sikumaanisha wewe in person lakini humu kwenye jf ndiyo wanakuja walalamikaji.
Sio walalamikaji bali ni wazalendo ambao wanaitakia mema nchi yao! Nchi yetu lini itaacha kuwa tegemezi ? Tumekuwa na TICS hapo bandarini kwa zaidi ya miaka kumi tumejifunza nini?
Kitu gani kinatushinda kuendesha bandari iwapo kila mwaka tunao vijana toka vyuo vikuu hawana ajira? How costly will it be to train them to be able to efficiently run our ports? Hata kama hatuna hao watu we can hire professionals but run the ports ourselves!
Hapa hakuna uzalendo bali harufu ya ufisadi wa kutafuta hela za uchaguzi. Tukumbuke tu kuwa remote iko Msoga!
 
Yaani Dubai waje kuendeleza bandari Tanzania??

Huu ni ulemavu wa aina Gani lakini??

Hawa wasomi wanaomaliza vyuo kila siku wanafanya nini na elimu zao??

Mbona huko ulaya hawatuiti tukaendeleze za kwao??
Akili za kibongo zinawaza wizi wizi tu.
 
Uwe na kawaida ya kupitia ukasoma kilichoandikwa ndipo utoe maoni yako, pia uwe una re-read ulichoandika usikurupuke, hiyo ni ishara ya uvivu
 
Potential ya Bagamoyo huwezi kulinganisha na Zanzibar. Tatizo ni bado hatujaweza ku utilise kabisa potential ya Dar port kabla ya kurukaruka.
 

Watabadilisha vipi mfumo wakati cranes ni time based processes. Ukiwa nalo la kisasa unajua its maximum capacity. Kilichobaki ni wewe tu sasa kujiwekea ‘balanced score card’ na kuhakikisha unafikia malengo. Uhitaji mwekezaji kukusaidia kufanya hilo.

Naelewa watanzania tuna culture ya kutojali, wizi na kauzembe fulani; ata tukipewa kila kitendea kazi. Personal sipingi kabisa wazo la ku-outsource sehemu ya bandari. Issue ni kwamba mwekezaji anapewa financial incentives zipi na je? Ni fair value for money. Kuna score card ya performance zake; au anakuja kuvuna tu kisa jina lake lina mbeba.

Ni lazima ujue ya thamani unachogawa na kupokea; vingine huna sababu kama wewe ndio unapoteza zaidi.
 
Mimi nafikir kama kila taasisi inakiboronga tunabinafsisha , baasi tuaanza na ikulu yetu kwa kuwa imeshindwa kabisa kuongoza nchi
 
Wakumtegemea mwenyew ndio kwaanza hata haelewi kitu hapo, keshawaagiza waende kulitizama!
Huyu mama sijui kama hata huwa analiumiza kichwa chake kwakweli , unaweza kumchomekea hata barua ya posa kwa mara ya pili na akasaini
 
Ubia haijawahi kuwa tatizo kama tunauwezo wa kufanya financial and operational analysis ya maana na kuachia maeneo tunayohitaji ku import management and technological skills.

Kiutendaji sisi Watanzania ni kama tumeshindikana, tunahujumu miundombinu ili kupata fursa za wizi, ufanisi mdogo n.k tunaweza kuingia ubia ili kutengeneza kizazi cha ku take over kwa ufanisi mkubwa kuliko sasa.
 
Mama anaupiga mwingi
 
Mimi nafikir kama kila taasisi inakiboronga tunabinafsisha , baasi tuaanza na ikulu yetu kwa kuwa imeshindwa kabisa kuongoza nchi
Sometimes hizi sector za serikali kuna umuhimu wa kupima efficiency. Either kwa kuangalia wengine wanafanya nini duniani kwa vifaa hivyo hivyo, kuleta consulting firms kushauri namna bora ya kuboresha system au ata ku-outsource sehemu ya huduma na kulinganisha utendaji kazi. Those are normal practice measures.

Shida ya Tanzania ipo wizarani na mamlaka ya teuzi. Hakuna targets wanazopewa hawa wakurugenzi wa hizi taasisi ata wakipatiwa kila kifaa cha kisasa, kuna kutokujali sidhani kama kuna known process ya TRA hapo bandarini ata ukimuuliza commissioner wa TRA mbinu inayotumika hapo (technically) kufanya hiyo process iwe fast baada ya kupokea mizigo anaweza asiwe na majibu; same waziri wa uchukuzi, wa fedha na mkurugenzi wa bandari.

So kuna management issues kuanzia juu serikalini mpaka kwenye work floor, mengine bandari inaweza ziondoa, zingine bila ya serikali kubadilika ata aje malaika kuendesha bandari those problems will remain.

Ndio maana ni vizuri kueleweshwa how exactly huyo mwekezaji ata boresha processes hapo bandarini na kwanini TPA wenyewe wameshindwa to justify huo uwekezaji. Je kuna ‘balance score card’ ya kupima matokeo ya kazi zake na nini tunampa huyo mwekezaji and for how long.
 
Kwani TICTS wewe uliwahi kuifahamu? Au JPM hakukusimulia? Issue za Mchina na mwarabu kama uandikavyo ni upungufu tu wa maarifa kichwani mwako Mkapa Alikusudia kubinafsisha TRC kwa wahindi
 
Bandari kavu lengo lake ni kuondoa msongamano wa makasha, magari bandarini.
Lengo ni zuri kwa nini TPA wasijitanue kwa kuwekeza kwenye maeneo ya bandari kavu sababu uwezo huo wanao kuwapa Private sector ni kuongeza wigo mpana wa upigaji na biashara za magendo kwa maslahi ya wachache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…