Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Sasa kama vimeshasafirishwa toka kenya hadi uvikamatie dar, kama vina magonjwa , utayakwepaje??sio busara kuvichoma moto, muhusika apigwe faini, na kusimamiwa kuvirudisha vilikotoka!!au vipigwe chanjo zinazotakiwa wajue cha kufanya.tatizo liko kwenye maamuzi mabovu yaliyofanywa huwezi kuzuia kuingizwa kwa vifaranga nchini wakati uzalishaji wake nchini hautoshelezi, waulize wafugaji wanavyopata tabu sasa kupata hivyo vifaranga!!na masharti kibao kuwa ni lazima ununue chakula toka kwa muuzaji huyo, .huwezi kulinda wazarishaji wa ndani wakati hawana uwezo wa kutosheleza mahitaji!!?
Kwani umekamatiwa Dar?
 
Kwa kweli haya si maamuzi sahihi na hiyo sheria imekaa kikatili ni bora ikaangaliwa upya,ni vyema tukaangalia ubinadamu na pia haileti picha nzuri kwa hawa jirani zetu. Ni dhahiri hawatajisikia vizuri na mambo kama haya yanazidisha choko choko kama majuzi nao walivyokataa kununua mahindi yetu.
 
Mimi hata viumbe vingine naogopa kutoa uhai wao kwa kuwagonga kwa gari. nilishagonga paka nikasali kwa kumuomba Mungu anisamehe
Wengine hatuli hata nyama kwakuwa tunavaa uhusika, fikiria ng'ombe, mbuzi, kuku, kondoo wanavyohangaika mioyo wakiona wenzao wanachinjwa, au hata binadamu akichinjwa na gari
 
Unaweza kuwaza zaidi ya hapo mzee jikaze.. Umepewa akili kutumia sio ushikiwe na watu

Tuletee hiyo Research hapa tuichambue..
Nenda kasome kwenye ans za Bunge kila kitu huwa zinawekwa kabla sheria haijapitishwa!
 
Kwa kweli haya si maamuzi sahihi na hiyo sheria imekaa kikatili ni bora ikaangaliwa upya,ni vyema tukaangalia ubinadamu na pia haileti picha nzuri kwa hawa jirani zetu. Ni dhahiri hawatajisikia vizuri na mambo kama haya yanazidisha choko choko kama majuzi nao walivyokataa kununua mahindi yetu.
Sheria ifuate mkondo wake fullstop.
 
Haya ndiyo maeneo ambayo jiwe alikuwa anajipatia umarufuu, yaani ndani ya wiki2 tangu jiwe afariki wafanyabiashara tayari mmeanza janja janja ya kukwepa kodi, hapana huyu ashughulikiwe vilivyo tena ikiwezekana anyongwe kabisa, ndiyooo huu ni zaidi ya uhujumu uchumi!
 
Haya ndiyo maeneo ambayo jiwe alikuwa anajipatia umarufuu, yaani ndani ya wiki2 tangu jiwe afariki wafanyabiashara tayari mmeanza janja janja ya kukwepa kodi, hapana huyu ashugurikiwe vilivyo tena ikiwezekana anyongwe kabisa, ndiyooo huu ni zaidi ya uhujumu uchumi!
Kwa akili yako enzi za mwendazake, ukwepaji kodi ulikuwa hakuna? Hayo madudu ya bandari alikuwa hayupo?! Ni suala la muda tu huyu mama akiamua kweli afunue kote mlikokuwa mmefunikwa mtamuona huyo meko kumbe alikuwa hata zaidi ya JK!! Hizo ndege kila siku alikuwa anawaambia ni ma faida tu??
 
Mimi nawaambia hii ni laana endelea kuua viumbe wasio na hatia mtaambulia kaburi kwani vifaranga wana hatia gani? Magari mbona hamyachomi moto?
Mungu waunguze awa wauaji.
 
Vifaranga vinasambaza magonjwa kwa haraka sana mkuu. Ungekuwa umefanya biashara ya kufuga kuku ungejua ukweli huo. Nafikiri unajua ugonjwa wa mafua ya ndege.
Mbona ng'ombe hawakuchoma moto? Wale ng'ombe hawawezi kuwa na magonjwa?
 
Kulikoni kuvichoma vifaranga tumchome huyo mhujumu uchumi kwanza, tukimwacha ata endelea na hako kamchezo na kuisumbua nchi, na hivi ndivyo china inavyo fanyia wahujumu uchumi
 
Vifaranga kutoka nchini Kenya vyenye thamani ya Milioni 40 vimekamatwa na mamlaka ya serekali Tanzania bila ya kua na vibali halali.
Kwa kujibu wa taarifa toka mamlaka husika Tanzania wamesema wataviteketezwa kwa mujibu wa sheria inavyotaka. Japo vifaranga hivyo havijathibitika kua na magonjwa ila kwa kua vimeingia bila kibali vitachomwa moto.

Source ;ITV
Nasikia mahindi yamekataliwa kuvuka kwenda Kenya😪
 
Back
Top Bottom