Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Kuna sheria zinazo ongoza uingizaji wa bidhaa au viumbe nchi fulani...sheria yetu iko wazi kuhusu kuingiza ndege au viumbe vingine lazima vipime na uwe na kibali! Na hii sheria sio Tanzania tuu ni karibu nchi zote duniani hii imewekwa hili kudhibiti kusambaa au kusambaza magonjwa au ugonjwa wa mafua ya ndege na magonjwa ya mifugo!

Hivyo kabla ya kulalamika muwe mnajipa muda wa kutafakari!
Hii watu humu wanajua basi? Wabongo kusoma ni wavivu wanajua siasa pekee
 
Sheria ifate mkondo wake,.hii mambo ya double standards katika kutoa adhabu haitakiwi.
Hata yeye alipokuwa anafanya hilo alijua kuwa anaweza kukamatwa mchezo ukaisha. Ila still alibeti na mkeka ushalost! Sheria zinavunjwa na watu wanaozijua kabisa ila tamaa ndio huponza watu. Afanyiwe anachostahili.

Haina tofauti sana na tunaobeti kwenye michezo kama mpira, basket n.k tunaelewa kwama kuna kula na kuliwa so tunakuwaga Neutral.

Sawa kama kwenye mikeka si unasema kuna kula na kuliwa; sawa nae huyu bwana vifaraga took a chance lakini kakamatwa ,hivyo apewe adhabu ya faini lakini kuviharibu vifaraga kama ni vizima itakuwa hasara kwa nchi!!! Mpigeni faini alafu muacheni akuze vifaranga vyake alafu alipe kodi stahiki!!
 
Naona jamaa anarudi kwenye umaskini kama utani. Why asipigwe tu fine then aachiwe? Au viuzwe kwa nusu bei kwa wafugaji? Ila viliingiaje Dar na vimetoka Kenya?
 
Tuwe wakweli na wawazi je huyu aliyeingiza hao vifaranga nchini hajui kwamba kuna mambo ya kufuata kabla ya kuviingiza au anaipima serikali? Ningekuwa Mimi ningemuamuru arudishe alipo watoa halafu sheria inachukua mkondo wake
 
Vifaranga kutoka nchini Kenya vyenye thamani ya Milioni 40 vimekamatwa na mamlaka ya serekali Tanzania bila ya kua na vibali halali.
Kwa kujibu wa taarifa toka mamlaka husika Tanzania wamesema wataviteketezwa kwa mujibu wa sheria inavyotaka. Japo vifaranga hivyo havijathibitika kua na magonjwa ila kwa kua vimeingia bila kibali vitachomwa moto.

Source ;ITV
Jamani si watugaie kama samaki wa Magufuli. Wanachoma moto tena? Sasa huko ni kuadhibu viumbe wasio na hatia, sasa Kosa la vifaranga liko wapi hapo.?
 
Vifaranga kutoka nchini Kenya vyenye thamani ya Milioni 40 vimekamatwa na mamlaka ya serekali Tanzania bila ya kua na vibali halali.
Kwa kujibu wa taarifa toka mamlaka husika Tanzania wamesema wataviteketezwa kwa mujibu wa sheria inavyotaka. Japo vifaranga hivyo havijathibitika kua na magonjwa ila kwa kua vimeingia bila kibali vitachomwa moto.

Source ;ITV
Vimewakosea nini
 
Sheria ni msumeno kama katenda kosa na inajulikana wazi basi aadhibiwe kadri ya makosa asionewe wala kupendelewa...
 
Kama sheria inasema hivyo wavichome tu ili liwefundisho kwa hao wanaingiza vifaranga bila kibali.
Nadhani hao wanaoingiza vifaranga ndio wachomwe vifaranga hapo ni innocent creatures. Lakini pia sioni sababu kwa nini tuwachome na tusitaifishe wawekwe quarantine kama hawana magonjwa wauzwe kwa mnada.
 
Back
Top Bottom