Tanzania Kinara wa Kupokea hela za msaada kutoka USAID Afrika nzima. Yasemekana tutaathirika sana

Wewe uko hapa Tanzania Huwa zinatumika vizuri na hao NGOs?

Magufuli alitaka kuwafuta

Mwigulu alitaka wapitishie hela Serikali for monitoring ila wakapiga makelele ikaishia.

Trump futa huo ujinga,wanakula tuu hizo hela hakuna wanachofanya
Waache wale.Kwani unataka wakugawie?As long as fedha zinatumika na kuingia kwenye mzunguko imekaa poa.
 
Inaonekana una hasira, huna taarifa za kutosha au wivu na NGOs, lakini kwa ujumla ufanisi wa kazi kwenye NGOs uko juu sana kuliko sehemu zingine. Wanatumia pesa kidogo lakini matokeo yake ni makubwa, na uwajibikaji ni wa hali ya juu ndiyo maana wafadhili wanaendelea kufanya nao kazi.
 
Kwa uchumi gani wa kuona trillioni moja ni hela ndogo??....

Huu huu unaoendeshwa kwa mikopo
 
Sawa.Sasa mzitumie kikamilifu.
Ndio maana nasema hiki kinachitwa misaada kinatupumbaza.
Kibaya zaidi kwa asilimia kubwa hii misaada haitumiki kwa nia njema kwetu ndio maana asilimia kubwa wanataka wao waleta misaada waicontral. Wanaajiri wazawa humuhumu wanawalipa pesa nyingi kwaajili ya kupata taarifa nyeti na wengine wanalipwa ili wasambaze tamaduni za nje huku wakitoa vitisho kwamba tukiwachukulia hatua tunakuwa tumekiuka haki za binadamu.
Mifano ni mingi
 
Ungetoa hiyo mifano ili tusiojua tujue.
 
Tutaathirika sisi au vitaathirika vi- NGO vya vigogo Serikalini ? Hizo pesa sidhani hata kama zinawafikia walengwa.

Niliwahi kuiona return report ya TACAIDS miaka ya nyuma ... Sikuamini hadi leo kwamba, nchi hii kwa wizi wa kitaasisi na ujanja ujanja imeshindikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…