100% iendeshwe na DP World, huu ni uwongo na wala huitaji degree wala elimu ya darasa la 7 kujua kuwa huu ni uwongo.

✅Hadi muda huu tunachojua ni kwamba, makubaliano ya awali yamesainiwa Dubai wakati Rais Samia Suluhu alipokwenda kwenye maonesho ya Dubai Expo 2020, na kama makubaliano ya mwisho yatasainiwa, basi mkataba huu utakuwa na thamani ya USD 500 milioni.

Nini Mtanzania unapaswa kujua kuhusu mkataba huu?

Kwanza, unatakiwa kujua kwamba DP World itapewa
kushughulikia gati ya 5 hadi 7.

DP World mbinu yake ni kuondoa vizuizi vya biashara na kuunda mfumo ikolojia wa biashara ili kupanua mtiririko wa biashara ya kikanda na kimataifa.

▶️Kama mkataba huu utasainiwa, ndani ya miaka 10 ijayo, ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam utaongezeka kwa asilimia 233.7%

▶️Mapato ya Bandari ya Dar es Salaam kuongezeka kutoka Trilioni 7.79 kwa mwaka hadi Trilioni 26, ndani ya miaka 10 ijayo.

▶️Ufanisi wa Bandari utaongezeka, mizogo itatoa haraka, ajira zitazalishwa kwa wingi na pia pato la taifa kuimarika maradufu.

▶️Mapato yakiongezeka kwenye kupitia Bandari ya Dar, serikali itapunguza mzigo wa kodi kwa Watanzania hivyo kuboresha hali ya maisha ya watu.

▶️DP World hawatowekeza bandari ya Dat tu, bali na bandari nyingine nchini na pia, wataalamu wetu watakwenda kupewa mafunzo na kuongezewa ubunifu kwenye utendaji wao.

🚨Angalizo, Kuna uzushi na uwongo mwingi sana unaendelea kutoka kwa watu ambao kimsingi hawana nia njema ya taifa letu na maendeleo yetu. Kikubwa, watanzania tusome tuache kupotoshwa.
6:52 PM · Jun 6, 2023
from Dar es Salaam, Tanzania·
Ndio nini hikinsasa
 
Ficha ujinga wako.Serikali mnayo wenyewe mambo yamewashinda wenyewe alafu unasingizia wengine.Uwezo wenu wakusimamia mambo ulishaisha.
 
Annexture zipo wapi tufanye proof reading za hiyo Dubai contract
 
Eti mkataba wa miaka 100
Nawaambia waarabu wataondoka kabla ya miaka 5 tu maana yataingia mabehewa 20 wataambulia 2

Labda walete wahindi wasimamie

Msijali hakuna mtu kanjanja kama ndugu zetu, watapiga mpaka camera
Mwisho atafunga virago kama Nakuman
 
Kila kitu kikiwekwa wazi hamna atakaelalamika,mikataba iwe wazi
 
Aiseee nacheka kama mazuri vile aiseee! Yani watu wanafikiri bila kubadili sheria zetu za biashara hata hao wanaokuja watafanikiwa?

Kwanini tulichukua mkopo kuboresha bandari wakati tunajua tutakuja kuwakodisha watu? Wao watafanya kazi gani ambayo serikali imeshindwa?

Tatizo kubwa la bandari ya dar linaanzia kwenye kanuni na biashara na makodi makubwa ya utoaji mizigo bandarini! Hakutakuwa na mabadiliko kama kodi zitaendelea kuwa zile zile…
 
Kupitia Maria Space tunaambiwa tumekodisha bandari zori, economic zones pamoja na Ardhi na katika kipindi chote cha mkataba hakuna chombo chochote kinaweza kuingia eneo la bandari Bila idhini ya Mwarabu.
 
Mwezi huu bunge linatarajia kujadili na kupitisha Mkataba wa Kiserikali (IGA) kati ya Tanzania na Dubai kuhusu kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam. Hili litaweka mazingira ya kufanyika kwa taratibu nyingine, ikiwamo mkataba wa makubaliano, kabla ya kuanza kwa sura mpya ya ushirikiano kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na DP World, kampuni ya kimataifa ya usafirishaji yenye makao yake makuu Dubai, Falme za Kiarabu.

Kampuni hiyo, ambayo mikakati yake ni kuondoa vizuizi vya biashara na kuunda mfumo ikolojia wa biashara ili kupanua mtiririko wa biashara ya ndani ya kikanda na kimataifa, itapewa gati namba tano hadi saba kushughulikia, kulingana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa.

Katika mahojiano na The Citizen, Prof. Mbarawa amesema kwa kufanya kazi na DP World, Serikali inatarajia kuongeza ukusanyaji wa mapato kupitia bandari hiyo kwa asilimia 233.7 katika miaka kumi ijayo.

Prof. Mbarawa alisema lengo ni kuongeza kiasi chamapato yanayokusanywa kutoka bandarini kutoka TZS trilioni 7.79 kwa mwaka hadi TZS trilioni 26 katika muongo ujao.

"Uwekezaji wa sekta binafsi unaweza kuongeza ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kuboresha ubora wa huduma na kuongeza ufanisi," amesema.

Kuhusu kwa nini serikali ilichagua DP World, Prof Mbarawa amesema kampuni hiyo ina nafasi ya kipekee ya kushirikiana na Serikali kwa kuwa ni kampuni ya kimataifa ya usafirishaji ambayo ina uwezo wa kuleta mabadiliko yanayohitajika nchini kote katika mnyororo mzima wa thamani wa vifaa.

Amesema kampuni ina rekodi iliyothibitishwa ya kusimamia, kuendesha na kuwekeza katika miundombinu ya biashara barani Afrika kwa zaidi ya miaka 20 kwa viwango vya juu zaidi vya kimataifa.

"Tukiwa na DP World, tunatarajia kuona uboreshaji katika utendaji wa bandari. Tunatarajia kuona muda wa uondoaji wa meli ukipunguzwa hadi siku moja kutoka nne hadi tano za sasa.

Prof. Mbarawa ameeleza kuwa inaweza kumaanisha kuondolewa kwa vikwazo vya biashara, ambayo ni muhimu kwa kuendesha na kuongeza mtiririko wa biashara.

Athari zinazowezekana za uwekezaji wa sekta binafsi zinasisitiza umuhimu wa kimkakati wa bandari kwa uchumi wa Tanzania na uwezo wake wa kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo nchini.

Utangulizi wa teknolojia za kisasa, vifaa vya hali ya juu na wafanyakazi wenye ujuzi, vinaweza kuwezesha bandari kushughulikia mizigo zaidi, kupunguza msongamano, na kuharakisha nyakati za ugeuzaji wa meli, na hivyo kupunguza gharama kwa wateja wa mwisho.

Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA), Daniel Malongo amesema ana imani na DP World, na kuongeza kuwa ni miongoni mwa kampuni nne zinazoongoza duniani katika uendeshaji wa bandari na kupongeza jinsi kampuni hiyo ilivyotengeneza mitambo yake ya kuhudumia pamoja na mifumo ya uendeshaji na ukusanyaji wa mapato.

"Uwazi ni wa hali ya juu kwa kuwa kila harakati kuanzia wakati kontena inatoka kwenye meli hadi bandarini na ICD (Depo ya Kontena ya Ndani), inaonekana kwenye mfumo. Hii itakuwa muhimu sana kwa nchi yetu kwani haitoi mwanya wa uvujaji wa mapato." amesema Malongo.

Rais wa Chama cha Mawakala wa Mizigo Tanzania (TAFFA), Edward Urio amesema DP World itaongeza thamani katika utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam pia kampuni hiyo italeta ubunifu, ufanisi na ushindani kwa waendeshaji wengine wanaoshughulikia gati namba nane hadi 11.

Kwa mujibu wa takwimu za TPA, bandari ilihudumia tani milioni 17 za shehena mwaka 2021, kutoka tani milioni 14 zilizorekodiwa mwaka 2017, kutokana na kupanuka kwa

uwezo, harakati za masoko, kuondokana na Covid-19 na mazingira wezeshi ya biashara. Inaaminika kuwa ushiriki wa sekta ya kibinafsi huleta matarajio ya kuboreshwa kwa muunganisho nauwezekano wa upanuzi na uboreshaji wa vifaa kwenye bandari.

Wadau wanaamini kuwa ushirikishwaji wa sekta ya kibinafsi utatoa njia ya kutengeneza vituo vipya, kukarabati vilivyopo, na kutoa huduma za ziada kama vile maghala, vifaa na ukarabati wa meli.

Hii inaweza kuunda nafasi mpya za kazi, kuongeza mapato, na kuvutia biashara zaidi kwenye bandari. Zaidi ya hayo, uwekezaji huu unaowezekana unaweza kuchochea mseto wa kiuchumi kwa kuvutia sekta na biashara mpya kwenye bandari.

Uwekezaji wa DP World nchini Tanzania utafanya miundombinu ya bandari kuwa ya kisasa kwa kuwekeza katika vifaa, michakato na mifumo katika bandari ya Dar es Salaam ili kuleta utendaji katika viwango vya ubora wa kimataifa vya tija, kampuni hiyo imesema katika taarifa yake ya hivi karibuni.

Taarifa hiyo imesema kampuni hiyo itaboresha urahisi wa kufanya biashara kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuchagiza mwonekano, uwazi, na kuongeza kasi ya usafirishaji wa mizigo katika bandari za Tanzania, Bohari za Kontena za Ndani na mipakani.

Chanzo: Swahilitime.

Pia soma: Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam
 
Mimi sielewi huku tumechukua mikopo kujenga, kupanua na kuboresha bandari ya Dar kabla mikopo hatujalipa hata robo tunaamua kuwaleta waarabu wawekeze mbona tunajichanganya sana? Mimi naona tutalia kilio cha mbwa mdomo juu!!! Msishangae hii SGR Dar Morogoro nayo haijaanza kazi inasubiri kampuni ya nje kuiendesha au kukodisha au kununua sijui
Ikiwezekana wampe muwekezaji
Sisi ni wapumbavu waliopitiliza
Hebu kapande mwendokasi ili ujue ujinga wetu
Scanner za tickets wameng'oa ili waibe vizuri
Mabasi yanaharibika hakuna services
Mnajazana kwenye kituo kwa kupanaga mstari Kama wanafunzi wanahesabu namba ,hapo hapo gari hazitoshi
Mi nadhani hatuwezi kuendesha shirika lolote kiufanisi ,maana kila mtu anawaza wizi
Kama kubinafsisha kutaleta tija basi iwe hivyo ,muhimu nafuu ya maisha ipatikane
 
Naona Kuna habari zinasambaa kuwa bandari Kuna watu wamepewa kwa 100yrs dah hv hawa waliokubali Wana akili kweli Yan mtoto azaliwe leo mpaka anapata vitukuu mkataba bado haijaisha tuu.
Screenshot_20230606-221855.png

Hivi wamesain kwasababu yanani wamesahau wao n wachache dhid ya sisi wengi hata hyo nafasi tuliowapa sio kwamba sir hatuwez bali tulikubali nyie mtuongozee je mmeshindwa?

Naskia kuna maoni ya kutoa kuhusu huu mchakato tena wanasema tuyapeleke haraka sana mana muda walio nao n mchache sana sasa hii haraka n Yann kwann tusiende polepole ili tuelewane vizuri.
Screenshot_20230606-223044.png

Kule wanasema MoU imeshatiwa sain na kiongoz wa Taifa tena ilkua n mwez February tena naskia ndio ile siku benders na picha ya Rais wa TANZANIA ilionekana kwenye majengo maarufu marefu pale Dubai.
Screenshot_20230606-222042.png


Jamani sisi wengine tunaona uchungu taifa letu linavyorubuniwa na kufanya sisi wengi tubebe mzigo wa maden na tozo nyingi huku wachache wakila pesa za rushwa nakuwa na kiburi nakusahau wao n wachache Kati ya wengi ambao tunaumia?
 
Pana kitu sielewe hapo wansema iga makubaliano kati ya serikali ila then waona bwana dp anaibuka hii dp ni serikali au kamouni binafsi iliyo based huko dubai?!

Na konekti dot za zile trip kadha wa kadha za dubai...

Anyway kweli umma umeshinda fanya biashara je tunabinafsisha kwa serikali nyingine au kampuni za njeee?!!! Why not ten au twenty years na review kila baada ya muda kidogo. ROI haipatikani ndani ya muda mfupi hadi 100 yrs.
 
Back
Top Bottom