Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Kama sheria inasema hivyo wavichome tu ili liwefundisho kwa hao wanaingiza vifaranga bila kibali.
Mnataka kumpoteza Mama kama mlivyofanya kwa mwendazake. Mnaanza kumpa sifa za kijinga
 
Vifaranga vinasambaza magonjwa kwa haraka sana mkuu. Ungekuwa umefanya biashara ya kufuga kuku ungejua ukweli huo. Nafikiri unajua ugonjwa wa mafua ya ndege.
Sasa kama vimeshasafirishwa toka kenya hadi uvikamatie Dar, kama vina magonjwa, utayakwepaje?? Sio busara kuvichoma moto, muhusika apigwe faini, na kusimamiwa kuvirudisha vilikotoka!! Au vipigwe chanjo zinazotakiwa wajue cha kufanya, tatizo liko kwenye maamuzi mabovu yaliyofanywa huwezi kuzuia kuingizwa kwa vifaranga nchini wakati uzalishaji wake nchini hautoshelezi, waulize wafugaji wanavyopata tabu sasa kupata hivyo vifaranga!! Na masharti kibao kuwa ni lazima ununue chakula toka kwa muuzaji huyo, huwezi kulinda wazalishaji wa ndani wakati hawana uwezo wa kutosheleza mahitaji!!?
 
Vifaranga hawana hatia, aadhibiwe mhusika, vifaranga wapimwe kujiridhisha kama wanafaa kuwepo nchini au warejeshwe walikotoka, kuna amri ya Mungu isemayo "usiue"
Usiue ili baadae uchinje ule ushibe.
 
Walioweka sheria walifanya research ya kutosha kufikia conclusion hiyo!
Unaweza kuwaza zaidi ya hapo mzee jikaze.. Umepewa akili kutumia sio ushikiwe na watu

Tuletee hiyo Research hapa tuichambue..
 
Sheria ifate mkondo wake, hii mambo ya double standards katika kutoa adhabu haitakiwi.
Hata yeye alipokuwa anafanya hilo alijua kuwa anaweza kukamatwa mchezo ukaisha. Ila still alibeti na mkeka ushalost! Sheria zinavunjwa na watu wanaozijua kabisa ila tamaa ndio huponza watu. Afanyiwe anachostahili.

Haina tofauti sana na tunaobeti kwenye michezo kama mpira, basket n.k tunaelewa kama kuna kula na kuliwa so tunakuwaga Neutral.
 
Hichi kitendo cha kuchoma kimekaa kiukatili zaidi
 
Hakuna diplomasia ya biashara? Kama mtasikia tena kupiga kelele mahindi ya wakulima yakipigwa pini mpakani kuingia Kenya.
 
Kama vizima wavipige mnada kwa wafugaji. Tena wafanye fasta visije wafia. Huu ukatili wa kuchoma viumbe wanatoa wapi?
 
Vifaranga vinasambaza magonjwa kwa haraka sana mkuu. Ungekuwa umefanya biashara ya kufuga kuku ungejua ukweli huo. Nafikiri unajua ugonjwa wa mafua ya ndege.
Kha....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…