Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Andika ukiwa huru bila mapepo ya chuki mkuu...

Njoo kanisani kwetu tukuombee
Kwa akili yako enzi za mwendazake, ukwepaji kodi ulikuwa hakuna? Hayo madudu ya bandari alikuwa hayupo?! Ni suala la muda tu huyu mama akiamua kweli afunue kote mlikokuwa mmefunikwa mtamuona huyo meko kumbe alikuwa hata zaidi ya JK!! Hizo ndege kila siku alikuwa anawaambia ni ma faida tu??
 
kwanza huyo mhujumu uchumi viranga tanzania viko kibao watu wanavyo wanauza kwa nini akanunue kenya?

Pili ni kuthibiti magonjwa huwezi toa viranga nchi nyingine bila vyeti bya afya na kupeleka nchi nyingine

Nchi vi apoingia haiwajibiki kuvipima ni kupiga kibititi tu Inatakiw mhusika kabla kusafirisha awe na vyeti husika toka nchi husika
 
Inashngaza
Leo wanyonge munalilia ‘Double Standard'
 
kuna mshkaji wangu aliingiza mzigo wa ml400 kimagendo 🤣🤣🤣🤣
sikuizi yupo merereni kawa mwanaapolo ili apate angalau kula!

utakua ni ujinga kuwekeza pesa yote hiyo af unakwepa kodi na kuhatarisha usalama na sovereignty ya taifa la Tanzania lakini pia biashara yake!!
 
Wacha kutuletea ujinga wako hapa, hakuna ng'ombe hai anateketezwa na moto bali ni nyama ya ng'ombe au mnyama yeyote aliyekufa mwenyewe au amechinjwa lakini nyama yake imegundulika haifai kuliwa na Binadamu. Machinjioni kila mnyama anayechinjwa kwa chakula nyama yake lazima ipimwe na mtaalamu ili kujua kama ni mzimà wa afya na salama kuliwa na Binadamu na ikikutwa haifai kabisa inatekelezwa au kama ugonjwa siyo mbaya sana inachemshwa hapohapo kwa usimamizi wa aliyepima.
acha ushamba dogo!!
duniani kote huchoma wanyama kama kumetokea pandemic ya wanyama
 
Mbona wakikamata magari hawayachomi moto wanataifusha?
Tunacoma milion 40 huku tukiendelea kutafuta walipa kodi wapya!
 
Naona jamaa anarudi kwenye umaskini kama utani. Why asipigwe tu fine then aachiwe? Au viuzwe kwa nusu bei kwa wafugaji? Ila viliingiaje Dar na vimetoka Kenya?
Hapo wapige fine ikishindikana bora wataifishe na sio kuvichoma moto
 
Tuwe wakweli na wawazi je huyu aliyeingiza hao vifaranga nchini hajui kwamba kuna mambo ya kufuata kabla ya kuviingiza au anaipima serikali? Ningekuwa Mimi ningemuamuru arudishe alipo watoa halafu sheria inachukua mkondo wake
Hapo sawa umetoa suluhisho jema na sio kuvichoma moto
 
Sheria ifate mkondo wake, hii mambo ya double standards katika kutoa adhabu haitakiwi.
Hata yeye alipokuwa anafanya hilo alijua kuwa anaweza kukamatwa mchezo ukaisha. Ila still alibeti na mkeka ushalost! Sheria zinavunjwa na watu wanaozijua kabisa ila tamaa ndio huponza watu. Afanyiwe anachostahili.

Haina tofauti sana na tunaobeti kwenye michezo kama mpira, basket n.k tunaelewa kama kuna kula na kuliwa so tunakuwaga Neutral.
Roho mbaya ni dalili ya umaskini
 
Vipigwe moto tu hakuna jinsi anaidharau serikali akileta mafua ya ndege nchini atasababisha hasara ya kiasi gani asee watumie petrol nyingi
 
Utachomaje kitu chenye uhai? Haniingii akilini

Ndiyo maana nalo lilikufa

Vinatakiwa vikabidhiwe kwa madaktari wa mifugo vipewe madawa.

Mbona gari ya shamimu na mumewe hawakuchoma moto? Ndiyo maana lile lijamaa linatafasiriwa km ni dikiteta

Atakaeyechoma moto naye afe. Ndiyo utagundua nchi za Afrika hakuna wanachoweza hata viongozi wakiumwa wanakimbilia nje za nchi na wengi huishia kufa tu
Kama sheria inasema hivyo wavichome tu ili liwefundisho kwa hao wanaingiza vifaranga bila kibali.
 
Vifaranga kutoka nchini Kenya vyenye thamani ya Milioni 40 vimekamatwa na mamlaka ya serekali Tanzania bila ya kuwa na vibali halali. Kwa kujibu wa taarifa toka mamlaka husika Tanzania wamesema wataviteketezwa kwa mujibu wa sheria inavyotaka.

Japo vifaranga hivyo havijathibitika kuwa na magonjwa ila kwa kua vimeingia bila kibali vitachomwa moto.

Source; ITV
Endeleeni kuvichoma,majibu watayapokea wafanyabiashara wa mahindi.
 
Ushauri wa buree.
1.WAVIPIME KUONA KAMA HAVINA MAGONJWA
2.MMILIKI ATOZWE KODI STAHIKI NA KA FAINI
3.VINADIWE NA SERIKALI ENDAPO MMILIKI HANA HIZO TOZO
3.VICHOMWE ENDAPO VITAKUTWA NA VIMELEA VYA MAGONJWA
 
Mbona wakikamata magari hawayachomi moto wanataifusha?
Tunacoma milion 40 huku tukiendelea kutafuta walipa kodi wapya!
Gari inasambaza magonjwa kama kuku?huwa yanaumwa kideri au mdondo kama kuku?
 
Uliwahi kuachiwa uja uzito na watu wa chadema nini?maana mimi sijataja chadema ila wewe tayari unakimbilia chadema. Kama mwanaume mmoja alikutenda wa chadema usichukie wote.😂
 
Vifaranga hawana hatia, aadhibiwe mhusika, vifaranga wapimwe kujiridhisha kama wanafaa kuwepo nchini au warejeshwe walikotoka, kuna amri ya Mungu isemayo "usiue"
Hii ndio Tanzania. Kumbuka swala la yule mbwa aliyeitwa Immigration
 
Taarifa ya Habari ya ITV ya leo imeonesha mfanyabiasha wa Ukonga aliyeingiza vifaranga vyenye thamani ya milioni 40 kutoka Kenya bila kufuata utaratibu.

Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa kulingana na sheria ni kubinafsisha mali na kuteketeza vifaranga wote kwa mujibu wa sheria.

Je, kipi bora kumuita mfanyabiasha ukampiga faini pia akalipia gharama za kuhakiki usalama wa vifaranga(kwa afya ya binadamu) alafu umrudishie vifaranga? Au ukateketeza mtaji au fedha milioni 40?
Mzimu wa Magufuli unatuandama
 
Back
Top Bottom